UTANGULIZI
Mihogo ni zao
muhimu sana kwa chakula kwa nchi nyingi za Afrika na Amerika ya kusini. Kwa mara ya kwanza zao hili lililetwa na wareno, hapa Afrika. Zao hili hulimwa nchi zaidi ya 34 za Afrika kwenye hekari zaidi ya ekari milioni 200. Kilimo cha mihogo huhitaji ujuzi kidogo sana na ni rahisi kulima. Zao hili hustahimili ukame na huweza kubakia ardhini kwa muda mrefu kuepukana na baa la njaa. Upatikanaji wa mavuno ni wa uhakika kuliko mazao ya nafaka. Mizizi ya mihogo ndio tegemeo kubwa la wakulima. Mihogo huwa na kiasi kikubwa sana cha VITAMINI ‘A’ na kiasi kidogo cha protini. Ulaji wa mihogo huwasaidia walaji kuepukana na ugonjwa wa ukavu macho. Pia majani ya mihogo huweza kutumika kama mboga za majani (KISAMVU). Kuna kemikali iitwayo CYNOGENIC GLUCOSIDE ambayo inaweza kuwa sumu kama mihogo isipoandaliwa vizuri. Mihogo mitamu ina kiasi kidogo sana cha kemikali hii na huweza kuliwa hata Mibichi.
HALI YA HEWA, UDONGO NA MAHITAJI YA MAJI
Kwenye ukanda wa Ikweta zao hili hulimwa hadi mita 1500 kutoka usawa wa bahari. Halijoto ya 20-30° hufaa kwa kilimo cha mihogo. Zao hili halistahimili maji yaliyotuama na hupendelea zaidi jua la kutosha. Mihogo huzaa vizuri kwenye udongo tifutifu-kichanga wenye rutuba ya kutosha. Pia huweza kuzalishwa kwenye sehemu iliyoathirika na mmomonyoko wa udongo ambapo mazao mengine hayasitawi. Rutuba ikizidi sana ardhini mihogo huwa na majani mengi sana na mizizi kidogo.
UPANDAJI WA MIHOGOKupanda mihogo kwa kutumia mihogo iliyohifadhiwa haiwezekani kwa sababu mizizi haina vichipukizi. Mihogo inapandwa kwa kutumia pingili za shina lake zenye urefu wa sm 20-30 na upana wa sm 2-2.5. Vipingili vizuri ni vile vitokanavyo na sehemu ya shina iliyokomaa vizuri. Mimea kwa ajili ya mbegu inatakiwa iwe na umri wa miezi 8-14. Kadiri mimea inavyokuwa na umri mkubwa ubora wake wa kuzalisha mbegu huongezeka. Pia pingili ndefu ni nzuri kuliko pingili fupi. Mimea yenye afya nzuri tuu itumike kwa ajili ya pingili. Kama zimeathirika kidogo zinaweza kutibiwa kwa kuzizamisha kwenye maji yenye joto la 50° kwa dakika 15 kabla ya kupanda.
Baada ya kukatwa vipingili visikae muda mrefu zaidi ya siku mbili. Huweza kupandwa kwa kusimamishwa, kuinamishwa kidogo ama kwa mlalo. Wakati wa kupanda EPUKA kugeuza vipingili juu chini kwani mihogo itazaa kidogo sana.
NAFASI ZA UPANDAJIKama mimea inapandwa peke yake nafasi huwa si sawa endapo ikipandwa pamoja na mazao mengine. Kama mihogo ikipandwa peke yake nafasi kutoka mmea hadi mmea ni mita 1. Kwahiyo kwa eka, vipingili 4000 vinatosha. Sehemu nzuri ya kupanda mihogo ni sehemu yenye muinuko kiasi isiyotuamisha maji. Sehemu inayotuamisha maji mihogo hushindwa kutoa mizizi yenye afya.
UTUNZAJI WA SHAMBAShamba lilpaliliwe kila baada ya wiki 3-4 mpaka zifikie muda wa miezi 2-3 tangu kupanda. Baada ya hapo mimea inaweza kufunika na kuzuiya magugu yenyewe kwahiyo kupalilia sio muhimu sana. Kama shamba halina rutuba ya kutosha, mbolea ya samadi inafaa na mkulima anashauriwa kuongeza majivu kama ukuaji si mzuri, majani kuwa ya giza na vialama vya kahawia kwenye majani. Kutandazia shamba ni muhimu sana.
