Habari ndugu msomaji wa wetu wa makala za kilimo, Natumaini tunaendelea vizuri na mapambano ya kila siku. Leo tutaanza kujifunza kilimo cha bora cha nyanya, na tutaanza kufahamu vitu vya msingi kwanza, na natumaini ukimaliza mfululizo wa makala hizi utakua mkulima hodari wa nyanya. Kila kitu lazima kiwe na msingi imara, karibu tujifunze wote: Utangulizi: • Nyanya ni zao la mboga ambalo hulimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Inahisiwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru/Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu. Uzalishaji wa nyanya duniani na hapa Tanzania Nchi zinazolima nyanya kwa wingi duniani ni pamoja na USA, Italia na Mexico. Kwa upande wa Africa nchi zinazo lima ni kama; Malawi, Zambia na Botswana. Zao hili hulimwa pia katika nchi za Africa Mashariki, ikiwemo Kenya, uganda na Tanzania. Zao la nyanya linalimwa karibu maeneo yote ya Tanzania. Uzalishaji wa nyanya ni mkubwa kuliko mazao mengine ya mbogamboga yanayolimwa hapa Tanzania, uzalishaji wa nyanya kwa mwaka ni jumla ya tani 129,578 ikiwakilisha asalimia 51 ya mazao yote ya mboga. Kwa mujibu wa Wizara ya kilimo ya Tanzania maeneo yanalolima sana nyanya ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro (Hai, Moshi na Rombo), Arusha (Arumeru), Morogoro (Mgeta), Tanga (Lushoto), Mbeya (Mbeya vijijini) na Singida. Morogoro ndiyo inayoongoza kwa kilimo hichi ikiwa na wazalishaji wenye zaidi ya hekta 6,159 (ekari 15,398). Pamoja na kwamba eneo la uzalishaji linaongezeka kwenye maeneo mengi lakini uzalishaji wa nyanya bado ni mdogo sana. Uzalishaji mdogo unasababishwa na kupungua kwa rutuba ya ardhi, upepo, joto, ukame. Sababu nyingine ni pamoja na ukosefu wa aina za nyanya zenye mavuno mengi amabazo zinahimili mazingira ya kwetu, wadudu, magonjwa na magugu. Mazingira • Hali ya Hewa: Nyanya hustawi vizuri zaidi kwenye mazingira ya joto la wastani kuanzia nyuzi joto 18-27 sentigreti. Mvua nyingi husababisha mlipuko wa magonjwa ya ukungu kama vile Baka jani chelewa n.k.) • Udongo: Nyanya hustawi kwenye aina zote za udongo kuanzia udongo wa kichanga, mweupe wa tifutifu hadi udongo wa mfinyanzi, ili mradi uwe na mboji ya kutosha na usiosimamisha/tuamisha maji. Pia uwe na uchachu wa wastani yaani pH 6.0 - 7.0. Aina za Nyanya Kutokana na tabia ya ukuaji, nyanya zinagawanyika katika makundi mawili: 1. Aina ndefu ( intermediate) kwa mfano ANNA F1, Tebgeru 97. Aina hizi hufanya vizuri zaidi zinapopandwa ndani ya greenhouse. Uvunaji wake ni wa muda mrefu, zipo ambazo zinavunwa hata zaidi ya miezi 6, yaani hiyo miezi 6 ni ya uvunaji. 2. Aina fupi (determinate) kwa mfano Tanya, Cal J, Mwanga, Onyx, Roma VF (nyanya mshumaa) Kotokana na uchavushaji, nyanya zinagawanyika makundi mawaili: 1. OPV (Open Pollinated Variety) - Aina za kawaida 2. Hybrid – Chotara: Hizi ni aina zenye mavuno mengi, kati ya hizo zipo aina fupi na ndefu. Katika karne hii ya 21, nyanya zinazopendelewa kulimwa zaidi na wakulima, ni zile zinazoweza kuvumilia magonjwa, zinazo zaa sana, na zenye ganda gumu ili kufanikisha usafirishaji, na kuhifadhika kwa siku nyingi bila kuharibika mapema. Kuandaa Kitalu cha Nyanya Mambo muhimu ya kuzingatia: • Kitalu kiwe karibu na maji ya kutosha na ya kudumu • Kiwe sehemu iliyowazi na yenye udongo ulio na rutuba ya kutosha • Eneo la kitalu kama ni kubwa liwe tambarare au na mwiinuko kidogo ili kuepuka maji yasituame kwenye kitalu, mtelemko ukiwa mkali sana nao sio mzuri kwani husababisha mmomonyoko wa udongo. • Kitalu kiwe sehemu ambayo