UMUHIMU MKUBWA WA KOMAMANGA (POMEGRANATE) JUU YA MARADHI YA KANSA - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Tuesday, September 26, 2017

UMUHIMU MKUBWA WA KOMAMANGA (POMEGRANATE) JUU YA MARADHI YA KANSA


Uchunguzi mpya umeonyesha kwamba, katika tunda la komamanga kuna kemikali zinazozuia kansa ya matiti isitambae mwilini.

Uchunguzi huo uliochapishwa katika jarada la Utafiti la kuzuia Kansa umeonyesha kwamba, kemikali ziitwazo ellegitannins zinazopatikana kwa wingi kwenye komamanga, zinaweza kuzuia kimeng’enyo (enzyme) aina ya aromatase, suala ambalo huzuia kukua kwa Homoni ya estrogen inayopatikana katika kansa ya matiti.

Shiuan Chen Kiongozi wa uchunguzi huo amesema kwamba, kemikali hizo hupunguza uzalishwaji wa estrogen, na kusaidia kuzuia seli za kansa ya matiti zisizaliane mwilini, pamoja na tezi la ugonjwa huo lisikue.

Aromatase, ni kimeng’enyo ambacho hugeuza Homoni ya androgen kuwa estrogen, na kushambulia kimeng’enyo hicho ndio lengo kuu la dawa za kupambana na kansa za matiti zinazosababishwa na homoni ya etrogen.

Huko nyuma pia uchunguzi ulionyesha kwamba tunda la komamanga lina faida kubwa kiafya hasa kwa kuwa na  anti Oxidant nyingi na vitamin mbalimbali, ambalo huzifanya tunda hilo liweze kusaidia katika kupambana na magonjwa ya saratani, matatizo ya moyo na hata ugonjwa wa kusahau uzeeni au Alzheimer.

Anti Oxidant huzuiaradikali huru ambazo ni hatari sana kwa miili yetu. Uwezo huo hupelekea mwili kukabiliana na magonjwa mbalimbali hata ugonjwa wa homa ya mafua ya nguruwe. Kama huwezi kupata tunda la komamanga sokoni, basi unaweza kutumia juisi ya Komamanga na daima tutunze afya zetu!

FAIDA YA JUISI YA KOMAMANGA

  1. Huweza kuzuia maendeleo ya saratani ya mapafu.
  2. Hupambana na saratani ya matiti
  3. Hupunguza ukuaji wa saratani ya kibofu
  4. Inaweza kuzuia na kupunguza kasi ya ugonjwa wa Alzheimer
  5. Inapunguza kolesterol
  6. Hushusha shinikizo la damu
  7. Hulinda meno

Inasemekana ukinywa juisi ya komamanga (pomegranate) nusu lita kila siku kwa muda wa mwezi mmoja, inasaidia kupunguza mafuta tumboni kwa wale wenye vitambi. Jitahidi kuwa na matumizi ya haya matunda unufaike na uboreshe afya yako.

No comments:

Post a Comment