Badili Maisha Yako Kwa Kuwekeza Kwenye KIlimo Cha Vitunguu Swaumu - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Wednesday, October 10, 2018

Badili Maisha Yako Kwa Kuwekeza Kwenye KIlimo Cha Vitunguu Swaumu

Mahitaji ya hali ya hewa na udongo
Zao hili hupendelea hali ya hewa ya baridi na udongo tifu tifu na wenye rutuba. Sehemu
nyingi zinazostawi vitunguu maji hufaa pia kwa zao hili. Maeneo ya mwinuko wa kiasi
cha zaidi ya mita 1000 juu ya usawa wa bahari hufaa zaidi

Maandalizi ya shamba
Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sen-
timita 30 hadi 45 Weka matuta ya mwinuko yenye upana wa mita 1 hadi mita 1.5 kutoka kati kati ya
tuta na tuta na upana wa mita 1

Maandalizi ya Mbegu
Kwanyua vipande/Vikonyo vya vitunguu sumu tayari kwa ajili ya kupanda katika nafasi. Mbegu sharti iwe imekaa kwa miezi mitano hadi sita tangu kuvuna ili iweze kuota. Ni muhimu kwa mkulima kupata ushauri wa kitaalam ili kujua namna ya kutam- bua mbegu ya vitunguu saumu iliyo tayari kwa kupanda kwani ikipandwa kabla haijawa tayari haioti

Upandikizaji
Tumia mashine alama kuweka alama za kupandia katika nafasi ya sentimita 15 hadi sentimita 25 na mistari minne hadi sita kwa tuta Hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda

Palizi
Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu Magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu.

Mbolea
Tumia mbolea ya DAP wakati wa kupanda, CAN ama SA wiki tatu baadaye na kisha tumia NPK wiki sita baada ya kupanda. Matumizi ya mbolea za maji yafanyike kila baada ya wiki mbili kutegemea na mahitaji.

Matumizi ya viuatilifu
Matumizi ya viuatilifu yafanyike kila baada ya wiki mbili kwa ushauri wa wataalam

Mavuno
Vitunguu saumu hukomaa miezi 6 tangu kupanda

Bei ya mbegu hizi ni tsh 30,000/= kwa kopo la lita moja(1) na tsh 600,000/= kwa ndoo ya lita ishirini.

Guarantee: Ndoo ya lita 20 ambayo ni sawa na makopo 20 ya lita moja inatosha kupanda eneo la hekari 1 (m70*m70) na kiwango cha chini cha mavuno ni gunia 100 na kiwango cha juu ni gunia 110-120 ndani ya siku 90 (3 months) toka kupanda. Gunia moja sokoni kariakoo, ilala, buguruni, temeke na mabibo kwa sasa bei ni tsh 130,000/= * gunia 100 = tshs 13,000,000/= ndani ya miezi 3

No comments:

Post a Comment