haikuwa na zao la nyanya au viazi mviringo (au mazao ya jamii ya nyanya k.m. mnavu, biringanya n.k.) • Kiwe sehemu ambayo ni rahisi kupata huduma zote muhimu kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na uhamishaji wa miche kwenda sehemu nyingine. Pia kurahisisha usambazaji wa miche kwenda sehemu nyingine. Kuandaa Matuta ya Kusia Mbegu za Nyanya Aina ya matuta: – matuta ya makingo (sunken seed bed) – matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed bed) – matuta ya kawaida (flat seed beds) Mambo Muhimu ya Kuzingatia wakati wa Kuandaa Matuta • Tuta liwe na upana kati ya sentimita 90-120, na urefu wowote, [ili mradi muhudumu anaweza kutoa huduma nyingine zote kitaluni bila kukanyaga miche]. • Kwatua/lima kina kirefu cha kutosha kiasi cha sentimita 15-20 ili mizizi iweze kusambaa vizuri ardhini. • Choma takataka juu ya kitalu, au funika tuta kwa nailoni, majuma 4-8 ili kuua vimelea vya magonjwa na wadudu. • Wakati wa kuandaa, kitalu, ongeza mbolea aina ya samadi/vunde au mboji kwenye udongo kisha kwatua ili ichanganyike vizuri na udongo. • Changanya kiasi cha debe 1 hadi 2 kila baada ya mita moja (hatua moja) mraba. • Tuta lisiwe na mabonde mabonde au mawe mawe ambayo yanaweza kuzuia usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta, lisawazishwe vizuri ili kuhakikisha usambazaji mzuri wa mbegu na kuepuka mbegu kufukiwa chini mno kiasi ambacho hazitaota. Faida na Hasara za Matuta yaliyotajwa hapo juu 1. Matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed beds); – matuta ya namna hii huruhusu maji, hewa na mizizi kupenya kwenye udongo kwa urahisi zaidi. – Mazao ya mizizi hupata nafasi ya kutosha kutanuka haraka zaidi – Matuta haya hayatuamishi maji kama mengine, hivyo hutumika zaidi kwenye maeneo yanayokuwa na mvua mara kwa mara. Hasara: o Matuta ya namna hii yana sababisha sana mmomonyoko wa udongo kama hayakutengenezwa vizuri. 2. Matuta ya makingo (sunken seed beds): Faida: · matuta haya ni rahisi kutengeneza · hutumika wakati wa kiangazi ili kuhifadhi maji na unyevu · nyevu mdogo unaopatikana ardhini · ni rahisi kumwagilia kwa kutumia maji ya mfereji au bomba · huhifadhi unyevu nyevu kwenye ardhi kwa muda mrefu · huzuia mmomonyoka wa ardhi Hasara: · Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye · mvua nyingi. 3. Matuta ya kawaida (flat seed beds): Faida: · ni rahisi sana kutengeneza kwani udongo ukisha kwatuliwa · na kusambazwa mbegu huoteshwa · ni rahisi kutumia eneo kubwa kuotesha mbegu Hasara: Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye mvua nyingi. Kusia Mbegu • Hakikisha ubora na uotaji wa mbegu kabla ya kuzipanda kitaluni (germination test) • Weka mistari kwenye tuta kulingana na ukubwa wa tuta, lakini mistari isiwe chini au zaidi ya sentimita 15-20 toka mstari hadi mstari • Kina cha mistari kisiwe cha kutisha bali kiwe kati ya sentimita 1-2 • Matuta yapate maji ya kutosha siku moja kabla ya kusia mbegu. Ni vizuri kutumia chombo cha kumwagilia (watering can). • Mbegu ziatikwe kwenye mistari na zisambazwe vizuri ili kufanikisha usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta. Changanya mchanga laini na mbegu kisha sambaza kwenye mistari iliyoandaliwa kwenye tuta. Mbegu zinaweza pia kuatikwa kwenye tuta bila mistari, lakini zisambazwe kwa uwiano mzuri kwenye tuta ili kupunguza msongamano. Msongamano husabisha magonjwa ya fangasi kama vile kinyausi (damping off) au ukungu (blight). • Weka matandazo kiasi cha kutosha ambacho hakitazuia kuota kwa mbegu. • Mara baada