Nyanya ni zao la chakula na biashara. Kilimo cha zao hili hufanyika majira yote (masika na kiangazi), na faida hupatikana haraka na ni ya kuridhisha ikilinganishwa na mazao mengine.
Pamoja na umuhimu wa zao hili, wadudu waharibifu na magonjwa huathiri uzalishaji na ubora wa matunda. Ili mkulima aweze kupata faida na kuongeza pato la kaya yake ni vema kuzingatia udhibiti wa magonjwa na wadudu wa zao hili. Kipeperushi hiki kinatoa maelezo ya udhibiti wa magonjwa na wadudu muhimu ya zao la Nyanya.
MAGONJWA YA NYANYA
Bakajani chelewa (Late blight)
Udhibiti
- Nyunyiza dawa ya kuzuia ukungu hasa wakati wa masika, Dawa
- zinazopendekezwa ni Ridomil, Dithane 45, Bravo, Funguran, milraz.
- Fanya mzunguko wa mazao. Usipande nyanya sehemu moja kila msimu au
- palipolimwa mazao jamii ya nyanya km viazi mviringo, bilinganya, aina zote
- za pilipili na nyanya chungu.
- Tumia mbegu safi
- Panda aina za nyanya zinazovumilia ugomjwa
Bakajani tangulia (Early blight)
Udhibiti
- Nyunyiza dawa ya Kocide, Funguran
- Teketeza mabaka ya mazao baada ya kuvuna
- Tumia mbegu safi na bora
Mnyauko fusari (Fusarium wilt)
Ugonjwa hujitokeza zaidi wakati wa kiangazi. Vimelea hushambulia sehemu au
mirija ya mmea ya kupitishia maji na chakula. Mmea hukosa maji na chakula na
hatimaye hunyauka. Shina la mmea likipasuliwa ndani huonekana rangi ya kikahawia.
Udhibiti
- Tumia mbegu safi na bora
- Tumia mzunguko wa mazao. Nyanya zisizungushwe na mazao jamii yake
- ke
- Choma kitalu cha nyanya kabla ya kusia mbegu
Mnyauko bacteria (Bacterial wilt)
Udhibiti
- Panda mbegu safi
- Panda nyanya sehemu ambayo haijawahi kupandwa viazi mviringo,
- bilinganya au nyanya chungu
- Tumia mzunguko wa mazao
- Hakikisha mfereji wa maji ya kumwagilia hayapiti kwenye shamba lenye
- historia ya ugonjwa huu.
- Choma kitalu cha nyanya kabla ya kusia mbegu
Mnyauko vetisili (Verticillum wilt)
kunyauka na kufa.
Udhibiti
- Tumia mzunguko wa mazao usiopungua miaka mine
- Ondoa mabaki ya nyanya shambani
- Tumia mbegu bora na safi
Bakadoa (Bacterial spot)
Udhibiti
- Panda mbegu bora na safi
- Tumia mzunguko wa mazao
- Teketeza masalia ya mazao
- Nyunyizia dawa ya funguran, Kocide101, Cobox, Bravo
Makovu bakteria (Bacterial canker)
Udhibiti
- Tumia mbegu bora na safi
- www.ariuyole.go.tz 2
- Teketeza masalia ya mazao
- Tumia mzunguko wa mazao
- Rasta (Yellow leaf curl)
Ugonjwa huu husababishwa na virusi na huenezwa na nzi wadogo weupe. Hutokea zaidi wakati wa kiangazi. Mimea hudumaa na majani yaliyoshambuliwa huwa na rangi ya manjano na pengine rangi ya zambarau. Nyanya hupasuka.
Udhibiti
- Nyunyiza dawa za sumu za kuua wadudu (Selecron, Dursburn, Actelic)
- Ng’oa mimea yenye ugonjwa
- Tumia mzunguko wa mazao
- Weka shamba katika hali ya usafi
Batobato (Tomato mosaic virus)
Udhibiti
- Tumia mbegu bora na safi
- Ng’oa mimea iliyoshambuliwa
- Teketeza masalia ya mazao
- Weka shamba katika hali ya usafi
WADUDU WAHARIBIFU
Viwavi Matunda (Fruit worm)
Udhibiti
Nyunyizia dawa ya kuua wadudu. Dawa hizo ni pamoja na Actelic 50EC, Selectron,
Dursbaan, Maji ya majani ya mwarobaini au utupa pia huua wadudu.
Utitiri wekundu (Red Spider mites)
Udhibiti
- Nyunyizia dawa za sumu. Dawa hizo ni pamoja na Actellic, Selecron,
- Dursbarn na Thionex
- Mwagilia maji mara kwa mara
- Weka shamba katika hali ya usafi
Inzi weupe (White flies)
Udhibiti
Nyunyizia dawa za sumu za kuulia wadudu kama Selecron, Actellic, Dursban na
thionex. Pia maji ya majani ya mwarobaini na utupa.
Vidukari au Wadudu mafuta (Aphids)
Udhibiti
Nyunyizia dawa za sumu za kuulia wadudu kama Rogor, Actellic, Selecron, Dursban
maji ya majani ya mwarobaini na utupa, maji ya pilipili.
Minyoo (Nematodes)
Udhibiti
- Tumia mzunguko wa mazao
- Choma udongo wa kitalu kabla ya kusia mbegu kwa kutumia karatasi la
- plastiki jeusi na nishati ya jua
- Choma masalia ya mazao
Sota (Cutworms)
Udhibiti
- Nyunyiza dawa za kuua wadudu kwenye shina usawa wa udongo
- Hakikisha miche inapata maji ya kutosha.
No comments:
Post a Comment