Dawa za Asili za Mimea (Kuzuia Wadudu Waharibifu wa Mazao) - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Thursday, September 28, 2017

Dawa za Asili za Mimea (Kuzuia Wadudu Waharibifu wa Mazao)

Unaweza kutumia mimea fulani kupunguza idadi ya wadudu waharibifu shambani mwako. Panda mimea ambayo huepukwa na wadudu waharibifu karibu na mimea inayohitaji kulindwa. Kwa mfano, minyoo fulani ambayo hula na kudhoofisha mizizi ya mimea mingi haiwezi kukaribia mimea ya matageta. Na vipepeo fulani ambao huharibu kabichi hawakaribii kabichi zilizopandwa karibu na mimea ya rosemary, sage, au thyme.Hata hivyo, tahadhari hii yafaa: Mimea fulani huwavutia wadudu waharibifu.
JINA TIBA UTUMIAJI
Mnyaa Kuua Mchwa Matone 10 ya mnyaa + maji lita moja. Koroga. Nyunyuzia/ Pulizia kwenye mchwa
Utupa Wadudu wanaoshambulia mboga Twanga kiganja kimoja cha majani. Loweka kwenye lita 1 ya maji kwa masaa 24. Chuja. Ongeza 1/8 ya kipande cha mche wa sabuni. Pulizia kwenye mboga
Muarobaini – Majani Wadudu wa mboga Ponda ganja mkona 1 wa majani. Changanya kwenye lita 1 ya maji. Loweka kwa siku mbili , halafu ongeza sabuni 1/8 ya kipande mche. Nyunyuzia kwenye mboga.
Muarobaini - Mbegu Wadudu wanaoshambulia mboga Twanga mbegu kilo 5 (kisado kimajo). Loweka kwenye maji lita 15 kwa masaa 24. Chuja na pulizia/ nyunyuzia kwenye mboga
Papai Kuua mchwa Ponda majani laini ya mpapai. Ongeza lita 1 ya maji. Chuja na pulizia/ nyunyuzia kwenye mchwa
Bangi Mwitu Kuhifadhi vyakula vya nafaka (food grains) Sambaza halafu weka gunia juu yake. Endelea hivyo hivyo.
Mkojo wa n’gombe Kuua mchwa/ wadudu wa mboga Uache mkojo kwa siku 10 –14. Kwa kila lita 1 ya mkojo ongeza lita 2 za maji na 1/8 sabuni ya mche. Nyunyuzia kwenye mchwa au mboga
Mnanaa (mbarika mwitu) Kuua wadudu wanaoshambulia mboga Gram 100 mbegu + lita 1 maji + 1/8 sabuni mche. Pulizia/ nyunyizia kwenye mboga
Kitunguu saumu Kuua wadudu wanaoshambulia mboga Gram 100 (3-4) twanga. Ongezea lita 1 ya maji. Acha kwa saa 24. Chuja na ongeza 1/8 ya kipande cha mche wa sabuni. Pulizia/ Nyunyuzia kwenye wadudu
Pilipili Kali Kuua wadudu kwenye mboga Changanya vijiko 3 vya chakula na lita 1 ya maji. Acha kwa saa 12. Ongezea 1/8 ya kipande cha sabuni mche. Nyunyizia kwenye mimea
Mashona nguo Kuua wadudu Chemsha mbegu kikombe 1 na lita 1 ya maji kwa dakika 10 au loweka siku moja na ongezea 1/8 ya kipande cha sabuni mche. Nyunyuzia kwenye mboga
Muarobaini Kideri (New Castle disease) Twanga majani 1kg, ongeza maji lita 1. Wanyweshe kuku asubui. Fanya hivi kila mwezi
Majivu Kuua wadudu mafuta (aphids) Nyunyizia majivu kwenye wadudu wanaoshambulia mboga
Majivu Kuhifadhi mazao Changanya majivu + pilipili kichaa + Cyprus. Sambaza kwenye gunia halafu weka gunia juu yake. Endelea hivyo hivyo.
Marejea Mbolea Panda shambani na baadaye limia chini ardhini

No comments:

Post a Comment