ya kuatika mbegu, mwagilia maji kiasi cha kutosha kulingana na unyevu nyevu ulioko ardhini Mambo ya Kuzingatia baada ya kusia mbegu pamoja na Matunzo Kitaluni • Mwagilia maji kwenye kitalu baada ya kuotesha kulingana na unyevu nyevu uliopo kwenye udongo. • Miche yote ikisha ota, ondoa matandazo, kisha weka chanja ili kupunguza mionzi ya jua ambayo inaweza kuunguza miche michanga. (kipindi cha baridi si muhimu sana) • Punguzia miche (thinning) ili ibakie kwenye nafasi ya kutosha. Hivyo miche ibakie kwenye umbali wa sentimita 2.5 - 4. Hii itapunguza magonjwa ya ulemavu na mnyauko, pia itasaidia kupata miche bora na yenye nguvu. • Endelea kumwagilia hadi miche ifikie kimo kinachofaa kuhamishia shambani. • Punguza kiwango cha umwagiliaji maji, siku chache kabla ya kuhamishia miche shambani, yaani siku 7-10. Kanuni na Mbinu za kuhamisha miche toka Kitaluni kwenda shambani (Transplanting Rules) • Mwagilia miche masaa machache kabla ya kuhamishia miche shambani ili wakati wa kung’oa miche mizizi ishikamane vizuri na udongo. • Kabla ya kuhamisha miche, mashimo yawe yamekwisha andaliwa katika nafasi zinazo stahili huko shambani. • Miche ihamishwe wakati wa jioni ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na jua. • Kwa ujumla karibu mazao yote ya mboga mboga huwa tayari kuhamishiwa shambani yakiwa na majani kamili kati ya 2-6 pamoja na mizizi mingi iliyostawi vizuri. • Mche lazima uwe na afya nzuri, uwe umenyooka vizuri, hivyo miche yote iliyonyongea au myembamba kupita kiasi isichukuliwe wakati wa kupeleka shambani. • Ng’oa miche kwa uangalifu hasa pamoja na udongo wake kwa kutumia vifaa husika ili mizizi isidhurike. • Miche ihamishiwe shambani mapema mara baada ya kung’olewa toka kitaluni. • Wakati wa kuhamisha miche, uangalifu mkubwa utumike ili kutoharibu miche/mizizi. Maandalizi ya Shamba la Nyanya • Shamba la nyanya liandaliwe mwezi 1-2 kabla ya kupanda miche. • Mara baada ya kulima choma nyasi juu ya udongo au ondoa magugu yote yanayoweza kuhifadhi wadudu na magonjwa ya nyanya. • Siku moja au mbili kabla ya kuhamishia nyanya shambani, mwagilia sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuhamishia nyanya. • Nafasi kati ya mche hadi mche ni wastani wa sentimita (50-60) x (50-75) kutegemeana na aina au hali ya hewa. Kama ni kipindi cha baridi ni vyema nyanya zikapandwa mbalimbali ili kuruhusu mzungungo wa hewa na kuzuia magonjwa ya fangasi. Jinsi ya kupanda miche: • Hamisha miche toka kitaluni pamoja na udongo wake • Sambaza mizizi vizuri kwenye shimo bila kukunja. • Fukia miche kina kile kile ambacho shina lilikuwa limefukiwa bustanini. • Mwagilia maji ya kutosha kulingana na unyevunyevu uliopo kwenye udongo kasha weka matandazo na kivuli ili kupunguza uharibifu unaosababishwa na mionzi ya jua. Mambo muhimu ya kuzingatia baada ya kuhamishia Miche Shambani • Kagua shamba mara kwa mara ili kujua maendeleo au matatizo yaliyoko shambani mapema • Hakikisha shamba ni safi wakati wote, palilia shamba na hakikisha magugu yote hasa yale ya jamii ya nyanya yamelimiwa chini. • Ondoa mimea iliyoshambuliwa na magonjwa au ondoa sehemu zilizoshambuliwa, kisha zifukiwe chini au kuunguza moto. • Punguza matawi na vikonyo ili kuongeza mwanga wa kutosha kwenye nyanya pamoja na kuruhusu mzunguko wa kutosha wa upepo na kusababisha mazingira magumu ya wadudu maadui kwenye nyanya, hasa wale wanaopenda kiza na magonjwa yanayopendelea unyevunyevu. Asante sana: - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Thursday, October 11, 2018

