Mahitaji ya hali ya hewa na udongo
Zao hili hupendelea hali ya hewa ya baridi na udongo tifu tifu na wenye rutuba. Sehemu
nyingi zinazostawi vitunguu maji hufaa pia kwa zao hili. Maeneo ya mwinuko wa kiasi
cha zaidi ya mita 1000 juu ya usawa wa bahari hufaa zaidi
Maandalizi ya shamba
Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sen-
timita 30 hadi 45 Weka matuta ya mwinuko yenye upana wa mita 1 hadi mita 1.5 kutoka kati kati ya
tuta na tuta na upana wa mita 1
Maandalizi ya Mbegu
Kwanyua vipande/Vikonyo vya vitunguu sumu tayari kwa ajili ya kupanda katika nafasi. Mbegu sharti iwe imekaa kwa miezi mitano hadi sita tangu kuvuna ili iweze kuota. Ni muhimu kwa mkulima kupata ushauri wa kitaalam ili kujua namna ya kutam- bua mbegu ya vitunguu saumu iliyo tayari kwa kupanda kwani ikipandwa kabla haijawa tayari haioti
Upandikizaji
Tumia mashine alama kuweka alama za kupandia katika nafasi ya sentimita 15 hadi sentimita 25 na mistari minne hadi sita kwa tuta Hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda
Palizi
Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu Magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu.
Mbolea
Tumia mbolea ya DAP wakati wa kupanda, CAN ama SA wiki tatu baadaye na kisha tumia NPK wiki sita baada ya kupanda. Matumizi ya mbolea za maji yafanyike kila baada ya wiki mbili kutegemea na mahitaji.
Matumizi ya viuatilifu
Matumizi ya viuatilifu yafanyike kila baada ya wiki mbili kwa ushauri wa wataalam
Mavuno
Vitunguu saumu hukomaa miezi 6 tangu kupanda
Bei ya mbegu hizi ni tsh 30,000/= kwa kopo la lita moja(1) na tsh 600,000/= kwa ndoo ya lita ishirini.
Guarantee: Ndoo ya lita 20 ambayo ni sawa na makopo 20 ya lita moja inatosha kupanda eneo la hekari 1 (m70*m70) na kiwango cha chini cha mavuno ni gunia 100 na kiwango cha juu ni gunia 110-120 ndani ya siku 90 (3 months) toka kupanda. Gunia moja sokoni kariakoo, ilala, buguruni, temeke na mabibo kwa sasa bei ni tsh 130,000/= * gunia 100 = tshs 13,000,000/= ndani ya miezi 3

Kilimo cha Nyanya Chungu
Zao hili pia hujulikana kwa jina la "Nyanya Chungu", "Ngogwe" au "Ntongo". Huu ni mmea wa kitropiki, na kustawi kwake karibu ni sawa na bilinganya.
Mmea hukua na kufikia urefu wa meta moja hadi moja na unusu na matawi na majani yake hufanya kichaka. Nyanya mshumaa zinaweza kuwekwa katika makundi mawili: yaani aina itoayo matunda madogo madogo na machungu sana na aina itoayo matunda makubwa na machungu kidogo.
Rangi ya matunda huwa kijani kibichi au kijani-njano, au njano-nyeupe, na yakipevuka kabisa hugeuka mekundu. Matunda yafikia hatua ya kupevuka huwa hayafai tena kuliwa, ila kwa kutoa mbegu za kupanda. Matunda hupikwa au kukaangwa na kufanywa mchuzi, au huchanganywa na mboga zingine. Pia hupikwa pamoja na ndi.
Kupanda: Miche huoteshwa kwa kupanda mbegu ambayo husiwa kwenye kitalu na kutunzwa kama mazao mengine. Miche ifikiapo kimo cha sentimeta 10 hadi 15 au majani manne 4 hupandikizwa bustanini , kwa umbali wa sentimita 50 kwa 75 au sentimeta 90 kwa 90, hadi 120 kwa 120; hii kutegemeana na ukubwa wa kichaka chake. Mimea ya "Ngogwe" hutunzwa kama bilinganya, huhitaji ardhi yenye rutuba na unyevu wa kutosha. Mazao huanza kuvunwa miezi miwili baada ya kupandikizwa, na uvunaji huendelea kwa muda mrefu kidogo.
Maadui: Nyanya Mshumaa ni mmea mgumu, kwani unaweza kustahimili upungufu wa maji kuliko aina nyingine za Mboga. Vile vile haushambuliwi sana na baadhi ya Magonjwa
yasababishwayo na mvua au uchepechepe mkubwa. Ingawa yako magonjwa na wadudu ambao hushambulia zao hili, madhara ya si makubwa sana kiasi cha kutisha au kumkatisha tamaa mkulima. Usafi wa bustani na kubadilisha mpando wa mazao, vinaweza kuondoa tishio hilo.
Kuvuna: Mboga huvunwa wakati zikiwa bado mbichi. Ili ziweze kukaa kwa muda mrefu (hata majuma mawili) bila kuharibika, inapendekezwa kuzichuma pamoja na sehemu ya vikonyo vyake. Vikonyo hivyo hukobolewa wakati wa kuzitayarisha kupikwa. Kwa hiyo, zao hili linaweza kusafirishwa hadi masoko ya mbali bila kuharibika.
Mkulima ongeza uzalishaji katika mazao ya mboga mboga ukuze uchumi wako.
NB: Umbali wa cm 50 kwa cm 75 ni mzuri sana kwa kuwa unaweza kupata mazao mengi na kupunguza wingi wa magugu ukizingatia in cover crop ila lazima uhakikishe ardhi yako ipo vizuri kwa rutuba maana matumizi ya mbolea ni amakubwa.

No comments:
Post a Comment