MZUNGUKO/MCHANGANYO WA MAZAOMazao ya mikunde kama karanga, kunde, hufaa sana kupanda pamoja na mihogo kwani huongeza rutuba ya udongo. Pia kuchanganya mihogo na mimea mingine husaidia kuthibiti mmomonyoko wa udongo.
MAGONJWA YA MIHOGO
African Cassava Mosaic Disease (ACMD)
Ugojwa huu ni ugonjwa hatari zaidi wa mihogo hapa barani Afrika na umeenea sehemu zote zizolima mihogo Africa. Husababishwa na kupanda vipingili vilivyoathirika na waduduweupe wa mihogo. Husababisha hasara ya zaidi ya asilimia 90%.
DALILI ZA UGONJWADalili za awali za ugonjwa huu ni muonekano wa michirizi meupe hasahasa kwenye majani.
NINI CHA KUFANYA
- Tumia vipandikizi visivyo na ugojwa huu. Inashauriwa kutumia vipingili kutoka kwenye matawi ya mihogo na siyo kwenye shina kubwa kwani uwezekano wa kuwa na ugunjwa huuu ni mkubwa kwenye shina kuliko matawi.
- Tumia aina za mihogo inayostahimili ugonjwa huu kama ( SS 4, TMS 60142, TMS 30337 and TMS 30572).
CASSAVA BACTERIAL BLIGHT (Xanthomonas campestris Pv. Manihotis)
(MNYAUKO BACTERIA)
Ugonjwa huu ni kizuizi kikubwa cha kuzalisha mihogo hapa Afrika.
DALILI
Mwanzoni ugonjwa huu huonekana kwenye majani, ambapo huonekana kama yameloweshwa na maji. Ugonjwa ukishamiri majani huanza kudondoka. Wakati wa unyevu unyevu bacteria hutoa uchafu kama gundi chini ya majani.Ugonjwa huu huenezwa sana kwa kutumia vapandikizi vilivyoathirika na pia matone ya mvua. Wadudu kama panzi hueneza ugojwa huu pia. Mkulima pia huweza kueneza huu ugojwa akipita shambani wakati ama baada tuu ya mvua.
NINI CH A KUFANYA
(MNYAUKO BACTERIA)
Ugonjwa huu ni kizuizi kikubwa cha kuzalisha mihogo hapa Afrika.
DALILI
Mwanzoni ugonjwa huu huonekana kwenye majani, ambapo huonekana kama yameloweshwa na maji. Ugonjwa ukishamiri majani huanza kudondoka. Wakati wa unyevu unyevu bacteria hutoa uchafu kama gundi chini ya majani.Ugonjwa huu huenezwa sana kwa kutumia vapandikizi vilivyoathirika na pia matone ya mvua. Wadudu kama panzi hueneza ugojwa huu pia. Mkulima pia huweza kueneza huu ugojwa akipita shambani wakati ama baada tuu ya mvua.
NINI CH A KUFANYA
- Tumia vipandikizi salama visivyo na ugojwa huu.
- Inashauriwa kuchanganya mihogo na mahindi ama tikiti maji ili kupunguza ugojwa huu.
- Fanya mzunguko wa mazao na ikiwezekana pumzisha ardhi.
- Ondoa na choma mimea yote na magugu shambani ama kwatua na kuyafukia chini ya ardhi
BROWN LEAF SPOT (Cercosporidium henningsii) UGONJWA MADOA YA MAJANI.
Majani yaliyokomaa tuu ndio yanayoonyesha dalili za ugojwa huu. Majani huonekana na madoa ya kahawia, baada ya muda huwa njano na mwisho kudondoka
Majani yaliyokomaa tuu ndio yanayoonyesha dalili za ugojwa huu. Majani huonekana na madoa ya kahawia, baada ya muda huwa njano na mwisho kudondoka
CASSAVA BROWN STREAK VIRUS DISEASE (Potyvirus - Potyviridae)
Ugonjwa huu ni hatari zaidi ukanda wa pwani na Zanzibar na huenezwa na wadudu weupe wa mihogo na pia kwa kupanda vipingili vilivyo na ugonjwa huu. Majani huonekana ya njano ila wakati mwingine majani huweza kuonekana yana afya nzuri wakati mizizi imeshaoza sana.
No comments:
Post a Comment