1. HISTORIA, UMUHIMU NA AINA ZA SOYA
Historia ya zao la Soya nchini Tanzania
Soya au Soybean (kwa kiingereza) ni zao la jamii ya mikunde. Kwa kitaalam linaitwa Glycine max.
Zao hilo asili yake ni nchi ya China ambako lilianza kulimwa takribani miaka 4800 iliyopita. Zao la soya liliingizwa nchini Tanzania mwaka wa 1907 katika maeneo ya Amani mkoani Tanga. Kati ya miaka ya 1930 na 1960, kilimo cha soya kilipanuka na kuenea hadi maeneo ya Nachingwea mkoa wa Mtwara, Kilosa mkoa wa Morogoro na Peramiho mkoa wa Ruvuma. Kuenea kwa zao hilo katika maeneo hayo kulitokana na msukumo wa mashirika ya Overseas Food Co-operation – (OFC), State Trading Cooperation (STC), General Agricultural Production for Export – (GAPEX) naNational Milling Corporation – (NMC). Mashirika hayo yalisafi risha soya kwenda katika nchi za Japan na Singapore. Kwa kuwa uzalishaji wa zao hilo katika mikoa hiyo ulilenga soko la nje, wananchi hawakufundishwa matumizi yake na kwa sababu hiyo baada ya mashirika hayo kuacha biashara ya zao hilo kilimo cha soya kilifi fi a hadi mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990 ambapo uzalishaji ulianza tena baada ya jamii kuhamasika katika matumizi ya soya hasa katika kutengeneza vyakula vya watoto.
Umuhimu wa zao la Soya
Soya iliyokomaa |
Zifuatazo ni faida za kutumia soya:-
(i.) Soya ina virutubisho vingi na vilivyokamilika vya aina ya protini ambayo ni muhimu katika kuboresha lishe na afya kwa binadamu na mifugo;
(ii.) Soya ni chanzo rahisi na chenye gharama nafuu cha protini ambacho hata mtu wa kipato cha chini anaweza kumudu kwa kuwa zao hilo linaweza kulimwa maeneo mengi hapa nchini;
(iii). Kwa kuwa soya ina kiasi kikubwa cha protini ikilinganishwa na nyama na mayai na maziwa, inasaidia kupunguza kasi ya mashambulizi ya vijidudu vya maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa ya kansa, moyo, na kuwaongezea nguvu wagonjwa hasa wa UKIMWI;
(iv.) Soya ni zao muhimu kwa watu wa kipato cha chini katika kuondoa utapiamlo hususani kwa watoto kwa kuwa hawawezi kumudu gharama za vyanzo vingine vya protini kama nyama na mayai;
(v.) Kutokana na uwingi wa protini, matumizi ya soya kwa watoto yanasaidia viungo kukua kwa haraka;
(vi.) Soya hurutubisha udongo kwa kutumia njia ya nitrogen fixation. Kwa hiyo ni zao linalofaa kutumika katika kilimo cha mzunguko (crop rotation) na katika kurutubisha ardhi ;
(vii.) Soya huongeza kipato na ni zao linaloweza kuchangia katika kuondoa umaskini kwa mkulima kutokana na gharama ndogo za uzalishaji. Aidha, ni zao linaloweza kuondoa umaskini kwa watengenezaji wa vyakula vya binadamu na mifugo, wafanyabiashara na wafugaji na kutoa ajira kwa rika zote yaani vijana na wazee, vijijini na mijini; na
(viii.) Utafi ti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa mafuta ya soya yanaweza kutumika kwa kuendeshea mitambo yaani bio-fuel na bio-diesel.
Aina za Soya
Kuna aina mbalimbali za soya, aina zilizozoeleka Tanzania na pamoja na:
Bossier, Uyole soya 1, Ezumu Tumu, Delma Hermon, Duiker na Kaleya.
Kila aina inahitaji mazingira na hali ya hewa inakowezakustawi, kukomaa kwa muda maalum na kutoa mavuno mazuri. Hata hivyo Bossier ni aina ambayo hustawi katika maeneo mengi nchini. Kwa wastani, aina mbalimbali za soya huchukua wastani wa miezi mitatu hadi saba kukomaa kutegemea na aina, mahali ilikopandwa na utunzaji katika shamba.