Habari ndugu msomaji wa wetu wa makala za kilimo, Natumaini tunaendelea vizuri na mapambano ya kila siku. Leo tutaanza kujifunza kilimo cha bora cha nyanya, na tutaanza kufahamu vitu vya msingi kwanza, na natumaini ukimaliza mfululizo wa makala hizi utakua mkulima hodari wa nyanya. Kila kitu lazima kiwe na msingi imara, karibu tujifunze wote: Utangulizi: • Nyanya ni zao la mboga ambalo hulimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Inahisiwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru/Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu. Uzalishaji wa nyanya duniani na hapa Tanzania Nchi zinazolima nyanya kwa wingi duniani ni pamoja na USA, Italia na Mexico. Kwa upande wa Africa nchi zinazo lima ni kama; Malawi, Zambia na Botswana. Zao hili hulimwa pia katika nchi za Africa Mashariki, ikiwemo Kenya, uganda na Tanzania. Zao la nyanya linalimwa karibu maeneo yote ya Tanzania. Uzalishaji wa nyanya ni mkubwa kuliko mazao mengine ya mbogamboga yanayolimwa hapa Tanzania, uzalishaji wa nyanya kwa mwaka ni jumla ya tani 129,578 ikiwakilisha asalimia 51 ya mazao yote ya mboga. Kwa mujibu wa Wizara ya kilimo ya Tanzania maeneo yanalolima sana nyanya ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro (Hai, Moshi na Rombo), Arusha (Arumeru), Morogoro (Mgeta), Tanga (Lushoto), Mbeya (Mbeya vijijini) na Singida. Morogoro ndiyo inayoongoza kwa kilimo hichi ikiwa na wazalishaji wenye zaidi ya hekta 6,159 (ekari 15,398). Pamoja na kwamba eneo la uzalishaji linaongezeka kwenye maeneo mengi lakini uzalishaji wa nyanya bado ni mdogo sana. Uzalishaji mdogo unasababishwa na kupungua kwa rutuba ya ardhi, upepo, joto, ukame. Sababu nyingine ni pamoja na ukosefu wa aina za nyanya zenye mavuno mengi amabazo zinahimili mazingira ya kwetu, wadudu, magonjwa na magugu. Mazingira • Hali ya Hewa: Nyanya hustawi vizuri zaidi kwenye mazingira ya joto la wastani kuanzia nyuzi joto 18-27 sentigreti. Mvua nyingi husababisha mlipuko wa magonjwa ya ukungu kama vile Baka jani chelewa n.k.) • Udongo: Nyanya hustawi kwenye aina zote za udongo kuanzia udongo wa kichanga, mweupe wa tifutifu hadi udongo wa mfinyanzi, ili mradi uwe na mboji ya kutosha na usiosimamisha/tuamisha maji. Pia uwe na uchachu wa wastani yaani pH 6.0 - 7.0. Aina za Nyanya Kutokana na tabia ya ukuaji, nyanya zinagawanyika katika makundi mawili: 1. Aina ndefu ( intermediate) kwa mfano ANNA F1, Tebgeru 97. Aina hizi hufanya vizuri zaidi zinapopandwa ndani ya greenhouse. Uvunaji wake ni wa muda mrefu, zipo ambazo zinavunwa hata zaidi ya miezi 6, yaani hiyo miezi 6 ni ya uvunaji. 2. Aina fupi (determinate) kwa mfano Tanya, Cal J, Mwanga, Onyx, Roma VF (nyanya mshumaa) Kotokana na uchavushaji, nyanya zinagawanyika makundi mawaili: 1. OPV (Open Pollinated Variety) - Aina za kawaida 2. Hybrid – Chotara: Hizi ni aina zenye mavuno mengi, kati ya hizo zipo aina fupi na ndefu. Katika karne hii ya 21, nyanya zinazopendelewa kulimwa zaidi na wakulima, ni zile zinazoweza kuvumilia magonjwa, zinazo zaa sana, na zenye ganda gumu ili kufanikisha usafirishaji, na kuhifadhika kwa siku nyingi bila kuharibika mapema. Kuandaa Kitalu cha Nyanya Mambo muhimu ya kuzingatia: • Kitalu kiwe karibu na maji ya kutosha na ya kudumu • Kiwe sehemu iliyowazi na yenye udongo ulio na rutuba ya kutosha • Eneo la kitalu kama ni kubwa liwe tambarare au na mwiinuko kidogo ili kuepuka maji yasituame kwenye kitalu, mtelemko ukiwa mkali sana nao sio mzuri kwani husababisha mmomonyoko wa udongo. • Kitalu kiwe sehemu ambayo haikuwa na zao la nyanya au viazi mviringo (au mazao ya jamii ya nyanya k.m. mnavu, biringanya n.k.) • Kiwe sehemu ambayo ni rahisi kupata huduma zote muhimu kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na uhamishaji wa miche kwenda sehemu nyingine. Pia kurahisisha usambazaji wa miche kwenda sehemu nyingine. Kuandaa Matuta ya Kusia Mbegu za Nyanya Aina ya matuta: – matuta ya makingo (sunken seed bed) – matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed bed) – matuta ya kawaida (flat seed beds) Mambo Muhimu ya Kuzingatia wakati wa Kuandaa Matuta • Tuta liwe na upana kati ya sentimita 90-120, na urefu wowote, [ili mradi muhudumu anaweza kutoa huduma nyingine zote kitaluni bila kukanyaga miche]. • Kwatua/lima kina kirefu cha kutosha kiasi cha sentimita 15-20 ili mizizi iweze kusambaa vizuri ardhini. • Choma takataka juu ya kitalu, au funika tuta kwa nailoni, majuma 4-8 ili kuua vimelea vya magonjwa na wadudu. • Wakati wa kuandaa, kitalu, ongeza mbolea aina ya samadi/vunde au mboji kwenye udongo kisha kwatua ili ichanganyike vizuri na udongo. • Changanya kiasi cha debe 1 hadi 2 kila baada ya mita moja (hatua moja) mraba. • Tuta lisiwe na mabonde mabonde au mawe mawe ambayo yanaweza kuzuia usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta, lisawazishwe vizuri ili kuhakikisha usambazaji mzuri wa mbegu na kuepuka mbegu kufukiwa chini mno kiasi ambacho hazitaota. Faida na Hasara za Matuta yaliyotajwa hapo juu 1. Matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed beds); – matuta ya namna hii huruhusu maji, hewa na mizizi kupenya kwenye udongo kwa urahisi zaidi. – Mazao ya mizizi hupata nafasi ya kutosha kutanuka haraka zaidi – Matuta haya hayatuamishi maji kama mengine, hivyo hutumika zaidi kwenye maeneo yanayokuwa na mvua mara kwa mara. Hasara: o Matuta ya namna hii yana sababisha sana mmomonyoko wa udongo kama hayakutengenezwa vizuri. 