KILIMO CHA MBOGAMBOGA ( HORTICULTURE ) - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Thursday, June 15, 2017

KILIMO CHA MBOGAMBOGA ( HORTICULTURE )


Hiki ni kilimo ambacho ni cha muda mfupi ambacho ni bora zaidi kukitumia ili kujaribu kuepukana na umaskini. kilimo cha mbogamboga ni bora zaidi sababu asilimia 95% duniani hutumia mboga na matunda ili kujenga mwili na kuutia mwili joto. mboga mboga husaidia kutubatia vitamini A kwa ajili ya kuona vizur na pia vitaminK.
     SALADI
Ni mboga ambayo hulimwa sana kanda ya kaskazini mwa tanzania kama Arusha, Tanga, Kilimanjaro,na Manyara. mboga hii huhimili ukame na pia huchukua muda mfupi kukomaa pindi inapooteshwa. kwa mkoa wa Tanga wakulima wengi ndani ya wilaya ya Lushoto huliza zao hili kwa ajili ya biashara ili kujipatia kipato kwa muda mfupi.

 saladi ambayo ipo karibu kukomaa na kuvunwa tayari kwa kutumiwa kama chakulaa na binadamu

      KITALU
mbegu hii ni vyema iandaliwe kwenye kitalu kabla ya kwenda kuoteshwa shambani.kitalu kinatakiwa kuwa sehem nzur yenye maji ya kutosha na udongo mlainim wenye rutba nzuri. mbegu inatakiwa isiwe vizur na kufunikwa na udongo kidogo na majani makavuu juu ili kuzui jua kupenyeza hadi kwenye mbegu. kitalu kinatakiwa kiwe sehem ya bondeni yenye kivuli kwa mbali

   KUOTESHA
mboga hii huoteshwa kwenye umbali wa sentimita 15x15 shina na shina na mstari kwa mstari sentimita20. huoteshwa kwenye udongo wa aina yoyote na hukua vizur bila tatizo lolote

    MBOLEA
mbolea zinazotakiwa kutumika kupandia ni mbolea za mboji ili kuongeza urutubishaji wa aridhi. mbolea za chumvi chumvi husababisha kupoteza ubora wa aridh kwa muda mfupi na pia kufanya mazao kutokua na ubora mzuri. mfano wa mbolea za kupandia za chumvichumvi ni NPK, DAP, TSP,  na mbolea za kukuzia ni kama UREA CAN BUSTER hizi husaidia kuupa nguvu mmea ili kukua kwa haraka na kuvutia pia

    PALIZI
ni vyema kufanya palizi mapema tu unapoona magugu yanapokua ili kuondoa ushindani kti ya mmea na magugu katika kuwania virutubisho ndani ya aridhi

    KUKOMAA/KUVUNWA
zao la saladi hukomaa kwa siku 50-60 tangu kuoteshwa shambani baada ya kuhamishwa kutoka kwenye kitaluu. pia wakati wa kuvunwa lazima uangalie kama imejaza vizuri katikati kwenye tunda lake.
        asnteni kwa ushirikiano wenu

USISAHAU KUDOWNLOAD APPLICATION YA KILIMO BORA IPO PLAY STORE

                                      DOWNLOAD HAPA SASA

                     

No comments:

Post a Comment