KILIMO BORA CHA BAMIA - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Thursday, October 18, 2018

KILIMO BORA CHA BAMIA


UTANGULIZI
Bamia ni moja ya zao la mbogamboga ambayo asili yake ni hapa hapa africa na nchini Ethiopia ambapo kwa sasa linalimwa katika nchi nyingine nyingi.
bamia ni moja kati ya mazao ambayo yanafaida sana ndani ya mwili wa binadamu
  • usaidia kusafisha utumbo mpana
  • usaidia kurainisha choo
  • uondoa uchafu mwilini
  • uongeza uroto kwa wale wenye upungufu wa uroto kwenye maungio
  • pia ina vitamin C ambayo husaidia kulainisha ngozi 
na faidia nyingine nyingi ambazo siwezi kuzitaja zote kwa wakati huu.

bamia hustawi vizuri katika maeneo 1000 mita kutoka usawa wa bahari

KUANDAA SHAMBA
Kama mazao mengine shamba la bamia linatakiwa kusafishwa vizuri na pia unaweza kuweka mbolea ya asili kama  vile mboji, samadi na mbolea ya kuku

UPANDAJI
Bamia ni moja kati ya mazao rahisi sana kuhudumia kama mtu ukiwa makini,
kabra ya kupanda mbegu ya bamia inatakiwa kulowekwa kwenye maji ya uvuguvugu kwa masaa 24 kama unakwenda kupanda maeneo ambayo hayana unyevu wa kutosha.
nafasi ya kupanda ni sentimita 40 kati ya mmea na mmea na sentimita 80 kati ya mstari na mstari.
bamia uchukua siku 8 hadi 10 kuota inategemea na eneo husika,.



MBOLEA NA KUPALILIA
Katika zao la bamia sio lazima sana kutumia mbolea ya chemicali kama haiitajiki unaweza kutumia mbolea ya asili
tumia mbolea ya kemikali kwa maeneo yasio na rutuba ya kutosha
na unatakiwa kipalilia nyasi na magugu pale unapoona yameesha anza kukua shambani.

KUVUNA
bamia kawaida inatakiwa kuvunwa pale ambapo inakua haijakomaa sana na hiyo inaweza kuchukua miezi m3 kutoka mda uliopanda inategemea na eneo husika.
na kwa eka moja unaweza kuvuna kilo 8000 inategemea na eneo na huduma zako.

MAGONJWA
Magonjwa yanayo sumbua sana bamia ni pamoja na
  • uburi unga
  • mosaic virus
  • na ukungu
hivyo tumia dawa ya kuzuia ukungu pamoja na za kuuwa wadudu pale wadudu wanapo onekana shambani.
palilia mapema pamoja na usafi shambani ili kuepusha magonjwa na wadudu. 


No comments:

Post a Comment