KILIMO BORA CHA TANGAWIZI - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Saturday, October 6, 2018

KILIMO BORA CHA TANGAWIZI

Tangawizi ni moja kati ya aina za mazao ya viungo ambayo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome). Zao hili kwa lugha ya kigeni linafahamika kama Zingiber officinale.
UDONGO NA KUSTAWI
Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1,500 au zaidi. Huhitaji mvua kiasi cha milimita 1,200-1,800 na joto la wastani wa nyuzi
joto 20°C-25°C. Hustawi vema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usio-tuamisha maji.
AINA
Mpaka hivi sasa hakuna aina rasmi za tangawizi ambazo zimeainishwa na kuthibitishwa kuzalishwa nchini Tanzania. Pamoja na hili, kuna aina tatu za tangawizi ambazo zimezoeleka kuzalishwa na wakulima hapa nchini. Aina hizo ni Tangawizi nyeupe maarufu kama White Africa au Jamaica, Cochin
(flint), na Bombay.
Tangawizi inayopandwa katika sehemu tambarare huwa laini zaidi
kuliko inayozalishwa kwenye maeneo ya milima, ambayo huwa ngumu na kuwa na nyuzi nyingi zaidi.
NAFASI
Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya sentimita 23-30 kwa 15-23 na kina cha sentimita 5-10. Unaweza kupanda sehemu yenye
miti au migomba ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji mara
kwa mara endapo mvua inakosekana hadi kufikia mwezi mmoja kabla ya kuvuna.
MATUMIZI
Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na kuchangamsha katika vinywaji kama vile chai, soda, juisi, vilevi na kadha-lika. Kuna aina mbalimbali za vyakula ambavyo pia hutengenezwa kwa kutumia tangawizi kama vile mikate,
biskuti, keki, nyama za kusaga, achari
na kadhalika.
Tangawizi pia hutumika katika viwanda vinavyotengeneza madawa ya tiba mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi. Hali kadhalika tangawizi
hutumika katika kutengeneza vipodozi vya aina mbalimbali vile
kama poda
MBEGU NA NAMNA YA KUPANDA
Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande vya tunguu. Vipande vya tangawizi huhifadhiwa mahali pakavu penye ubaridi ili kuweza kuchipua.
Machipukizi hukatwa urefu wa sen-timita 2.5-5. Baada ya hapo, unaweza kupanda machipukizi hayo kwenye matuta au shambani kawaida endapo eneo lako ni tambarare.
Baada ya kupanda, tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale kivuli kinapokosekana.
MATAYARISHO
Ondoa takataka zisizohitajika shambani. Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 25-30 kwa hekari moja.
PALIZI
Katika kipindi cha wiki mbili, magugu huanza kuchomoza kwa kuwa udongo huwa na unyevu kwa wingi. Fanya palizi mara majani yanapojitokeza.
Endelea kung’oa magugu na kuweka shamba katika hali ya usafi hadi wakatiwa kuvuna.
KUPANDA
Tangawizi ni mmea unaotambaa chini ya ardhi, wakati wa masika hutoa majani juu ya ardhi. Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia na tunguu fupi wakati Cochin ina tunguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo kati ya kijivu na nyekundu. Mmea una urefu wa futimbili na majani yake ni membamba marefu, ambayo hufa kila mwaka
yakiacha tunguu ardhini likiwa hai. Maua ya mmea huu yana rangi nyeupe au manjano.
MAGONJWA NA WADUDU
Madoa ya majani: Yanayosababishwa na viini vya magonjwa viit-
wavyo Colletotrichum zingiberis na Phyllosticta zingiberi.
Kuoza kwa tunguu: Kunasababishwa na viini viitwavyo Pithium spp.
Mizizi fundo: Inasababishwa na Meloidegyne spp.
UVUNAJI
Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda, wakati majani yake yanapo-geuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa.
Tangawizi itakayohifad-hiwa ivunwe mapema kabla haijako-maa kabisa, na ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi
hivyo hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana kulinganana na huduma ya zao, yanaweza kuwa kiasi
cha tani 20-30 cha tangawizi mbichi huweza kupatikana kwa hekari moja.
SOKO LA TANGAWIZI
Soko la tangawizi lipo ndani na nje ya nchi, kiasi kikubwa kinauzwa nchini. Bei yake ni kati sh. 300-1,500/- kwa kilo moja kutegemeana na msimu.

No comments:

Post a Comment