Ndugu mpenzi msomaji, leo nataka nikupe elimu kidogo kuhusiana na faida za kuhasi nguruwe, japo ni somo fupi ila litakupa uelewa wa kutosha kuhusiana na kuhasi nguruwe. Ila kabla nitakufahamisha maana ya kuhasi.
Kuhasi, ni kitendo cha kuondoa sehemu za mbegu za kiume (testicles) za mnyama, mara nyingi kuhasi hufanyika kwa ng'ombe na ng'uruwe.Ila kitendo cha kuhasi hufanyika kwa madume ambao huandaliwa kwa lengo la kuchinjwa.
SIFA YA NGURUWE ANAETAKIWA KUHASIWA
Sio kila nguruwe anaweza kuasiwa, hivyo ni muhimu sana kuaangalia kabla ya kuhasi ili kuepusha vifo visivyo vya lazima.
UMRI, japo hata nguruwe wakubwa wanaweza kuhasiwa, ila ni vizuri zaidi nguruwe ahasiwe akiwa na umri mdogo yaani kuanzia wiki 2, hii itapunguza usumbufu ambao unaweza kujitokeza pengine kusababisha madhara.
AFYA, pia ni lazima sana kuzingatia afya ya nguruwe kabla ya kumuhasi kwa sababu nguruwe akiwa na afya mbovu anaweza kushindwa kuhimili hivyo kumpelekea kufa. mfano nguruwe akiwa na ugonjwa wa scrotum hernia inaweza kupelekea utumbo kutoka nje hivyo nguruwe anaweza kufa.
FAIDA ZA KUHASI NGURUWE
Kama nilivyo sema awali kua nguruwe wanao hasiwa, huasiwa kwa lengo la nyama tu. hivyo zifuatazo ni baadhi ya faida ya kuhasi nguruwe.
- uongeza ubora wa nyama
- hupunguza usumbufu bandani
- upunguzo kusambaa kwa magonjwa ya tokanayo na ngono.
- uondoa sifa za mnyama ambazo hazitakiwi kusambaa bandani.
usisite kuendelea kua nasi.
USISAHAU KUPAKUA / KUDOWNLOAD APPLICATION YA KILIMO BORA IPO PLAY STORE ILI UPATE HABARI KWA URAHISI BONYEZA LINK HII KUDOWNLOAD ==> http://ift.tt/2tqvrGF
No comments:
Post a Comment