Jifunze Kutengeneza Mchwa Kwaajili Ya Kuku - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Tuesday, February 6, 2018

Jifunze Kutengeneza Mchwa Kwaajili Ya Kuku


KANUNI AU HATUA ZAKUFUATA KUTENGENEZA MCHWA 
Unaweza tazama video hiyo apo juu
1. Andaa mahitaji muhimu yanatakiwa -kinyesi kikavu cha ngombe au mbuzi -majani makavu,au mabua ya mahindi,maharage hata maranda unaweza tumia mojawapo au ukachanganya -chungu,au sufuria au box 2. Changanya vitu tajwa hapo juu vyote vizuri 3. Nyunyizia maji kila kilichomo kilowane kiasi 4. Weka mchanganyo wako kwenye chombo ulichokiandaa,chungu,sufuria au box 5. Chukua chombo hicho kakiweke sehemu ambayo unahisi mchwa wanaweza kupatika mfano,kichuguu, kwenye njia mchwa, sehemu nyingi ya ardhi kavu mchwa wanapatika 6. Acha chombo chako hapa kwa masaa 24, ila chombo umekiweka kwa kukifunika upande mmoja uwe umenyanyuka kidogo kuruhusu hewa kuingia kwenye mchanganyiko 7. Baada ya huo muda mchwa wengi watakuwa wamezalishwa ndani ya chombo chako 7. Chukua chombo kwa upesi kwa kukigeuza ili mchwa usirudi aridhini kisha kawape kuku wako, zoezi hili ni jipesi sana halihitaji wewe kutumia muda mwingi fanya kila siku ili vifaranga na kuku wako wastawi vizuri.



from FUGA KIBIASHARA http://ift.tt/2nJGxq3

No comments:

Post a Comment