2. Matuta ya makingo (sunken seed beds): Faida: · matuta haya ni rahisi kutengeneza · hutumika wakati wa kiangazi ili kuhifadhi maji na unyevu · nyevu mdogo unaopatikana ardhini · ni rahisi kumwagilia kwa kutumia maji ya mfereji au bomba · huhifadhi unyevu nyevu kwenye ardhi kwa muda mrefu · huzuia mmomonyoka wa ardhi Hasara: · Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye · mvua nyingi. 3. Matuta ya kawaida (flat seed beds): Faida: · ni rahisi sana kutengeneza kwani udongo ukisha kwatuliwa · na kusambazwa mbegu huoteshwa · ni rahisi kutumia eneo kubwa kuotesha mbegu Hasara: Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye mvua nyingi. Kusia Mbegu • Hakikisha ubora na uotaji wa mbegu kabla ya kuzipanda kitaluni (germination test) • Weka mistari kwenye tuta kulingana na ukubwa wa tuta, lakini mistari isiwe chini au zaidi ya sentimita 15-20 toka mstari hadi mstari • Kina cha mistari kisiwe cha kutisha bali kiwe kati ya sentimita 1-2 • Matuta yapate maji ya kutosha siku moja kabla ya kusia mbegu. Ni vizuri kutumia chombo cha kumwagilia (watering can). • Mbegu ziatikwe kwenye mistari na zisambazwe vizuri ili kufanikisha usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta. Changanya mchanga laini na mbegu kisha sambaza kwenye mistari iliyoandaliwa kwenye tuta. Mbegu zinaweza pia kuatikwa kwenye tuta bila mistari, lakini zisambazwe kwa uwiano mzuri kwenye tuta ili kupunguza msongamano. Msongamano husabisha magonjwa ya fangasi kama vile kinyausi (damping off) au ukungu (blight). • Weka matandazo kiasi cha kutosha ambacho hakitazuia kuota kwa mbegu. • Mara baada ya kuatika mbegu, mwagilia maji kiasi cha kutosha kulingana na unyevu nyevu ulioko ardhini Mambo ya Kuzingatia baada ya kusia mbegu pamoja na Matunzo Kitaluni • Mwagilia maji kwenye kitalu baada ya kuotesha kulingana na unyevu nyevu uliopo kwenye udongo. • Miche yote ikisha ota, ondoa matandazo, kisha weka chanja ili kupunguza mionzi ya jua ambayo inaweza kuunguza miche michanga. (kipindi cha baridi si muhimu sana) • Punguzia miche (thinning) ili ibakie kwenye nafasi ya kutosha. Hivyo miche ibakie kwenye umbali wa sentimita 2.5 - 4. Hii itapunguza magonjwa ya ulemavu na mnyauko, pia itasaidia kupata miche bora na yenye nguvu. • Endelea kumwagilia hadi miche ifikie kimo kinachofaa kuhamishia shambani. • Punguza kiwango cha umwagiliaji maji, siku chache kabla ya kuhamishia miche shambani, yaani siku 7-10. Kanuni na Mbinu za kuhamisha miche toka Kitaluni kwenda shambani (Transplanting Rules) • Mwagilia miche masaa machache kabla ya kuhamishia miche shambani ili wakati wa kung’oa miche mizizi ishikamane vizuri na udongo. • Kabla ya kuhamisha miche, mashimo yawe yamekwisha andaliwa katika nafasi zinazo stahili huko shambani. • Miche ihamishwe wakati wa jioni ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na jua. • Kwa ujumla karibu mazao yote ya mboga mboga huwa tayari kuhamishiwa shambani yakiwa na majani kamili kati ya 2-6 pamoja na mizizi mingi iliyostawi vizuri. • Mche lazima uwe na afya nzuri, uwe umenyooka vizuri, hivyo miche yote iliyonyongea au myembamba kupita kiasi isichukuliwe wakati wa kupeleka shambani. • Ng’oa miche kwa uangalifu hasa pamoja na udongo wake kwa kutumia vifaa husika ili mizizi isidhurike. • Miche ihamishiwe shambani mapema mara baada ya kung’olewa toka kitaluni. • Wakati wa kuhamisha miche, uangalifu mkubwa utumike ili kutoharibu miche/mizizi. Maandalizi ya Shamba la Nyanya • Shamba la nyanya liandaliwe mwezi 1-2 kabla ya kupanda miche. • Mara baada ya kulima choma nyasi juu ya udongo au ondoa magugu yote yanayoweza kuhifadhi wadudu na magonjwa ya nyanya. • Siku moja au mbili kabla ya kuhamishia nyanya shambani, mwagilia sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuhamishia nyanya. • Nafasi kati ya mche hadi mche ni wastani wa sentimita (50-60) x (50-75) kutegemeana na aina au hali ya hewa. Kama ni kipindi cha baridi ni vyema nyanya zikapandwa mbalimbali ili kuruhusu mzungungo wa hewa na kuzuia magonjwa ya fangasi. Jinsi ya kupanda miche: • Hamisha miche toka kitaluni pamoja na udongo wake • Sambaza mizizi vizuri kwenye shimo bila kukunja. • Fukia miche kina kile kile ambacho shina lilikuwa limefukiwa bustanini. • Mwagilia maji ya kutosha kulingana na unyevunyevu uliopo kwenye udongo kasha weka matandazo na kivuli ili kupunguza uharibifu unaosababishwa na mionzi ya jua. Mambo muhimu ya kuzingatia baada ya kuhamishia Miche Shambani • Kagua shamba mara kwa mara ili kujua maendeleo au matatizo yaliyoko shambani mapema • Hakikisha shamba ni safi wakati wote, palilia shamba na hakikisha magugu yote hasa yale ya jamii ya nyanya yamelimiwa chini. • Ondoa mimea iliyoshambuliwa na magonjwa au ondoa sehemu zilizoshambuliwa, kisha zifukiwe chini au kuunguza moto. • Punguza matawi na vikonyo ili kuongeza mwanga wa kutosha kwenye nyanya pamoja na kuruhusu mzunguko wa kutosha wa upepo na kusababisha mazingira magumu ya wadudu maadui kwenye nyanya, hasa wale wanaopenda kiza na magonjwa yanayopendelea unyevunyevu. Asante sana:

