AINA
Mchanganyiko; za kienyeji (ndogo) na za kigeni ( kubwa)
HALI YA HEWA NA UDONGO
KUSIA MBEGU KWENYE VITALU
UTUNZAJI
KUVUNA
MATUMIZI
JINSI YA KUTUMIA
MANUFAA
Mchanganyiko; za kienyeji (ndogo) na za kigeni ( kubwa)
HALI YA HEWA NA UDONGO
- Mvua nyingi za kutosha 2000mm -2500mm kwa mwaka
- Udongo wenye rutuba
- Joto kwa wingi
- Hewa yenye unyevunyevu
KUSIA MBEGU KWENYE VITALU
- Mbegu hupatikana kwenye miti iliyokomaa
- Sia mbegu kwenye kitalu zikiwa nusu sentimeta chini ya udongo
- Baada ya kuchipua, mbegu huchukua miezi 6 hadi mwaka mmoja kufikia umri wa kupandikiza shambani
- Panda miche wakati wa masika
- Panda kwa nafasi ya 2m x2m. Nafasi hizi huwezesha miti kutoa machipukizi mengi. Nafasi kubwa hufanya miti kuwa na matawi mengi pia mashina hayanenepi wala kurefuka
UTUNZAJI
- Acha machipukizi kwenye shina
- Toa matawi kwenye mashina ili kunenepesha mashina
- Weka shamba katika hali ya safi
- Zuia magonjwa kama.
- Vinundu (galls)wanaosababishwa na utitiri na wadudu scales na mealbugs kwa kutumia dawa za sumu kama Selecron, Karate nk.
KUVUNA
- Anza kuvuna miaka 3 baada ya kupanda
- Mazao ya mdalasini ni maganda ya mashina ya miti
- Kata shina la mti,na tenganisha maganda na mti kwa njia ya kumenya
- Kuwa mwangalifu ili ganda litoke vizuri bila kupasukapasuka
- Seli za nje ya ganda la mdalasini ni chungu hivyo ni vizuri ziondolewe kwa kukaruza kwa kisu
- Kausha vizuri siyo kwenye jua kali Mavuno
- 0.25 kg – 10kg maganda yaliyokaushwa kwa mti mmoja. Kiasi cha mazao hutegemea ukubwa na umri wa mti
- Ubora wa mdalasini hushuka kulingana na umri wa mti. Mti wa umri mkubwa hutoa mganda yenye ubora wa chini
MATUMIZI
- Mdalasini baada ya kukaushwa ikiwa umesagwa au bila kusagwa hutumika kama:
- Kiungo kwenye chakula na vitafunwa kama keki, mandazi,vitumbua
- Vikolezo kwenye vinjwaji km. chai, kahawa
- Dawa ya tumbo hasa wakati wa kuvimbiwa, kutoa hewa tumboni pia kuongeza hamu ya chakula
- Dawa ya ngozi
JINSI YA KUTUMIA
- kiungo kwenye chakula
- Tumia maganda au saga magada yaliyokauka. Tumia ili kuongeza ladha kwenye vyakula kama pilau, ndizi, mchuzi nk
- Kutengenezea kinywaji
- Weka vipanda vichache 2-3 (30gm) vya maganda kwenye kikombe ongeza maji yanayochemka, funika kwa dakika 15, ongeza vipande vya limao. Kunywa kila baada ya kula
MANUFAA
- Miti hudumu shambani zaidi ya miaka 20. Miti huchipua na kutoa machipukizi mengine kila baada ya kuvuna
- Gharama ndogo ya uzalishaji
- Mazao yaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu
- Magonjwa na wadudu ni kidogo
- Rahisi kuchanganya na mazao mengine
- Nguvu kidogo, kipato kikubwa.
No comments:
Post a Comment