KILIMO BORA CHA MAHARAGE - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Tuesday, October 2, 2018

KILIMO BORA CHA MAHARAGE

MAHARAGE-BEANS (Phaseolus vulgaris)




Image result for picture of beans plant

UTANGULIZI

Maharage ni zao jamii ya mikunde ambalo hulimwa kwa ajili ya kuliwa kama mboga au futari.linaweza kama maharage mabichi au maharage makavu.Pia majani yake mni chakula cha mifugo na yanatumika pia kama mboga kwa binadamu.katika ekari moja unaweza kupata Kg 600 hadi 1200 za maharage.

Image result for image of beans
HALI YA HEWA IFAAYO

Hustawi vizuri maeneo yenye mwinuko wa mita 1000 hadi 2000 kutoka katika usawa wa bahari .Pia  yanaweza kulimwa pungufu ya mita 1000 au zaidi ya mita 2000 kutoka usawa wa bahari.Maharage huitaji mvua ya kutosha kipindi cha kabla ya uwekaji maua na kipindi cha ukuaji wa vitumba vya maharage.Huitaji unyevu kidogo kipindi cha kuweka maua na ukavu kipindi cha kukomaa na kukauka vitumba.Maharage hulimwa kwa wingi MBEYA,IRINGA,KIGOMA,ARUSHA,MOSHI,morogoro n.k

UDONGO

Hustawi vizuri katika udongo usiotuamisha maji na ambao ni mfinyanzi kichanga ambao una mboji ya kutosha wenye pH 5.5 - 7.Pia unaweza kulima katika udongo wa aina tofauti tofauti.

MBEGU BORA ZA MAHARAGE

Kuna aina mbalimbali za mbegu bora za maharage kama vile canadian wonder,Tengeru,Uyole,SUA,Ilonga na Lyamungo.

UPANDAJI

Maharage hupandwa mwishoni mwa msimu wa https://ift.tt/2eQ1r5Cmvua kuepusha kunyeshewa kipindi cha uekaji maua.Yanawezwa kupandwa mwezi Februari,machi,aprili inategemea mvua katika eneo lako zinaisha mwezi gani,hivyo hakikisha angalau yanapata mwezi mmoja wa mvua ya kutosha.Fukia mbegu zako katika kona cha sm2.5 hadi 4 katika ardhi kutegemea na aina ya udongo shambani kwako.
Maharage hupandwa kwa kutumia mbegu ambazo ni safi na hazijaharibika kwa kuvunjika au kuliwa na wadudu.Kabla ya kupanda maharage yako unaweza kuyatibu kwa kutumia Rhizobia bacteria ambapo itakupunguzia matumizi makubwa ya mbolea za nitrojeni.

NAFASI YA UPANDAJI

Maharage yapandwe kwa nafasi ya sentimeta 40-60 mstari hadi mstari na sentimeta 8 -15 shina hadi shina.
Image result for picture of beans plant in rows




Image result for picture of beans plant in rows

MBOLEA

Unaweza kupanda katika shamba lililotawanywa mbolea ya samadi.
Pia uanweza kwa uzuri zaidi kupandia mbolea za viwandani kama vile TSP au MInjingu mazao au minjingu kwa kiasi cha kg 50 -100 kwa ekari.https://ift.tt/2eQ1r5C
Wakati wa mmea  kuanza  kuweka maua  unaweza kutumia mbolea ya N.P.K au SA au Kwa Kiasi Kidogo CAN au UREA Angalizo Mbolea hizi zikizidi maharage huwa na majani mengi kuliko maua na kusababisha mavuno kuwa machache.
UPALILIAJI

Upaliliaji inabidi ufanyike mapema mara tuu maharage yanapoota na kshamba kuwa na magugu.Palizi ya kwanza inaweza kufanyika Kati ya siku 8-12 baada ya mmea kuota na yapili ifanyike siku ya 20- 30 baada ya palizi ya kwanza.ILi kuyarinda maua ya maharage yako yasipukutike wakati wa palizi hakikisha unaepuka palizi kipindi cha uwekaji maua.

WADUDU
 Funza wa maharage ni wadudu wanaoshambulia mimea michanga ya maharage. Funza wa maharage hawa huweza kusababisha uharibifu hadi kufikia asilimia 100 kufuatana na hali ya hewa-unyevu kidogo, rutuba kidogo, kuwepo kwa maotea ya aina ya maharage na magonjwa kwenye udongo, kurudia kupanda zao la maharage kila msimu na aina ya naharage.
Njia nzuri ya kudhibiti funza wa maharage  ni:-
1. Kupanda mapema
2. Kupakaza mbegu dawa kama endosufan, Acephate, Murtano (mchanganyiko wa dawa ya fungas na wadudu) nasaidia kuzuia funza wa maharage na visababishi vya kuozesha mizizi.
TAHADHALI: Dawa ya Murtano ni sumu kali hivyo mbegu zenye dawa hii zisitumike kwa chakula.
3. Kunyunyizia dawa mfano DUDUBA au DUDUALL Karate 5EC au Actellic 50EC ndani ya siku 4 hadi 5 baada ya maharage kuota.https://ift.tt/2eQ1r5C
4. Kupanda mbegu zenye afya kwenye udongo wenye rutuba.
5. Kupanda mbegu zenye ukinzani wa funza wa maharage.
6. Kuweka matandazo kama pumba ya mpunga husaidia kuotesha mizizi mipya n kurudisha afya ya mmea wa maharage
.
Pia maharage yanaweza kushambuliwa na wadudu mbalimbali kama vile nzi weupe wa maharage na wengineo ambao wanweza kuzuiwa kwa kutumia dawa mbalimbali za wadudu.

MAGONJWA

Magonjwa maarufu ni ndui ya maharage, madoa pembe, kutu, magonjwa yanayosababishwa na bacteria na virusi. Mbegu iliyoambukizwa, udongo na takataka za maharage ni vyanzo vikubwa vya uambukizaji kwa magonjwa yote isipokuwa ugonjwa wa kutu ya majani.
1. Punguza athari kwa kupanda mbegu safi, zenye afya zisizo na vidonda/ magonjwa, aina zinazovumilia na kutunza shamba.
2. Panda kwa mzunguko wa mazao ya jamii nyingine.
3. Ondoa na kuchoma yaliyougua.
4. Tumia dawa zilizopendekezwa kama Kocide, Funguran, Bayleton n.k kwa kuzuia magonjwa yanayosababishwa na ukungu na bacteria.

UVUNAJI
Image result for picture of beans harvesting

Maharage huvunwa mara tuu yanaponza kukauka na kabla vitumba havijapasuka.Ng'oa mashina ya maharage na na upigepige kuyaondoa katika vitumba vyake.

KUHIFADHI

Baada ya kuyapiga na kupeta kuondoa uchafu yaanike juani kwa siku kazaa kuhakikisha yamekauka na hayana unyevu unaoweza kusababisha yapate fangasi.yahifadhi katika magunia,kama yatakaa muda mrefu bila kuliwa basi hakikisha unayahifadhi kwa kutumia dawa za kuulia wadudu kama vile Shumba, Kama vile ACTELLIC DUST au MALATHION. au Tumia mifuko maalum ya kuhifadhia nafaka.

No comments:

Post a Comment