Kwa kawaida makundi ya nyuki katika nchi ya Tanzania na baadhi ya nchi zinazolingana kwa tabia za nchi, makundi ya nyuki huanza kutafuta sehemu salama na yenye chakula kwa wingi kuanzia mwezi wa kumi katika mwaka mpaka mwezi wa nne kwa mwaka unaofuata.Kipindi hiki huwa na makundi mengi yanayozunguka hapa na pale kutafuta nyumba ambayo itawafaa kwa ajili ya makazi yao na kwa ajili ya kuhifadhia chakula.

Hiki ndio huwa kipindi muafaka sana kwa wafugaji kuanza kutega mizinga ambayo imeshaandaliwa kwa ajili ya kufugia nyuki.Kwa kuwa makundi mengi huwa yanatafuta sehemu za makazi hivyo ni rahisi sana kuyakama na kuyahifadhi makundi hayo kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya nyuki.

Kutokana na hilo, mfugaji anapaswa kuanza kuandaa sehemu ya kufugiua nyuki na mizinga yake mapema zaidi kabla ya msimu huo kufika ili asiweze kukosa makundi ya nyuki.Unashauriwa kuanza kuandaa mazingira ya kufugia nyuki na mizinga angalau mwezi mmoja kabla kwa kusafisha, kukarabati au kutengeneza kile unachokihitaji.

