Umuhimu Wa Bruda Kwa Vifaranga - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Tuesday, November 14, 2017

Umuhimu Wa Bruda Kwa Vifaranga



UMUHIMU WA BRUDA KWA VIFARANGA
Habari ndugu mfugaji Leo tujifunze umuhimu wa bruda/brooder kwa Vifaranga.
Brooder/ Bruda Hiki ni kifaa cha kulelea Vifaranga, unachoweza kutengeneza kwa kutumia mabox singbod au viroba.
Kifaa hiki Mara nyingi huwa ni cha duara Hii ni kwasababu ya kuzuia Vifaranga visikusanyike pembeni
Katika kulea Vifaranga kitu kikubwa ni matunzo bora, kuwapati chanjo, chakula bora hasa joto hasa wakiwa wadogo pale wanapo anza maisha mapya.
Kuna madhara mengi yanayo sababishwa na baridi kwa Vifaranga kama kudumaa, kufa nk
Wafugaji wengi hawapendi kulea Vifaranga kwasababu Mara nyingi wanapo jaribu hujikuta Vifaranga wengi sana wana kufa.
Tukiachana na mambo mengine yanayo husu kulea Vifaranga kwanza tuuone umuhimu wa bruda

UMUHIMU WA BRUDA KWA VIFARANGA
Mfugaji anaetumia bruda na yule asiye tumia bruda wana utofauti Mkubwa
Kwanza ukitumia bruda jinsi ya kufanya usafi ni rahisi kwasababu Vifaranga huwa kwenye eneo lile la bruda na kama wanapo chafua huo uchafu hauwezi sambaa banda zima
Ukitumia bruda utapata urahisi wa kuhakikisha Vifaranga wako wana pata joto la kutosha, kwasababu kama Vifaranga wapo kwenye bruda na umewafungia taa ile joto ya taa itaenda moja kwa moja kwenye Vifaranga halisambai ovyo
Kwa kuwa joto halisambai ovyo Basi kuna uwezekano wa kutumia vyanzo vichache vya joto tofauti na yule asiye tumia bruda
Kama utatumia umeme , mkaa au Mafuta katika kuwapatia joto Vifaranga, utakapo tumia bruda cost itapungua kwasababu joto litawahi kuwatosheleza Vifaranga. Tofauti na yule asietumia bruda na kuweka balbu nyingi ili Vifaranga wapate joto
Kwa kuwa Vifaranga wanapata joto vizuri basi utafanikiwa kupunguza vifo kwa Vifaranga wako

VITU MUHIMU NDANI YA BRUDA
1. Vyombo vya maji
2. Vyombo vya chakula
3. Chanzo cha joto unaweza tumia
• Balbu
•Jiko _ ila hakikisha unaliwashia nje ya banda la Vifaranga
• Chemli
•Vyungu.
FANYA HAYA NDANI YA BRUDA KABLA YA KULETA VIFARANGA.
Hakikisha brooder unayotarajia kuweka vifaranga vyako liwe
1. Kavu na safi kwa kuisafisha na dawa ya kuua wa dudu
2. Imewekwa maranda
3. kutandazwa magazeti kwenye sakafu
4. Umeweka jiko la mkaa lenye moto/balbu au chanzo chochote cha joto saa moja kabla ya kuwaingiza kwaajili ya kupasha chumba joto.
5. Wanapatiwa glucose kwenye maji kuwapa nguvu kabla ya kuanza kuwapa chakula.
_________

Whatsapp 0655610894




from UFUGAJI YAKINIFU http://ift.tt/2zZGFJK

No comments:

Post a Comment