MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MTADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI. Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka. Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine. Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae. Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula. Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia. Mchanganuo Wa 69500 ni:- Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70. - paraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku. -mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500 - layer's consetraite Kilo 25 kifuko. = 21500. Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8. Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi. Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300. Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu. TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU. Mchanganuo wake Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000. Jogoo 1 = 20000 Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000. Itakuwa imebaki shs. 60500 -Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi
from Kijana Endelevu Group http://ift.tt/2E1NNng
USISAHAU KUPAKUA / KUDOWNLOAD APPLICATION YETU INAYOITWA KILIMO CHA KISASA SASA INAPATIKANA PLAY STORE BUREEE KABISA
No comments:
Post a Comment