Ufugaji Kuku Wa Asili - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Wednesday, December 6, 2017

Ufugaji Kuku Wa Asili


Kuku wa Asili ni wale ambao wamekuwepo hapa nchini kwa miaka mingi na damu yao
haijachanganyika na ya kuku wa kigeni.
 Kuku hawa wana rangi na maumbo mbali mbali.
Idadi ya kuku wa Asili hapa Tanzania inakadiriwa kufikia milioni 56. Kati ya kaya milioni 3.8
zinazojishughulisha na kilimo nchini, kaya milioni 2.3 hujishughulisha na ufugaji wa kuku wa asili.
Kwa kawaida ufugaji wa kuku wa Asili hapa nchini kwetu Tanzania hufanywa na wafugaji wadogo
wadogo wanaoishi kando kando ya miji na wale wanaoishi vijijini. Kuku hawa hufugwa huria (freerange),yaani hufungiwa ndani nyakati za usiku na hufunguliwa asubuhi ili wajitafutie chakula.

Kuku hawa hutoa mazao machache sana yaani nyama na mayai, kwa mfano kuku mmoja hutaga
kiasi cha mayai 40-60 kwa mwaka badala ya 100-150 iwapo atatunzwa vizuri. Pia uzito wa kuku
hai ni wa chini sana, wastani wa kilo 1.0–1.5 katika umri wa zaidi ya miezi 6 badala ya kilo 1.8–2.5
iwapo atatunzwa vizuri.

Sifa za Kuku wa Asili:

-Wastahimilivu wa magonjwa, lakini ni muhimu wakikingwa na baadhi ya magonjwa ya kuku
kama mdondo, ndui ya kuku nk. ili kuweza kuwaendeleza.
-Wana uwezo wa kujitafutia chakula ardhini, lakini ili kuwaendeleza ni lazima kuwapa chakula
bora cha ziada.
-Wana uwezo wa kuatamia mayai, kutotoa, kulea vifaranga na ustahimilivu wa mazingira
magumu (ukame, baridi nk).
-Nyama na mayai yake vina ladha nzuri kuliko kuku wa kisasa.
-Kwa kiasi fulani wana uwezo wa kujilinda na maadui kama vile mwewe.

Pamoja na sifa hizi ni muhimu kuku hao wakapewa matunzo mazuri, wawekwe kwenye mabandamazuri na imara, pia wapewe maji na chakula bora cha kutosha bila kusahau chanjo. 

Faida za Ufugaji wa Kuku wa Asili:

-Chakula – nyama ya kuku na mayai hutumika kama chakula muhimu cha wanadamu, chenye
protini
-Chanzo cha kipato – mkulima hupata fedha akiuza kuku au mayai.
-Chanzo cha ajira – ufugaji wa kuku hutoa ajira kwa jamii.
-Huzaliana haraka na hufugika kiurahisi tofauti na mifugo mingine
-Gharama nafuu za kuanzisha na kuendesha mradi huu.

Sifa za kuzingatia wakati wa kuchagua mitetea:
Jogoo na mitetea aina ya Sussex
Wawe na:
-Umbile kubwa.
-Uwezo wa kutaga wakiwa na umri mdogo (miezi 6).
-Uwezo wa kustahimili magonjwa.
-Uwezo wa kukua haraka.
-Uwezo wa kutaga mayai mengi {zaidi ya 15 kwa mtago mmoja (clutch)}.
-Uwezo wa kuatamia na kuangua vifaranga wengi na kuwalea.

Sifa za kuzingatia wakati wa kuchagua majogoo:

Jogoo bora, awe na:
-Umbo kubwa.
-Miguu imara na yenye nguvu.
-Kucha fupi.
-Mwenye nguvu.
-Machachari.
-Upanga/kilemba kikubwa.
-Tabia ya kupenda vifaranga.

Njia zitumikazo katika kuchagua kuku wa kuendeleza kizazi:

-Kwa kuangalia kuku wenyewe kulingana na sifa zilizotajwa hapo juu.
-Kwa kufuatilia kumbukumbu za wazazi wa kuku unaotaka kuwachagua.
-Kwa kuangalia kumbukumbu za familia (wazazi, kaka na dada).

Wakati muafaka wa kuchagua kuku wa kuendeleza kizazi:
-Mara tu wakitotolewa.
-Wakati wa ukuaji.
-Zoezi endelevu.
-Uzalishaji ukishuka chini ya asilimia 50.
-Wakati kuku wanapoangusha manyoya.

Faida ya kuondoa kuku wasiofaa kwenye kundi:
-Inasaidia kuongeza uzalishaji wa mayai.
-Inapunguza kulisha kuku ambao uzalishaji wake ni hafifu.
-Inapunguza uenezaji wa magonjwa ya kuku.
-Huongeza nafasi zaidi kwa kuku wazuri kwenye banda.
-Uwezekano wa kuuza kuku kama hao ni mkubwa kabla hawajafa.

AHSANTENI KWA LEO TUISHIE HAPA SOMO LITAENDELEA.................


TEMBELEA BLOG HII KILA SIKU UKIWA NA SWALI COMMENT HAPO CHINI UTAJIBIWA








from FUGA KIBIASHARA http://ift.tt/2iwih7R

No comments:

Post a Comment