Zifuatazo ni dalili za nguruwe mgonjwa;-
· haonyeshi dalili za kupenda chakula
· anaweza kuhema kwa kasi dalili ya homa
· macho makavu
· ngozi kavu
· anakua anajitenga
· masikio kulala
· kwenye ngozi nyeupe ngozi inaweza kua nyekundu
· mkia kua mwembamba
· kuhalisha mda mwingine kuhalisha damu
MAGONJWA YANAYO SABABISHWA NA WADUDU
Wadudu wa ndani
Minyoo ndo wadudud wakuu wanaathiri tumoni kwa nguruwe, kuna minyoo zaidi ya 30,ila minyoo ambao wanaathiri kwa wakati mwingi ni minyoo duara(round worm) na minyoo tape(tape worm).
Round worm
Hii ukaa kwenye utumbo mpana wa nguruwe na uchukua chakula kutoka kwa nguruwe hivo nguruwe anaweza kukonda.minyooo mikubwa(Ascaris lumbricoides) hii ndo inapatikana sana.minyoo hii nimikubwa urefu wa penseli.maambukizi yanaanza pale myama anapo kula chakula chenye mayai ya monyoo hao.
DALILI
· Kunyonyoka manyoya(anorexia).
· Upungufu wa damu(anaemia).
· Baadae uzito upungua.
· Minyoo wakitibiwa wakati washakua wengi wanaweza kukata utumbo na kusababisha kifo.
KUKINGA/PREVENTION
· Kuzuia kwa kuweka dawa kwenye chakula na kutumia vyombo visafi
· Kuchunga kwa kutumia njia ya mzunguko na kutibu nyasi
· Kuwatenga watoto na wakubwa
· Kuwapatia dawa ya minyoo mara kwa mara
· Muoshe jike kabla ya kuzaa
· Unaweza kutumia miti shamba aina ya moringa
Tape worm
Hawa wanakua frat kama rebon na wanapatikana mahali tofauti tofauti dunian.hawana utumbo hivyo wanakula kupitia ngozi yao na wanachukua virutubisho.hua wanachukua folic acid na vitamin B-12 mwilini,wanaweza kusababisha sumu kwakua baada ya kula wanaacha uchafu na unakua kama mpira ambao unakaa karibu na ini.
DALILI
· Kudumaa
· Upungufu wa damu
· Ngozi kubadilika nakua mbaya
KINGA/PREVENTION
· Kuwapa dawa ya minyoo
· Hakikisha wanao hudumia nguruwe wawe wanatumia choo na kusafisha
WADUDU WA NJE
Wadudu wa nje inahusisha mange.lies na myiasis
Mange
Husababishwa na wadudu wanao itwa mites wanaishi kwenye ngozi ya nguruwe maeneo ya machoni, masikioni,miguuni na shingoni
DALILI
· Nguruwe anakua anjikuna kuna kwenye ukuta kwenye miguu,masikio,macho na masikio
· Ngozi inakua na mabaka kama vibarango na mistali mistali mwenkundu kama vidonda
· Manyoya hua yamevurugika
· Ngome anakua hatulii
· Vifo
· Na kupungukiwa damu kwa watoto
KINGA/PREVENTION
· Osha nguruwe mara mbili kwa wiki
· Madume wanatakiwa kuoshwa pia
· Wape dawa kila nguruwe anapoingia shambani kwako
· Usafi wa banda
TIBA/TREATMENT
· Unaweza kuwaosha pia kwa maji safi na sabuni
· Unaweza kuwaosha kwa organophosphate
· Unaweza kuwachoma Ivermectin kwakua inasaidia sana
CHAWA
Hawa wanakua wananyonya damu na dalili zake ni upungufu wa damu na pia mnyama anakua na madoa mekundu mwilini. Na pia unaweza kutibu Kwa kutumia viuadudu (insecticide) benzene hexachloride ndo hua inatumika kuua chawa.
MYIASIS
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na nzi wanao taga mayai kwenye vidonda,mayai hayo hukua hadi kufikia hatua ya kua nzi mkubwa na husababisha kidonda kua kikubwa zaidi.
Kidonda hua kichafu na kua kama na ukungu mweusi ambayo hayo ni mayai ya nzi,hivyo kuzuia hii unatakiwa kusafisha banda na kupunguza idadi ya nguruwe katika banda wasisongamane
KUWAPA DAWA ZA MINYOO(DEWORMING)
Dawa za minyoo ambazo zimehakikishwa nan i salama pale zinapo pewa kutokana na maelekezo sahihi ni kama
vermectin (Ivomec®), fenbendazole (Safe-Guard®), levamisole (Tramisol®, Levasole®), pyrantel (Banminth®), dichlorvos (Atgard®) na piperazine.