2. MAZINGIRA, MVUA NA RUTUBA YA UDONGO
Mazingira na mikoa inayofaa kilimo cha soya
Mmea wa soya uliozaa |
Jambo muhimu linalotakiwa ni kufahamu na kupanda aina za soya zinazofaa katika eneo husika kulingana na maelekezo ya wataalamu. Kwa sasa mikoa inayoongoza kwa kilimo cha soya ni Ruvuma, Mbeya, Rukwa, Iringa na Morogoro. Mikoa mingine yenye uwezo na sifa za kuzalisha soya ni Tanga, Mtwara, Lindi, Kagera, Mara, Kigoma, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na Wizara ya Kilimo na Chakula mwaka wa 2005, zaidi ya tani milioni mbili za soya zinaweza kuzalishwa kwa mwaka endapo maeneo yote ya nchi yanayofaa kwa kilimo cha soya yakitumika ipasavyo. Uzalishaji wa sasa unakadiriwa kuwa tani elfu tano (5,000). Kiwango hiki cha uzalishaji ni cha chini sana ukilinganisha na kiwango kinachoweza kufi kiwa. Aidha, kiasi hiki kidogo na uwezo unaoweza kufi kiwa ni changamoto katika kuongeza uzalishaji na matumizi ya zao hilo.
Mahitaji ya Mvua
Soya huhitaji wastani wa mililita 350 hadi 1,500 za mvua kwa mwaka na inayonyesha kwa mtawanyiko mzuri hususan katika kipindi chote cha ukuaji wa zao hilo. Soya pia inafaa katika kilimo cha umwagiliaji kwani katika maeneo hayo kunakuwa na uhakika wa unyevu muda wote. Jambo la kuzingatia ni kutowepo kwa mvua wakati soya inapokauka.
Rutuba ya Udongo na Mahitaji ya Mbolea
Mmea wa soya kabla haujazaa |
3. UTAYARISHAJI NA UTUNZAJI WA SHAMBA LA SOYA
Kutayarisha shamba
Shamba la soya linahitaji maandalizi mazuri kama ilivyo kwa mazao mengine. Utayarishaji huo wa shamba ni pamoja na kuondoa magugu yote kwa kuwa soya haivumilii magugu hasa ikiwa katika hatua za mwanzo za ukuaji (seedling stage).
Shamba la soya linaweza kulimwa kwa sesa au matuta. Kilimo cha sesa chaweza kulimwa kwa kutumia jembe la mkono au la kukokotwa na wanyama kazi kama maksai na punda au kwa kutumia trekta. Kilimo cha matuta kukinga mteremko kinafaa na kinapendekezwa kwa maeneo yenye mwinuko. Vilevile kilimo cha matuta kinafaa sehemu tambarale lakini zenye mvua nyingi ili kupunguza madhara ya maji yanayotuama baada ya mvua kubwa kunyesha.
Mbegu
Ni muhimu kuandaa mbegu bora na safi mapema kabla ya msimu wa mvua kuanza. Kwa wastani kilo 20 hadi 30 za mbegu za soya zinatosha kwa hekta moja kutegemeana na aina ya mbegu. Kwa kuwa aina nyingi za soya hazistawi kila mahali, ni muhimu kwa mkulima kuhakikisha kuwa anatumia mbegu inayofaa katika eneo analotaka kulima soya hususani mahitaji ya mvua. Kwa sababu hiyo ni muhimu kwa mkulima kupata ushauri toka kwa mtaalam aliyekaribu naye kabla ya kuamua kulima soya. Aidha, mkulima anashauriwa kununua na kutumia mbegu kutoka katika sehemu ambazo chanzo cha mbegu hizo kinaeleweka. Mfano wa sehemu hizo ni pamoja na maduka ya pembejeo, wakala wa mbegu, mashamba ya mbegu na vituo vya utafi ti. Hii ni kwa sababu mbegu ya soya hupoteza nguvu ya uotaji katika msimu mmoja hasa katika sehemu za joto. Kwa hiyo mkulima anatakiwa kuhakikisha kuwa anapanda mbegu itakayoota. Kama mkulima hana uhakika na chanzo cha mbegu au ana wasiwasi wa kuota kwa mbegu alizonazo anaweza kufanya majaribo ya uotaji (germination test) kabla ya kupanda. Njia rahisi ni kuzilowesha mbegu kwa maji na kisha kuziweka kwenye kitambaa mahali penye joto la kutosha. Mbegu ziloweshwe na maji kila siku mpaka zitakapoota. Hesabu mbegu zilizoota na iwapo mbegu zilizoota ni chini ya 75 kati ya mbegu 100 yaani asilimia 75, mkulima anashauriwa kutopanda mbegu hizo.
