KUKU KUDONOANA - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Tuesday, May 23, 2017

KUKU KUDONOANA

                                                             
KUKU KUDONOANA "Cannibalism,"


Kudonoana kwa kuku ni tatizo linalo wa sumbua wengi, ni moja ya athari ya lishe duni. Ni kisema lishe duni na maanisha chakula wanacho kula kukosa vurutubisho muhimu vya madini au kuku kutokula chakula cha kutosha.

Hizi ni moja ya sababu zinazo pelekea kuku kudonoana.

1.Kuku kukaa wengi kwenye eneo dogo
2.Upaguzi wa rangi👇
    
    Hii Mara nyingi hutokea kwa kuku weusi ukiwachanganya na kuku mweupe au rangi ingine tofauti, kuku weusi Mara nyingi huwa ni wakali sana Kwahiyo ukiona kuku bandani kwako kadonolewa chunguza kwa makini chanzo ninini! Kama ni ubaguzi wa rangi unaweza watenga hao weusi.
 3. Kuku kutokupata chakula cha kutosha
4.Upungufu wa madini

5. Kukosa kitu walicho kizoea👇

       Kwa mfano kuku ukiwazoesha kuwa changanyia Damu kwenye chakula , siku utakapo punguza kipimo au kuacha kabisa kuwa changanyia  damu  ambayo umewazoesha kuwa changanyia lazima watadonoana.👇

Kuku ukiwa zoesha kuwa fungia mchicha hasa wale kuanzia  mwezi mmoja hadi wa miezi 4  siku utakapo acha kuwafungia mchicha inaweza sababisha wakadonoana.

6. Mwanga mkali

7. Uhaba wa vyombo bandani👇

     Hii hutokana na kuwa na kuku wengi harafu vyombo vichache vya chakula , Kwahiyo wakati wa kula lazima watadonoana

Tiba Kinga

_ Hakikisha kwenye chakula cha kuku wako kuwepo na virutubisho vya madini. Mara nyingi vitu vinavyo tokana na wanyama ni vyanzo vizuri vya madini.

 _Hakikisha kuku wako wanakaa kwenye eneo la kutosha . hii inategemea  aina ya kuku na umri wake.

_Kata midomo

_ Mifupa , chokaa na Damu hivi vitu vinatakiwa viwepo kwenye chakula cha kuku wako  kwa kipimo maalumu. Ukiweka Damu zingatia kama nilivyo elezea hapo juu. "Pia kumbuka virutubisho vinahitajika kwenye chakula hutegemea na aina ya kuku"✅

_ Hakikisha kuku wako wana kula chakula cha kutosha, simaanishi wale sanaaa mpaka waache  hapana! "Ila hakikisha wanashiba"✅

_ Wafanye kuku wako wawe wenye furaha , kwa kuwawekea vifaa vya michezo  bembea. Pia wafungie mchicha ili wawe bize na kuudonoa huo. Unaweza wafungia mchicha, kabeji nk   mboga za majani ni chanjo kizuri cha vitamn.

Ahsante

FUGAKIBIASHARA INAWATAKIA UFUGAJI MWEMA.

USISAHAU KU DOWNLOAD APP YA KILIMO BORA IPO PLAY STORE

BONYEZA HAPA KUPAKUA;

                              

Tembelea blog hii kila siku

No comments:

Post a Comment