HOMA KALI YA MATUMBO (Fowl Typhoid)
Ni ugonjwa unao sababishwa na bacteria (sallmonella gallinarum). Chanzo cha maambuziki ni maji maji na chakula kilicho chafuliwa na kinyesi cha kuku mgonjwa. Maambukizi yanaweza kupitia katika mayai yaliototolewa na Vifaranga kuathirika.Pia machine za kutotolea zilizo chafuliwa zinaweza kuambukiza ugonjwa huu.
Dalili za ugonjwa huu:
Vifaranga
_Vifaranga wanatotolewa wakiwa wamekufa, au kufa Mara baada ya kutotolewa.
_Hujikunyata pamoja Karibu na chanzo za joto
_ Kuharisha kinyesi cha maji maji na chanjano
_Uharo huganda kwenye manyoa na sehemu ya kutolea haja.
_Vifo vya ghafla kwa Vifaranga ambao hawajaonesha dalili .
Kwa kuku wakubwa:
_ Vifo vya ghafla, kuharisha kinyesi cha maji maji na cha njano
_Kupungua uzito
_Kuku kuzubaa na kutokuwa na hamu ya kula pia hunywa maji sana _Mapanga na mashavu kuonesha kutokuwa na damu
_Upumuaji huweza kuwa ni wa haraka haraka na joto kupanda.
Ukiupasua mzoga :
_Ini na Wengu kuvimba
_ Misuli iliyovia na damu kuwa nyeusi
_Ini lililovimba na kuwa na rangi ya pinki
_ Bandama lililovimba
_Mabaka meupe kwenye sehemu ya juu ya figo
Figo na bandama za Bata mzinga: Figo zimevimba, na bandama zina madoa doa. Figo na bandama zenye ugonjwa zinalinganishwa na nzima |
Aina nyingine ya Homa ya Matumbo (Avian Paratyphoid) inafanana na aina iliyoelezwa hapo juu, tofauti kubwa ni aina ya vimelea vinavyosababisha aina hii ya homa, na huathiri zaidi kuku na bata wadogo.
HOMA YA MATUMBO (Avian Paratyphoid}
Maelezo: Ni ugonjwa wa kuku unaosababishwa na bakteria wa spishi tofauti na ya bakteria wanaosababisha homa kali ya matumbo na hushambulia zaidi kuku na bata wadogo. Vimelea vya ugonjwa huu huweza kusababisha homa ya matumbo kwenye binadamu.
Jinsi Ugonjwa Unavyoenea• Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi cha kuku wagonjwa. Panya, mbwa, ndege na wanyama wengine wanaweza kueneza ugonjwa kwa kubeba mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa na kuchafua vyanzo vya maji na vyakula. • Maambukizi pia yanaweza kupitia katika mayai yanayototolewa na vifaranga kuathirika. Pia mashine za kutotolea zilizochafuliwa zinaweza kuambukiza vifaranga.
Dalili:
Vifaranga• Vifaranga wanatotolewa wakiwa wamekufa au mara tu baada ya kuanguliwa
• Hujikusanya pamoja karibu na joto
• Uharo kuganda kwenye manyoya ya sehemu ya kutolea haja
• Vifo kwenye vifaranga vinaweza kufikia hadi asilimia 50.
Kuku wakubwa• Vifo vya ghafla Kuharisha kinyesi cha majimaji na cha rangi ya njano
• Kuku kuharisha
• Kupungua kwa uzito
• Kuku wa mayai hupunguza utagaji
• Kuku anaonekana mchovu
Uchunguzi wa Mzoga
Mabadiliko muhimu katika mzoga
_Mzoga kuonesha rangi ya njano
_Utumbo kuvimba
Utumbo wa kuku wenye uvimbe mweupe uliotapakaa |
_Uvimbe mdogo mdogo mweupe kwenye ini
_ Mapafu kuvimba, pia{yanaweza kuwa na rangi ya hudhurungi }.
Jinsi ya kuzuia: 1.Fanya usafi bandani na mazingira yote yanayo kuzunguuka 2. Hakikisha Vifaranga wanapata joto la kutosha 3.Mayai yakusanywe Mara kwa Mara 4. Weka utaratibu wa kuhakikisha watu, wanyama, ndege wa aina nyingine na ndege wa porini hawazururi shambani. 5. kuku wa banda lingine la jirani wasiingie ovyo ndani ya banda lako
Tiba Kwa Magonjwa Haya: Tumia madawa ya antibiotic au dawa za sulfa,
unaweza kutumia kwa ajili ya magonjwa haya.Esb3, Tremazine 30% TyphoprimTyphoprim, Trisul nk
Kwa ushauri zaidi onana na doct aliye karibu yako au njoo whatsapp 0655610894
HAKIKISHA HUPITWI NA KITU TEMBELEA BLOG YETU HII MPYA KILA SIKU KUJIFUNZA MBINU MBALI MBALI ZA KILIMO NA UFUGAJI
from FUGA KIBIASHARA http://ift.tt/2Aavu0M
No comments:
Post a Comment