KIBANDA CHA KUFUGIA
Tunasaidia kwenye ujenzi wa vibanda bora vya sungura, kwagharama ya Tshs 65,000/= tu kwa kimoja cha ukubwa wa futi 2.53 , chenye uwezo wa kufugia Sungura mmoja mkubwa wakuzalisha pamoja na watoto wake kwa mwezi mmoja baada yakuzaliwa yaani kipindi chote cha unyonyeshwaji, na kibanda cha saizi hiyo pia kinaweza kufugia hadi sungura kumi wa umri wa miezi mitatu.
Tunashauri ujenzi wa vibanda vitatu kwa kila jike (kupata nafasi ya watoto wanaomaliza kunyonya kwani jike huzaa kila baada ya miezi 2) na pia kibanda kimoja kwa kila dume.
MBEGU
Tunawataka wakulima wetu kufuga mbegu bora na halisi ya sungura watakaotupa nyama bora kwa soko letu, na tunawauzia kwa gharama ya Tshs 80,000/= kwa kila jike aliyetayari kubeba mimba na Tshs 40,000/= kwa kila dume mwenye umri wakuzalisha.
MAFUNZO YETU
Tuna mafunzo mara kwa mara pia, na zaidi kuhusu ujezi wa mabanda bora, Utunzaji na ufugaji kwa ujumla, na kuhusiana na maswala ya magonjwa na namna yakuzuia.
Tuna saini mkataba na mkulima/mfugaji (kwa ada maalum kila mwaka) ambao utamuhakikishia mfugaji/mkulima soko kwa kipindi chote cha mkataba pale sungura wake wanapokuwa tayari kwa kuuzwa.
Tunanunua sungura katika umri wa miezi 4-5. Kwa umri huo sungura mwenye afya aliyelishwa vizuri anapaswa kuwa na uzito wa kilo 3-4, na kilo moja ya sungura akiwa hai tunamnunua kwa Tshs8,000/=.
ENDELEA KUTEMBELEA BLOG HII KILA SIKU AU PAKUA APP YETU
No comments:
Post a Comment