Je wajua Vyura, Ndege, na Wadudu Huboresha Shamba - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Thursday, September 28, 2017

Je wajua Vyura, Ndege, na Wadudu Huboresha Shamba


Lakini unaweza kuwamalizaje wadudu waharibifu shambani mwako bila kutumia dawa? Usisahau kwamba zaidi ya kuwaua wadudu waharibifu, dawa hizo huua viumbe muhimu kama vile minyoo na kuvu. Pia, kumbuka kwamba vyura ni muhimu sana katika kilimo. Chura anaweza kula wadudu waharibifu 10,000 kwa muda wa miezi mitatu naye hachagui anachokula. Yeye hula viumbe wanaoharibu mimea kama vile nyenje, wadudu na viwavi wa aina fulani, na konokono.
Ndege pia hula viumbe waharibifu. Kitabu Gardening Without Poisons chasema kwamba ndege aina ya wren alionekana akiwalisha “makinda wake buibui na viwavi 500 alasiri moja katika majira ya kiangazi.” Ukitaka ndege kadhaa aina ya wren au ndege wengine wanaokula wadudu waje shambani mwako basi weka chakula cha ndege na vifaa vya kujenga kiota mahala wanapoweza kuviona. Muda si muda, utaona wakija! Na vipi wadudu? Wadudu wengi wanaoboresha shamba hula wadudu waharibifu. Ukinunua wadudu aina ya ladybug kisha uwaweke shambani mwako, watawamaliza mara moja wadudu aina ya aphid kwani wanapenda kula wadudu hao sana. Mayai ya kivunja-jungu yanaweza pia kununuliwa na kuwekwa shambani. Mayai hayo yakianguliwa, vivunja-jungu watakula wadudu wote walio karibu nao.

No comments:

Post a Comment