Mbinu za Kuzuia Wadudu, Ndege na Wanyama Waharibifu wa Mazao - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Tuesday, September 26, 2017

Mbinu za Kuzuia Wadudu, Ndege na Wanyama Waharibifu wa Mazao

Wadudu
Wadudu wanaoweza kushambulia mazao ni pamoja na katapila na jongoo.
Katapila
  • Hukata ncha ya mmea inayokua
Kudhibiti
  • Kagua shamba mara kwa mara ili kutambua kuwepo kwa wadudu hao na kuwaua.

 Jongoo
  • Hukwangua shina na kuacha michubuko
Kudhibiti
  •  Kagua shamba mara kwa mara na kuwaua.
Kuku
  • Huharibu mmea kwa kuparura juu ya ardhi na kusababisha kujeruhi na kukata mizizi. Uharibifu huu husababisha mmea kuwa katika mazingira rahisi ya kushambuliwa na vimelea kama Fusarium batatis ambao huozesha mizizi ya mmea.
Kudhibiti
  • Zuia kuku wasiingie shambani.
Konokono
  • Husababisha uharibifu zaidi kipindi cha mvua. Wanapotambaa kwenye mmea huacha utando, hasa katika sehemu inayochipua na kusababisha mmea kudumaa.
Kudhibiti
  • Kagua shamba mara kwa mara na kuwaondoa.
  • Weka mchanganyiko wa mbolea ya samadi na majivu kuzunguka shina la mmea ili kuzuia wasiweze kupanda juu ya mimea.
ANGALIZO: Ni muhimu kupulizia / kunyunyizia dawa uharibifu ukiwa mkubwa sana. Tembelea maduka ya Kilimo kwa aJili ya Ushauri Zaidi na kununua Dawa.

No comments:

Post a Comment