NDUI YA KUKU
Ndui ni ugonjwa unaosababishwa na virus aina ya avipoxvirus ambao hushambulia zaidi kuku na jamii yote ya ndege,katika umri wowote wa kuku ndui inaweza ikampata kuku.virus aina ya avipoxvirus.
Virusi hivi vya Ndui husambaa kwa njia nyingi yaweza ikiwemo.
- Kwa njia ya kuku kudonoana.
- Kupitia ndege wa porini kwa kuingiliana vyombo vya maji na chakula.
- Pia vyombo vya maji na chakula vinavyo chafuliwa na kuku mwenye vimelea vya ugonjwa wa ndui.
- Pia maabukizi ya virus vya ugonjwa wa ndui kwa kuku husababisha kuku kudumaa na kua na ukuaji usio mzuri,kuku hupunguza kiwango cha utagaji.
- Pia virus avipoxvirus vinaweza kuishi katika mazingira kwa mda mrefu.
DALILI ZA UGONJWA WA NDUI
1. Hushambulia zaidi sehemu zilizo wazi zisizo na manyonya kwa uwepo wa vinundu(viuvimbe)vya rangi ya kahawia.
2.Kupumua kwa shida,macho ya kuku kuonekana kusinzia na kuwa na mfano wa kitu cheupe kwenye jicho,
3.Utando mweupe mdomoni,vifo vinaweza kufikia hadi 50%.
Jinsi Ya Kuuzuia Maambukuzi Na Husambaaji Wa Virusi Vya Ugonjwa Huu.
Kinga na tiba.
Ugonjwa wa ndui hauna tiba unashauriwa kuchanja kuku wako mapema hasa kipindi cha miezi ya joto wachanje wakiwa na umri wa wiki 6 hadi wiki8 , tenga kuku wanao umwa ili kuzuia maambukizo kuenea.
Fukia au choma mizoga yote iliyo kufa kwa ugonjwa.
Kuku anae umwa mpatie vitamini pamoja na glucose ili kupunguza makali ya ugonjwa,pia tumia antibiotic ili kuzuia maambukizi mapya yanayo weza kujitokea.
Mambo Yakuzingatia Katika Kuzuia Magonjwa Katika Kuku.
- Hakikisha unawapatia chanjo zote za muhimu katika uzuiaji wa magonjwa yanayosambazwa na virusi kwani magonjwa haya hayana tiba endapo pale yanapo kuwa yamewapata kuku, ikiwemo, ndui ya kuku, mdonde na gumboro. Vifo vingi hutokea hatimae mradi kuyumba.
Ndugu mfugaji ofa Bado inaendelea Bado nafasi ya Mtu mmoja kutukabizi mradi wake ili tuusimamie kwa miezi5 kwa sh 20000. Wahi kuchukua nafasi hii ilikuwa sh 50000 kwa miezi mitano ila ofa ni sh 20000 tu nafasi Bado moja kwa mawasiliano Zaidi whatsapp namba
0655610894.
TEMBELEA BLOG HII KILA SIKU
No comments:
Post a Comment