VIFAA VINAVYOPASWA KUANDALIWA.
Kabla ya kuanza kufuga nyuki kuna vifaa ambavyo mfugaji wanyukiu anapaswa kuanza kuviandaa mapema kabla ya msimu wa ufugaji wa nyuki kufika.Vifaa hivyo ni kama vifuatavyo:-

UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.
Eneo ambalo kuna wanyama wa aina mbalimbali ambao wanaweza kufanya uharibifu mbalimbali wa mizinga pindi ikiwa na nyuki na kusababisha uharibifu wa mizinga, kuua nyuki au hata mnyama mwenyewe kufa kutokana na kudungwa na nyuki.Hivyo ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki ni vyema ukafanyika.

DHAMIRA YA UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.
Mabanda hayo ya kufugia nyuki yanaweza kuwa ya udongo, tofali au ya miti pekee pande zote, milango pamoja na kuezekwa kwa nyasi.

Kuna sababu mbalimbali ambazo zinasababisha mfugaji nyuki kuweza kujenga mabanda ya kufugia nyuki, miongoni mwa sababu hizo ni:-

1. Kukinga mizinga na jua na mvua.
Hii ni sababu moja wapo ambayo inasababisha mfugaji wa nyuki kuamua kujenga mabanda ya kufugia nyuki, mzinga unapokuwa kwenye kivuli huusaidia mzinga kuweza kudumu kwa kipindi kirefu, pia kivuli husaidia nyuki kufanya kazi zao kwa juhudi.Iwapo mzinga utakuwa upo kwenye jua nyuki hutumia muda mwingi kupunguza joto la ndani ya mzinga badala kutumia muda huo kwa ajili ya kutafuta chakula.

Nyuki wanapoona jua ni kali zaidi na kusababisha joto kali ndani ya mzinga huamua kuhama katika mzinga huo na kwenda kutafuta makazi sehemu nyingine.Hivyo nio vyema mzinga ukakaa kwenye kivuli na sehemu isiyoweza kunyeshewa na mvua.

Pia mvua inaponyeshea mzinga husababisha mbao kuweza kuoza ndani ya muda mfupi, hivyo kwa kujengea banda la kufugia nyuki huweza kuukinga mzinga wako dhidi ya mvua ambayo inasababisha kuozesha mbao za mzinga wako.

2. Kukinga na wanyama waharibifu
Mabanda haya ya kufugia nyuki husaidia sana kwa wanyama waharibifu wa mizinga kushindwa kuifikia mizinga lakini pia husaidia sana kupunguza mashambulizi ya nyuki kwa viumbe wengine.Mizinga huwekwa ndani ya banda na banda kufungwa milango.

3. Ulinzi na ukaguaji
Ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki husaidia sana kuiweka mizinga yako sehemu salama dhidi ya wezi wa mizinga au asali lakini pia husaidia sana wakati wa uangalizi wa mzinga.Mizinga inapokuwa pamoja uangalizi wa mizinga hiyo huwa ni rahisi sana na pia huweza kusaidia kipindi cha uvunaji na uwekaji wa kumbukumbu za kila mara.

Pembeni ya banda hilo sehemu ambazo mizinga inawekwa huwekwa matundu maalumu ya kutoka na kuingia nyuki kwa ajili ya kujitafutia chakula chao.

MIZINGA YA KUFUGIA NYUKI.
Mizinga ya kufugia nyuki inapaswa kuandaliwa mapema kabla ya msimu wa kukamata makundi ya nyuki haujafika.Mizinga inayopaswa kuandaliwa ni kama ifuatayo:-

1. Mzinga wa kibiashara
Huu ni mzinga wa kisasa unaotumika kwa wafugaji wa nyuki hasa wale wanaotaka kuvuna asali kwa wingi kwa ajili ya kuuza.Mzinga huu huweza kuzalisha asali kwa wingi kadri misimu ya uvunaji inavyoongezeka mwaka hadi mwaka.