Wakati wa kupanda
Upandaji wa soya unategemea na aina na mahali husika. Kwa aina za soya zinazokomaa mapema, soya ikipandwa mwanzoni mwa msimu wa mvua katika maeneo yanayopata mvua kwa kipindi kirefu itakomaa wakati mvua bado zinaendelea kunyesha na hivyo kufanya uvunaji na ukaushaji kuwa mgumu na kuhitaji nguvu kazi na muda wa ziada la sivyo mbegu zitaoza au kuanza kuota na kupoteza ubora wake. Kwa hiyo ni budi kujua mwenendo wa mvua mahali husika ili kupanda kwa wakati na aina ya soya kulingana na mahali hapo. Jambo la muhimu ni kuhakikisha kuwa soya inakomaa wakati hakuna mvua ili kurahisisha uvunaji na soya kutooza. Jedwali Namba 1 linaonyesha mahali, aina na muda wa kupanda soya.
Jedwali Namba 1: Muda unaoshauriwa kupanda soya
Na.
|
Mahali
|
Mbegu
|
Muda
| |
1
|
Sumbawanga, Nkasi, Songea,
| |||
Mbeya, Njombe, Dabaga na sehemu
|
Uyole soya 1
|
Novemba/Desemba
| ||
zenye mvua nyingi/ndefu
| ||||
2
|
Sumbawanga, Songea, Mbeya,
| |||
Njombe na sehemu zenye mvua
|
Bossier
|
Januari
| ||
nyingi/ndefu
| ||||
3
|
Ileje, Mbarali, Chunya, Mtwara na
| |||
sehemu zenye mvua kidogo na fupi
|
Bossier
|
Novemba/Desemba
| ||
4
|
Morogoro na Tanga
|
Bossier
|
Februari na Machi
|
Nafasi ya kupanda
Mmea wa soya baada ya kuota |
Panda mbegu moja kila shimo na zifukiwe kwa kina cha sentimeta mbili hadi sentimita tano ili zisiharibiwe au kuliwa na wanyama kama panya. Mkulima ahakikishe kuwa soya inapandwa kwenye udongo wenye unyevu wa kutosha; haitakiwi kabisa kupanda soya kwenye udongo mkavu au kuloweka soya kabla ya kupanda.
Palizi
Soya ni zao ambalo huzongwa na magugu hususani ikiwa katika hatua za mwanzo za ukuaji. Kwa hiyo mkulima anashauriwa kuwahi palizi katika kipindi cha wiki mbili baada ya soya kuota. Palizi ya mara ya pili inategemeana na kiwango cha magugu shambani. Endapo magugu yatakuwa yamefunikwa na majani ya soya palizi ya pili inaweza isihitajike kwa kuwa soya iliyopandwa kwa nafasi zinazotakiwa hukua na kufunika magugu yote na hivyo palizi ya pili kutohitajika.
Soya ikipandwa kwa nafasi pana na isiyotakiwa haikui kufi kia kiwango cha kufunika magugu na hivyo kulazimisha palizi ya pili kufanyika. Magugu katika shamba la soya yanaweza kudhibitiwa pia kwa katumia dawa ya kuzuia magugu kama GALEX; hata hivyo inafaa kufuata maelekezo ya kutumia ya dawa husika.
No comments:
Post a Comment