Ufugaji Samaki (Mtaji wa awali) - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Saturday, December 30, 2017

Ufugaji Samaki (Mtaji wa awali)


Habari ya uzima ndugu mwana familia wa blog hii, ni matumaini yangu haujambo.

Tazama video hiyo apo juu kufahamu mchanganuo wa mtaji wa awali wa ufugaji samaki

MATATIZO KATIKA UFUGAJI SAMAKI

Ingawa ufugaji wa samaki si kazi ngumu sana, kuna matatizo mbali mbali ambayo mfugaji anaweza kukumbana nayo. Lakini, matatizo mengi yanaweza kuepukika kama mfugaji ataweza kufuata kikamilifu

1. Tatizo mojawapo ni la kuvuja kwa kuta za bwawa. Tatizo hili
hutokea iwapo ujengaji wa bwawa haukufuata maagizo na taratibu za ujengaji wa bwawa. Iwapo utakumbana na tatizo hili, muone afisa uvuvi aliye karibu nawe upate ushauri.

2. Tatizo la maadui wa samaki kama vile ndege, kenge, fisi maji, nyoka hutokea. Kwa kiasi kikubwa tatizo hili huambatana na ujengaji bwawa mbali na nyumbani na bwawa kuwa na nyasi nyingi (halifyekewi). Suluhisho ni kufweka nyasi
kila mara, kujenga uzio kwa kutumia matete na hata nyaya za seny’enge, kuwinda ndege na kuharibu mazalia/maskani yao, bwawa kuwa karibu na maskani ya watu.

3. Kudumaa kwa samaki kutokana na kuwa wengi bwawani kupita idadi inayotakiwa. Tatizo hili hutokana na kutokukaushwa bwawa kwa kipindi kirefu. Utatuzi huweza kuwa; kukausha bwawa kila baada ya miezi 6 hadi 9

4. Ugumu wa kukausha maji bwawani. Husababishwa na bwawa
kujenjwa kwenye eneo la tambarare kiasi kuwa hakuna uwezekano wa kutumia bomba au kukata kuta za bwawa kuondoa maji. Utatuzi; chimba bwawa kwenye eneo
lenye mteremko wa wastani

5. Bwawa lisilo kaushika huwa mazalia ya Mbu wakati linapokuwa halina samaki ndani yake na kusaidia kuenea kwa malaria. Konokono wenye mabuu ya kichocho huzaliana kwenye mabwawa yenye kina kifupi au yenye majani mengi.
Ni vema kuwa na bwawa yenye kina cha kutosha, lisilo na nyasi au majani ndani yake na linaloweza kukaushika kirahisi ili kuondokana na matatizo haya.

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHAGUA ENEO KWAAJILI YA UFUGAJI SAMAKI
1. Aina ya udogo: hili nijambo muhimu kwani aina ya udogo huathiri kwenye kuchagua aina gani ya bwawa litumike. Tambua kuwa kuna aina nyingi ya mabwawa kama bwawa la udogo tupu (earthen pond) na bwawa la zege (concrete pond). Bwawa la zege hutumia gharama nyingi kulijenga ukilinganisha na bwawa la udogo tu. Hivyo ili bwawa liwe la udogo ni lazima aina ya udogo wa eneo husika uwe na sifa ya kutunza maji.

2. Maji: samaki huishi kwenye maji hivyo nilazima uwahakikishie upatikanaji wa maji safi na salama kwa uhai wao. Maji yawe yanapatika kwa Wingi, Salama na yenye kuweza kuwekwa katika miundombinu sahihi kwaajili ya kutumika wakati wowote. Maji yanaweza kuwa ya kisima, mto, ziwa, chemchem,au bomba. Kila aina ya maji ina faida zake na changamoto zake. Kwa mfano wakati maji ya mto huwa yanaweza kupatikana kwa urahisi lakin yanachangamoto yakuweza kukuletea vijidudu vya magonjwa kama minyoo, typhoid na kipindupindu.

3. Vifaranga: usishangae! Ndiyo mbegu za samaki yaani samaki wadogo huitwa vifaranga. Nilazima ujihakikishie upatikanaji wa mbegu bora kwaajili ya matokeo mazuri. Mbegu duni huchukua muda mwingi kukuwa na hivyo kumuongezea mkulima gharama za ufugaji na kumpunguzia kipato.

4. Chakula: ufugaji wa samaki kwaajili ya biashara humuitaji mkulima kuwapatia samaki chakula za ziada (supplementary feed) ili samaki wakue kwa haraka zaidi. Kumbuka ukuwaji wa samaki hutegemea UBORA WA MAJI + UBORA WA CHAKULA.

5. Ulinzi na usalama: ni vyema mkulima kuepukana na migogoro yeyote kama ya umiliki wa ardhi na matumizi ya maji ili kuondoa uwezekano kukuhujimiwa katika mradi wake.

6. Usafiri: kwa nyakati tofauti mkulima atahitajika kusafirisha ima malighafi zitumikazo kwenye ufugaji au mazao ya ufugaji baada ya kuvuna. Hivyo ni muhimu kuzingatia uwezekano wa usafiri sahihi wakati wote. Usafiri siyo mtu awe na gari hapana ila uwepo wa miundombinu safi yaweza tosha.

7. Soko: Mwisho wa ufugaji ni kuuza mazao yako kwa faida hivyo ni vyema mkulima akafanya tafiti za kupata soko la uhakika kwa mazao yake. Mkulima huweza tumia soko la karibu kama majirani na wafanyabiashara wa karibu. Pia anaweza kutumia soko la mbali.

Ufugaji wa samaki unalipa endapo tu mkulima atapata mtaalamu sahihi na akazingatia kanuni za ufugaji.





from FUGA KIBIASHARA http://ift.tt/2lomT1v

No comments:

Post a Comment