VENT PROLAPSE UGONJWA WA KUKU UNAO WASUMBUA WENGI - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Thursday, December 21, 2017

VENT PROLAPSE UGONJWA WA KUKU UNAO WASUMBUA WENGI


SOMO: MAGONJWA/TIBA/KINGA.

VENT PROLAPSE

Kutoka kwa nyama ya ndani ya  sehemu ya haja kuja nje na mara nyingi huwa na rangi nyekundu.

Tatizo hili huwa tokea watu wengi sana, na huwa likiwepo katika maswali mengi leo acha tuliongelee hili

CHANZO CHA TATIZO HILI

Tatizo hili mara nyingi hukumba kuku wa mayai, broiler au aina nyingine tofauti na hizi:
_Kuku kulishwa chakula chenye protein nyingi
_Kuku mwenye uzito mdogo kutaga mayai
_Ukubwa wa mayai
_Ukosefu wa madini joto (calcuim) ambayo husababisha kuku kushindwa kusukuma mayai

KWA KUKU BROILER

 Tatizo hili ni mara chache sana kutokea kwa kuku wa nyama/ broiler
-Kuku wa nyama hupatwa  na tatizo hili kutokana na kupewa chakula chenye mchanganyiko usio sahihi(ratio) hii hupelekea kuku kushindwa kumeng'enya chakula kwa usahihi na kusababisha kuku kutoa kinyesi kigumu na kusabaabisha kutoka kwa nyama sehemu ya haja pale anapo jisaidia.

TIBA
-Endapo tatizo hili litatokea Unashauri kutumia mafuta (ointment) kumpa huyu kuku hata matone matatu ili kuweza kulainisha mmeng'enyo..
_Kutumia mchanganyo sahihi kwa kuku sio chakula cha kuku wa mayai kuwapa kuku wa nyama au hata kuku wanyama kumpa kuku wa mayai..
-Kutumia njia ya kawaida kurudisha hiyo nyama iliyo toka nje safisha hiyo nyama kwa maji safi kisha rudisha ndani pole pole kwa kutumia kidole.

DAWA

-Tumia  antibiotic mfano Otc 20% changanya na Electrolytes,

Kama ukiikosa Electrolytes   tumia antibiotic Otc 20% + vitamin

Ahsante kwa leo tuishie hapo.

SAKINISHA APP YA UFUGAJI BOFYA HAPA

Kwa maoni na ushauri, mafunzo ya ufugaji Whatsapp 0655610894

TEMBELEA BLOG HII KILA SIKU



from FUGA KIBIASHARA http://ift.tt/2BtsoWM

No comments:

Post a Comment