MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,amekiagiza Chama Cha Ushirika cha Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU), kumnyang'anya mwekezaji wa Kichina M/S Guoming Tang ,hekari 300 kati ya 380 alizozihodhi,ili zitumiwe na wakulima msimu mpya wa kilimo.
Aidha ameuagiza ushirika huo, halmashauri ya Chalinze na serikali ya wilaya ya Bagamoyo kukakikisha hekta 1,800 kati ya 3,209 zilizopo kwenye shamba hilo ,zinatumika kupandwa mikorosho ya kisasa.
Ndikilo aliyatoa maagizo hayo wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa kilimo ikiwemo mpunga msimu wa 2018/2019.
Alisema ,mwekezaji huyo anapaswa kubakia na eneo atakaloweza kulifanyia kazi kuliko kuchukua eneo kubwa ambalo analikodisha na kujinufaisha nalo.
"Tena asisuesue ,nashukuru uongozi wa CHAURU uliopo umefanyia kazi maelekezo aliyoyatoa Naibu Waziri kilimo, uvuvi na mifugo, William Ole Nasha na mie naagiza ,maelekezo hayo yafanyiwe kazi;"
"Msikubali kuwa watumwa kwenye ardhi na nchi yenu ,nasikia ameanza kutoa baadhi ya vitu vyake hivyo anyanganywe eneo hilo ,na nitakuja tena hapa kuona kama eneo hilo amenyang'anywa" alisisitiza.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani ,alikemea tabia inayofanywa pia na baadhi ya watu ya kuchukua maeneo makubwa kwenye shamba hilo na kuyakodisha.
Ndikilo ,alieleza ni marufuku kuwa madalali kwa kukodisha maeneo badala ya kulima wenyewe.
Pamoja na hayo ,alisema CHAURU ina eneo lenye hekta 3,209 ,ambapo zinazotumika katika Kilimo cha umwagiliaji ni 720 ,hivyo alielekeza hekta 1,800 zitumiwe kwenye kilimo kingine cha korosho .
"Leo hii mnaweza mkadharau lakini niwahakikishie miaka ijayo ,wakati mkifanikiwa katika kilimo hiki cha korosho ,mtanikumbuka ," alisema Ndikilo.
Akizungumzia msimu mpya wa kilimo ,Ndikilo aliwataka wakulima mkoani Pwani kulima kilimo cha kisasa kwa kujipanga kutumia zana za kisasa.
Alikemea kulea migogoro na uchochezi inayofanywa na baadhi ya wanachama na kusema atakaejihusisha na vitendo hivyo achukuliwe hatua hata kufukuzwa uanachama.
Mkuu Wa Mkoa Wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,akizindua msimu Mpya Wa Kilimo 2018/2019,ikiwemo mpunga, Mkoani hapo ,kwa kulima kisasa kwa kutumia trekta
Mkuu Wa Mkoa Wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo akikagua mchele unaolimwa kupitia chama cha ushirika cha wakulima wa umwagiliaji Ruvu (CHAURU )wilayani Bagamoyo
Mkuu Wa Mkoa Wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo, akizungumza jambo kabla ya kuzindua msimu mpya wa Kilimo 2018/2019 katika mashamba ya Ushirika wa CHAURU ,huko Ruvu,Bagamoyo mkoani Pwani.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
USISAHAU KUPAKUA / KUDOWNLOAD APPLICATION YA KILIMO BORA IPO PLAY STORE ILI UPATE HABARI KWA URAHISI BONYEZA LINK HII KUDOWNLOAD ==> http://ift.tt/2tqvrGF
No comments:
Post a Comment