Mzinga huu una sehemu kuu tatu kama zifuatazo:-

A. Box la kuzalishia watoto wa nyuki
Ni box ambalo kwa kawaida huwa la kwanza kwa upande wa chini.box hili ndilo ambalo huwa na mlandfo wa nyuki kuingia na kutoka pindi wanapokwenda na kutoka kwenye utafutaji wa chakula. Box hili hutumika na malikia wa nyuki kwa kutagia mayai pamoja na kulelea watoto ambao husubiri kuanguliwa na kuwa nyuki kamili.

Pia box hili hutumika kwa ajili ya nyuki kuhifadhia chakula chao kwa ajili ya msimu wa kiangazi, msimu ambao huwa hauna maua yenye chakula cha nyuki cha kutosha,Hivyo mfugaji hapaswi kuvuna asali anayoikuta katika brood box, kwa kuvuna asali unayoikuta katika brood box husababisha kundi lako kuhama kwa kukosa chakula.

Kwa kawaida matumizi ya mzinga huu huanza kuvuna asali baada ya wastani wa misimu miwili mikubwa yaani sawa na miaka miwili.Na mara baada ya kipindi hicho kipita mfugaji huweza kuanza kuvuna kwa vipindi tofauti tofauti vya mwaka na kuendelea.

B. Kitenga malikia
Hiki ni kifaa kama nyavu ambacho huwekwa kati ya brood box na super box, wavu huu huweza kumzuia malikia asiweze kupanda katika super box kwa lengo la kutaga mayai.matundu ya waya huu ni madogo kulingana na umbile la nyuki watenda kazi peke yao.Hivyo malikia na madume ya nyuki hayawezi kupanda kuelekea kwenye super box.

C. Box la kuhifadhia asali
Hili ni box ambalo huwekwa juu mara tu baada ya queen excluder.Box hili huwa ni maalumu kwa nyuki watenda kazi kuweza kuhifadhi asali yao kwa wingi.Asali inayokuwa katika box hili haiwezi kuchanganyika na watoto wa nyuki wala chavua kutokana na kuwapo kwa queen excluder chini yake.Asali inayotoka katika Box hili huwa nzuri na safi kutokana na kutochanganyika na masega ambayo yalitumika kwa kuangulia watoto wa nyuki.

Uvinaji wa asali katika mzinga huu, mfugaji anapaswa kutoa frame zilizopo katika super box ambazo asali yake tayari imeiva.Mara baada ya kutoa frame hizo mfugaji anapaswa kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya kisasa iitwayo  Honey Centrifuge Machine.Mashine hii huweza kufyonza asali yote iliyopo katika sega na kubakiza sega likiwa halina asali.

Mara baada ya hapo mfugaji anapaswa kurudisha sega hilo kwenye mzinga likiwa na frame yake ili nyuki aweze kujaza asali tena.Hii inamsaidia sana nyuki kumpunguzia kazi ya kujenga sega jipya la Sali kila baada ya mvuno wa asali na hivyo kuongeza uzalishaji wa asali mara dufu.Tofauti tu ya aina ya mzinga huu ni kwamba huwezi kupata zao la nta.

2. Mzinga wa viunzi
Huu ni mzinga wa teknolojia ya kati kutoka kwenye mizinga ya kienyeji na kuelekea mizinga ya kisasa.Mzinga huu uhifadhi wake wa asali hautofautiani sana na uhifadhi wa asali katika mizinga ya kienyeji, isipokuwa katika mzinga huu masega hupangwa kwa kufuata utaratibu wa viunzi vilivyowekwa.nyuki huweka sega moja katika kila kiunzi kimoja cha mzinga huu.

Mzinga huu pia haujagawanywa kwa kutenganisha sehemu za kuhifadhia asali na sehemu ya malikia kuangulia watoto.Hivyo asali itokayo katika mzinga huu huweza kuchanyanyika na watoto iwapo mfugaji hatakuwa makini katika uvunaji wa asali hiyo.

Uvunaji wa mzinga huu, mfugaji anapaswa kukata sega lote lenye asali pekee na kulihifadhi katika chombo kisafi kwa jili ya kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya kusasa au kwa kutumia njia za kitamaduni.

No comments:

Post a Comment