umwagiliaji wa matone (Drip irrigation system) - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Friday, September 29, 2017

umwagiliaji wa matone (Drip irrigation system)

UMUHIMU WA MAJI UNATUPEREKEA KUWEKEZA NGUVU ZETU KWENYE UCHIMBAJI WA KISIMA. Asilimia 80 ya uhitaji mkubwa wa mazao mengi ni maji na moja ya changamoto kwenye kilimo ni maji. Mfumo huu wa umwagiliaji umetengenezwa kupunguza tatizo hili kwa asilimia kubwa sana kama nitakavyoelezea baadae kidogo.
Utangulizi.
Mfumo wa umwagiliaji wa matone (Drip irrigation system) unafanya kazi kama zile drip za hospital za kuongezewa maji au damu ambazo huwa tunaziita drip... wanasemaga mtu katundikiwa drip ya maji.
Vitu vinavyotengeneza mfumo huu.
1. Pump... Hii inafanya kaza ya kuvuta maji kutoka kwenye chanzo cha maji na kupeleka shambani direct au kwenye tank au water resevour kwa kuhifadhi
2. Filters/ chujio... Filter zinachuja maji ili takataka na particles nyingne siziingie kwenye mfumo wa umwagiliaji na kuleta shida kama za kuziba pipes na emmiters
Emmitters ni visehemu vya kutolea maji kwa ajili ya kumwagilia
3. Back wash controller/ back flow contorller ni vivalve vinavyozia maji kurudi nyuma ya mfumo hasa mgandamizo wa maji ( pressure) inapokuwa ndogo. Maji yanatakiwa yawe na uelekeo mmoja tu (Unidirection). Hizi ni kama valves za mishipa ya vein zinavyozuia damu isirud nyuma
4. Pressure regulator au control valve... inafanya kaz ya kucontrol pressure ya maji inayoingia kwenye pipes... ni muhimu sana kuregulate pressure maana ikizidi tu unaweza kukuta sio drip tena ila pipes au tape zimeburst zote ukazimia😊
5. Water tank/resouvr au chanzo cha maji... kazi ni kusupply maji kwenye drip... lazima maji yawepo ndio uwe mfumo wa umwagiliaji
6. Main line/ pipe ni bomba kubwa linalotoa maji kwenye tank au kwenye source nyingine kwenda shambani kwa ajili ya kusambazwa. 7.Small poly tubes/tapes hizo ndio zileee zinasambaza maji shambani sasa na ndio zenye vitobo vya kudodondoshea maji sasa
Kuna connectors pia ambazo zinaunganisha hizo tubes na pipes
Pia kuna gate valves... hizi zinasaidia kumwagilia shamba kwa awamu... yani unaweza kumwagilia nusu shamba kwanza ukaendelea na nusu baadae. Gate valves Ikifungwa zinazuia maji kwenda eneo moja na kuruhusu eneo jingine hasa kama maji yana pressure ndogo
Kuna source ya power kama umeme au solar kwa ajili ya pump lakin pia unaweza kutumia mafuta tu
Naombeni niendelee na faida za kutumia mfumo huu wa umwagiliaji.
Matumizi mazuri ya maji
Mara nyingi wakulima hawajui kama kumwaga maji hovyo ni tatizo as long as yapo😊. Sasa drip inapunguza kupotea maji unnecessarily kwa sababu inadondosha maji kwenye mmea tu
Kwa wenzangu wa kanda ya kati ambao kuna shida ya maji wataelewa kirahisi au kama unatumia ya DAWASCO yanye mita mtaelewa zaidi😂😂😂
2. Kwa sababu mfumo huu unamwagia maji kwenye shina la mche tu... unasaidia sana kupunguza shida ya magugu shambani... wakat mmea unapata maji tena ya kutosha magugu yanalala njaa😊😊😊 inapunguza usumbufu na gharama za palizi
Ukimwagia kienyeji kwa sababu unamwaga maji mengi kwa wakat mmoja... yanapotea haraka sana na mengine ndio yanaenda kustawisha magugu
3. Matumizi mazuri ya mbolea... hapa patamu😋😋😋
Kwa mbolea za dukani zinazoyeyuka kwenye maji... water soluble...unaziweka kwenye tank zinayeyuka (kutengeneza solution) na then zinaenda kwenye mimea kwa kupitia matone yanatoka kwenye tubes... once again magugu yanalala njaa ðŸ˜‚😂😂. Tofauti na kumwaga shimon then unamwaga lita 5 za maji mbolea inayeyuka na kupoletlea pembeni magugu nayo yanasherehekea😊
4. Haki sawa kwa kila mmea.
Mfumo wa umwagiliaji wa matone unatoa kiwango sawa sawa cha maji na mbolea kwa mimea yoooote shambani. Yami mmea ambao upo karibu na chanzo cha maji unapata kiasi cha maji sawa sawa na mmea ambao upo hukooo mwisho wa shambani... kwa sababu hii basi mazao yanatoka mengi uniform kama matikiti mengi yanakua makubwa na yanayokaribiana sana size.
Tofauti na umwagiliaji wa kawaida ambapo mmea karibu na kisima ndio umapendelewaaa halafu ile ya kwenye margin inakonda kwa sababu watu wanachoka sana pia kubeba ndoo nenda rudi
5. Inapunguza gharama ya nguvukazi na kupunguza chamhamoto ya nguvu kazi
Watu wengi wanaishi mjini wana mashamba bush na vijana wanawadanganya sana kuwa wamemwagilia kumbe sio au wamemwagilia kwa kumbe wamerashia tu... hii system kwa sababu ni ya kufungua tu na kufunga bomba hata mtoto wa darasa la kwanza anaweza kuelekezwa kufungua na kufunga bomba kama ina kijana wa kazi safi angalau kwa sababu hatumii nguvu kubwa sio rahisi kukudanganya
5. Mfumo wa drip unapunguza trembling/ kukanyaga kanyaga shamba ambapo kunasababisha compaction ya shamba na kupunguza circulation ya hewa ardhini
6. KUONGEZA UZAAJI.
Nimeandika kwa herufi kubwa kabisaaaaaa....
Drio irrigation bwana inaongeza uzaaji almost 3-4 times normal irrigation... natumia kwenye matikiti maji... kwa kawaida nilipata tani 4 kwa heka na tani 12 kwa drip. Hii inasababishwa na usawa kwenye maji na mbolea
7. Drip zinapunguza mmomonyoko wa ardhi... tofauti na kumwagilia kienyeji au kwa mitaro
Yan kama unatumia drip na ukaweka matandazo ya plastic (Plastic mulch) umemaliza... no palizi... no energy... high yield... grt production
Pia mfumo wa drip ni portable ambao unaweza kuutumia hata kwenye shamba la kukodi na kuutoa unaweka kwenye kirikuu mpaka home... kuwe na chanzo kizur cha maji tu
Diadvantages
- Mfumo huu ni ghali kidogo hawa kwa wanaoanza kwa sababu roll moje ya mita 2000 inauzwa 1.8M mpka 3.6 ambayo inatosha heka moja tu ya matikiti maji... japo otakisaidia sana kuweka mbegu nyingi shambani na kuvuna sana sana sana
Disadvantage nyingne ni kwamba installation yake inahitaji utaalami kidogo kitu ambacho kinaongeza gharama kwa sababu sio kila mtu anaweza kufunga drip

No comments:

Post a Comment