UFUGAJI BORA NI SULUHISHO LA AJIRA - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Wednesday, June 7, 2017

UFUGAJI BORA NI SULUHISHO LA AJIRA




UFUGAJI BORA NI SULUHISHO KWA TATIZO LA AJIRA

Kwa miaka mingi nchini Tanzania, na katika baadhi ya nchi nyingine za mashariki mwa Afrika, shughuli za kilimo na ufugaji zimekuwa zikichuku- liwa kuwa ni shughuli za wazee na watu wasio kuwa na uwezo hasa waishio viji- jini, huku vijana wakikimbilia kazi za kuajiriwa maofisini na kwenye biashara mijini. Kutokana na hali hii uzalishaji wa chakula na mazao ya biashara ulishuka kwa kiasi kikubwa sana, na kusababisha bei ya vyakula na mazao ya mifugo kuwa ya bei kubwa kutokana na uhaba. Hali hii pia ilisababisha kuyumba kwa uchumi katika maeneo husika. Watu wenye kipato pia wakitumia fedha nyingi kununulia chakula na mazao ya mifugo na maskini wakiendelea kuwa na maisha duni, na afya hafifu kwa kutoweza kumudu kupata lishe kamili kama inavyotakiwa. Kwa kuwa sekta hii ni muhimu na inategemewa na kila mtu ingawa haiku- pewa kipaumbele, hali ya uchumi mijini pia ilibadilika na kusababisha vijana walio wengi ambao walikuwa waki- kimbilia humo kujipatia ajira kukosa fursa hiyo. Na hapa ndipo ule usemi usemao shida ni mwalimu mzuri ulipo- chukua nafasi yake. Hivi sasa, wimbi la vijana wanaofanya shughuli za kilimo na ufugaji, limekuwa likiongezeka siku hadi siku. Hii inatokana na ukweli kwamba kilimo na ufugaji ndiyo sekta pekee ambayo ina ajira ya uhakika, na uweze- kano wa kujipatia fedha kwa mwaka mzima ni mkubwa mno.
 Tumeshuhudia na kusikia kwa siku za karibuni, vijana wanavyohangaika kupata fursa za kujipenyeza kwenye kilimo, na kuweza kufanya shughuli hii kibiashara. Tunawapongeza wale wote ambao wameweza kugundua kuwa kilimo na ufugaji ni kazi ya heshima na yenye tija kubwa kwa maisha yao. Pia tunawatia shime wale wote ambao bado hawa- jaanza wafanye hivyo, kumbuka, jembe halimtupi mkulima.

Katika ufugaji kuku kuna vitu vya kuzingati kabla hujaanza kufuga.

_Mbegu bora ya kuku
_Soko la kuku utakao wafuga
_Uzoefu kabla ya kuanzisha mradi
_Kujitoa kwa moyo wako wote katika ufugaji kuku. Ili uchukulie kama ni moja ya ajira yako katika maisha yako.
 Kabla ya kuanza kufuga kuku embu kwanza jiulize ! Kwanini umeamua kufuga kuku?

Ukisha pata jibu basi anza kujiekea malengo kiufugaji ili ufanikishe nia na lengo lako.
Kuna useme watu wanasema ufugaji kibiashara ni mpaka uanze na kuku 500! Lakini mimi nakwambia hii Leo ufugaji kibiashara unaweza ukaanza tu na kuku 10 na baada ya miezi 6 ukawa na kuku wengi.
 Hapa nimekumbuka ule usemi wa " Mtafutaji sio sawa na mkaa bure"

Katika ufugaji kuku changamoto ni

1. Magonjwa
2. Matunzo ( uzoefu)
3.Chakula
4.Soko
Kuhusu yote hayo yasikutishe Karibu Fugakibiashara (Uwkt).

Kwa wale wote wanaopenda kupata ushauri juu ya ufugaji kuku , kusimamiwa mradi wako kwa miezi 5 kwa gharama nafuu kabisa na baada ya hiyo miezi mitano utakuwa mzoefu katika ufugaji kuku kibiashara.



USISAHAU KUDOWNLOAD APPLICATION YA KILIMO BORA IPO PLAY STORE

DOWNLOAD HAPA SASA

                     
TEMBELEA BLOG HII KILA SIKU

No comments:

Post a Comment