COCCIDIOSIS
Ugonjwa huu husababishwa na protozoa.
Coccidiosis(kuhara damu)_ ugonjwa huu huonekana katika sura mbili.
(1) Caecal coccidiosis ___Sura hii ya ugonjwa hushika vifaranga.
Dalili zake_Vifaranga huonekana wamezubaa, kushusha mabawa
_Kinyesi kuonesha damu
_Vifo vingi hutokea
_Vifaranga kushindwa kula na kunywa.
_Damu huonekana kwa wingi katika kinyesi kabla ya kifo.
Katika sura hii Kifaranga chenye coccidiosis sio lazima kionesha dalili zote au kinyesi cha damu. Hapana unaweza kuona Vifaranga wako wamezubaa , huku wameshusha mabawa, kuharisha kijivu, ugoro, vifo vingi kila asubuhi unakuta vimekufa .
Usipo kuwa makini unaweza kujiuliza ni ugonjwa gani? Kwa kuwa umezoea mpaka uione damu kwenye kinyesi ndio ujue kuwa ni coccidiosis.
Pia ni moja ya ugonjwa rafiki sana na uchafu, hivyo ugonjwa huu unapoingia bandani jitahidi sana kuzingatia usafi, na kuwa tenga wale kuku wagonjwa sana ili kudhibiti ugonjwa kuenea bandani.
(2)Intestinal coccidiosis__ Sura hii ya ugonjwa hushika kuku wakubwa.
Dalili zake. _Kuku kupunguza ulaji wa chakula _Kuku kupungua uzito
_ Kuku kuangusha mabawa
_Kuku kuharisha kijivu , ugoro na mara nyingi kinyesi kuwa na damu damu
_ Kuku kukonda
_Utagaji wa mayai kupungua sana.
UKIUPASUA MZOGA
1 Utumbo kuonekana na damu
2Utumbo butu kuwa na damu damu
3Utumbo butu kuvimba
4Utumbo sehemu za ndani kuonekana kama vile umesagika,cloaca ya kuku hubadilika rangi na kuwa na vidotidot kama vya damu tunaita [hemorrhage]
KUZUIA UGONJWA HUU:
_ Epeka hali ya unyevu unyevu katika banda la kuku
_Ni muhimu kizingatia hali ya usafi kwenye banda la kuku
MATIBABU YA UGONJWA WA COCCIDIOSIS.
_Esb3 _Anticox _Vitacox _Amprolium_[ dawa yeyote kati ya hizo]
Dawa yeyote kati ya hizo changanya na vitamin
Maoni na ushauri Whatsapp 0655610894
Ukiwa na swali comment hapo chini
SAKINISHA APP YA BLOG HII PLAY STORE GUSA HAPA
TEMBELEA BLOG HII KILA SIKU
from FUGA KIBIASHARA http://ift.tt/2BMNmPI
No comments:
Post a Comment