Kilimo cha Nyanya Chungu - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Friday, June 30, 2017

Kilimo cha Nyanya Chungu

 Zao hili pia hujulikana kwa jina la "Nyanya Chungu", "Ngogwe" au "Ntongo". Huu ni mmea wa kitropiki, na kustawi kwake karibu ni sawa na bilinganya.

Mmea hukua na kufikia urefu wa meta moja hadi moja na unusu na matawi na majani yake hufanya kichaka. Nyanya mshumaa zinaweza kuwekwa katika makundi mawili: yaani aina itoayo matunda madogo madogo na machungu sana na aina itoayo matunda makubwa na machungu kidogo.

Rangi ya matunda huwa kijani kibichi au kijani-njano, au njano-nyeupe, na yakipevuka kabisa hugeuka mekundu. Matunda yafikia hatua ya kupevuka huwa hayafai tena kuliwa, ila kwa kutoa mbegu za kupanda. Matunda hupikwa au kukaangwa na kufanywa mchuzi, au huchanganywa na mboga zingine. Pia hupikwa pamoja na ndi.

Kupanda: Miche huoteshwa kwa kupanda mbegu ambayo husiwa kwenye kitalu na kutunzwa kama mazao mengine. Miche ifikiapo kimo cha sentimeta 10 hadi 15 au majani manne 4 hupandikizwa bustanini , kwa umbali wa sentimita 50 kwa 75 au  sentimeta 90 kwa 90, hadi 120 kwa 120; hii kutegemeana na ukubwa wa kichaka chake. Mimea ya "Ngogwe" hutunzwa kama bilinganya, huhitaji ardhi yenye rutuba na unyevu wa kutosha. Mazao huanza kuvunwa miezi miwili baada ya kupandikizwa, na uvunaji huendelea kwa muda mrefu kidogo.

Maadui: Nyanya Mshumaa ni mmea mgumu, kwani unaweza kustahimili upungufu wa maji kuliko aina nyingine za Mboga. Vile vile haushambuliwi sana na baadhi ya Magonjwa
yasababishwayo na mvua au uchepechepe mkubwa. Ingawa yako magonjwa na wadudu ambao hushambulia zao hili, madhara ya si makubwa sana kiasi cha kutisha au kumkatisha tamaa mkulima. Usafi wa bustani na kubadilisha mpando wa mazao, vinaweza kuondoa tishio hilo.

Kuvuna: Mboga huvunwa wakati zikiwa bado mbichi. Ili ziweze kukaa kwa muda mrefu (hata majuma mawili) bila kuharibika, inapendekezwa kuzichuma pamoja na sehemu ya vikonyo vyake. Vikonyo hivyo hukobolewa wakati wa kuzitayarisha kupikwa. Kwa hiyo, zao hili linaweza kusafirishwa hadi masoko ya mbali bila kuharibika.

Mkulima ongeza uzalishaji katika mazao ya mboga mboga ukuze uchumi wako.

NB: Umbali wa cm 50 kwa cm 75 ni mzuri sana kwa kuwa unaweza kupata mazao mengi na kupunguza wingi wa magugu ukizingatia in cover crop ila lazima uhakikishe ardhi yako ipo vizuri kwa rutuba maana matumizi ya mbolea ni amakubwa.

No comments:

Post a Comment