UTANGULI
Ndugu mpenzi msomaji asante kwa kuendelea kua nasi kila siku, naleo napenda nikupe elimu kuhusiana na kilimo bora cha zao la matango.
Asili ya matango ni katika bara la Asia au Africa, lakini kwa sasa ustawishwa katika maeneo mengi ya kitropikia. Matunda yake hukatwakatwa na kuliwa kama achali au kachumbari, au uwekwa kwenye siki na pia yanaweza kupikwa na kuliwa.
Katika nchi yetu ya Tanzania matango hulimwa katika mikoa ifuatayo; Tanga, Morogoro, Mbeya, Lindi, Mtwara na Pwani ambako kunajua la kutosha.
Wasiliana nasi kwa kubofya HAPA
AINA ZA MATANGO
Zipo aina nyingi za matango lakini huofautiana kwa umbo na rangi, aina zinazo jilikana na kulimwa hapa kwetu ni Colorado, Telegraph, Palmetto, Chicago, Pickling, Straight 8 na Marketer.
USTAWISHAJI NA HALI YA HEWA
Zao hili la matango huitaji hali ya joto ya wastani yaani nyuzi joto 20 hadi 25 na hukua kwa haraka sana, matango usitwai katika aina nyingi za udongo na huitaji umbali wa sentimita 60 hadi 75 kati ya mmea na mmea na hizo hizo kati ya msitari na msitari. na mimea michanga hutakiwa kuwekewa kinga ili isidhuriwe na upepo.
UDONGO
Matango hukua na kustawi kwa haraka katika udongo mwepesi, lakini utoa mavuno mengi zaidi katika udongo mzito kiasi, hataivyo ardhi inayo tuamisha maji haifai katika kilimo cha matango na ikibidi yapandwe katika matuta. hata hivyo zao hili utumia chakula kingi zaidi kutoka ardhini hivyo ni muhimu kuweka samadi au mboji mara kwa mara shambani ili kuongeza chakula cha mimea.
UANDAAJI WA SHAMBA
Kabla ya kupanda udongo unatakiwa utifuliwe vizuri na majani yaondolewe kabisha shambani, usafi wa bustani ni muhimu ili kuweza kuondo mmea mingine inayo weza kua kero kwa matango.
MATANDAZO
Mkulima unaweza kutumia nyasi au mabaki ya mmea mingine katika kufunika ardhi, baada ya mmea kuanza kutambaa unaweza kuweka matandazo ili kuweza kuzuia upotevu wa unyevu nyevu shambani, kupunguza kasi ya magugu na pia matandazo yanapo oza huongeza rutuba zaidi shambani.
UPANDAJI
Ni vizuri zaidi mkulima kupanda mbegu moja kwa moja shambani, sia mbegu moja kwa umbali wa sentimita moja kwenda chini na pia umbali kati ya mbegu na mbegu usipungue sentimita 30.
sehemu ya kupanda iwe na jua la kutosha kwani matango huitaji jua lisilo pungua masaa 6- 8 kwa siku, mwagilia maji ya kutosha angalau mara moja kwa siku hasa wakati wa jioni.
PALIZI
Hii ni muhimu kwani usaidia kupunguza baadhi ya magonjwa na mgawanyo wa chakula na magugu, tumia jembe la mkono ili kuzuia kujeruhi mazao.
MAGONJWA
- Mnyauko bakteria (bacteria wilt), hushambulia majani na kuyafanya kudhoofika na baadae kufa kabisa, ili kuzuia nyunyuzia dawa ya copper kila baada ya siku 10 na pia tumia mbegu zenye uvumilivu mkubwa kama palmetto
- ubwiri unga au ukungu (powdery mildew), ukungu ushambulia majani a mashina, zuia kwa kunyunyuzia dawa ya unga ya sulphur kila baada ya siku 10
- magonjwa ya virusi (cucumber mosaic virus), ugonjwa huu usababishwa na virusi, isipo tibiwa mapema mimea ugeuka na kua yanjano na kushindwa kutoa mazao, ugonjwa huu uenezwa na wadudu kama vidukari na nzi weupe.kudhibiti fanya usafi unao itajika shambani kama vile kuondoa na kuchoma taka
- Dudu kobe wa matango, huyu ni moja kati ya wadudu hatari kwani hutafuna miche ya matango pale inapo chipua na uafuna majani ya mimea michanga.
- funza(pickel worm), hawa wadudu hupenya kwenye ua na kutafuna baada ya kumaliza huamia kwenye tunda.dhibiti kwa kutumia dawa za rote- none au crylite kila baada ya juma moja.
- vidukari au vidudu mafuta(aphids), wadudu hawa ufyonza utomvu wa mmea na kuufanya ushindwe kuzaa matunda dhibiti kwa kutumia dawa za marathion au nicotine na hakikisha dawa inafikia sehemu ya chini ya majani
KUVUNA
Matango hua tayari kuvunwa pale yanapofikisha siku 50 hadi 60 baada ya kupandwa , pia matunda hutakiwa kua na urefu wa sentimita 15 hadi 20 hii inategemea na aina.
baada ya mvuno wa kwanza mkulima hutakiwa kusubili kwa kipindi cha wiki 3 hadi kuvuna mvuno wa pili.
Nitumaini langu umejifunza kitu kuhusiana na kilimo cha matango, hivyo usisite kuwasiliana NASI kwa ushauri, elimu zaidi au kwa jambo lolote lile kuhusiana na kilimo na mifugo.
Unaweza kuendelea kufatilia makala nyingine nyingi zaidi kupitia UKURASA WETU
USISAHAU KUPAKUA / KUDOWNLOAD APPLICATION YA KILIMO BORA IPO PLAY STORE ILI UPATE HABARI KWA URAHISI BONYEZA LINK HII KUDOWNLOAD ==> http://ift.tt/2tqvrGF
No comments:
Post a Comment