Unaweza kupanga ratiba ya kuwapa dawa zaminyoo na ukapanga na mtalaamu ili kua anawapa chanjo ifikapo siku sahihi
· Dume/Boars – kila miezi 6 months
· Jike/Sows – wiki 2 kabla ya kuzaa na baada ya kuwatenga watoto
· Watoto/Piglets – wiki 1 baada ya kuwatenga
· Wanao nenepeshwa/Fatteners – wiki moja baada ya kuwatenga na miezi mitatu badae
· Gilts – wiki 1 aada ya kuwatenga na unaweza kurudia miezi mitatu badae
DAWA ZA WADUDU WANAO JITOKEZA MARA KWA MARA
MINYOO NA HATUA
|
DAWA
|
Ascarids(adult)
|
Zote
|
Ascarids(hatua ya larva wanao hama)
|
Fenibendazole
|
Ascarids(hatua ya larva waalibifu)
|
Fenibendazole.pyrantel
|
whipworms
|
Feniendazole, , dichlorvos
|
Noduluar worm
|
Zote
|
Minyoo ya figo(wakubwa)
|
Fenbendazole, ivermectin, levamisole
|
Minyoo wa figo(larva katika ini)
|
Fenbendazole, levamisole
|
strongloydes
|
Fenbendazole
|
|
Levamisole, ivermectin
|
Matatizo ya uzazi na magonjwa
ANAPHRODISIAS
Pale nguruwe anaposhindwa kuingia kwenye joto.hapa nguruwe anakua haingii kwenye joto hii inaweza kusababishwa Na uzito mdogo kutokana na kuwalisha chakula kisicho tosha au kisicho na virutubisho, uzito ulio zidi, upungufu wa madini, minyoo kwenye utumbo, magonjwa sugu.
LEPTOSPIROSIS
Dalili ya ugonjwa huu ni homa, kuhara,kukojoa damu na kupolomosha mimba kwa hatua ya mwisho na unaweza kuwatibu kwa streptomycin kabla ya tendo. Na unaweza kutumia dawa za antibiotic.
.
BRUCELLOSIS
Ugonjwa huu unatokea kwa dume na jike na inakua na dalili kama vile kunyonyoka manyoya,homa,kupooza miguu,kilema,na kutoa mimba mapema, na kwamjike ambao tayari wanazaa huzaa watoto zaifu,uke hua na mwekundu na pia kondo hutoka nje na kwa dume hua na uvimbe kwenye mapumu ya nguruwe.
Na ugonjwa huu hauna tiba hivyo chinja nguruwe wenye ugonjwa huu.
UTERINE PROLAPSED
Ugonjwa huu usababisha uterus kutoka nje,napia ugonjwa huu hauna tiba hivyo mnyama hutakiwa kuchinjwa.
.
MASTITIS
Bacterial husababisha kuvimba kwa kiwele na kupelekea kubadili uzalishaji wa maziwa,
Dalili za ugonjwa huu ni kiwele kuvimba kua chamoto na maumivu napia uzalishaji wa maziwa upungua.
Unaweza kutibu kwa kukanda chuchu ambazo na usiruhusu watoto kunyonya,toa maziwa yote kwenye kiwele baada ya hayo tumia antibiotics.penicillin-streptomycin.
.
ATROPHIC RHINITIS (KUVIMBA KWA PUA)
Dalili ya ugonjwa huu kwa watoto wanakua wana koroma,kukohoa na kupumilia mdomo na unaweza kutibu kwa kutumia antibiotics na usafi pia ni muhimu
GREASY PIG DISEASE
Huu ni ugonjwa unao sababisha mabaka,vibarango kwenye ngozi,pia mnyama upungua kilo na anaweza kufa.zuia kwa kuzuia ugomvi wa nguruwe kwa kuwakata meno,kuwapa chakula cha kutosha,usafi na tumia antibiotics
FOOT AND MOUTH DISEASE (FMD)
huu ni ugonjwa wa mdomo na miguu na inadhulu wanyama wenye kwato
Dalili zake nguruwe anaweza kua kilema,homa na vidonda mdomoni na miguuni
unaweza kutibu kwa kutumia antibiotics.
Vaccination Disinfection No therapy (treatment)
ANTHRAX/kimeta
Kimeta kinasababishwa na kuwalisha nyama nguruwe na dalili zake ni kupumua kwa shida,kuvimba shingon,homa na kutoa kinyesi chenye damu
na mnyama alie kufa na kimeta hutoa damu maeneo ya wazi mwilini.
Na unaweza kutibu Kwa kutumia antibitics.
No comments:
Post a Comment