Ufugaji wa Kuku wa Mayai - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Saturday, October 20, 2018

Ufugaji wa Kuku wa Mayai

Misingi na taratibu za ufugaji bora
Tanzania ni moja ya nchi za Afrika zinazokabiliwa na tatizo la ajira hasa kwa vijana wengi wanao maliza elimu ya juu kuanzia ngazi ya astashahada hadi shahada. Mfumo wa elimu yetu unatuhitaji baada ya kuhitimu, kijana yampasa kuanza kutembea na bahasha zenye vyeti katika ofisi mbalimbali ili kuomba nafasi za kazi. Hii pia inachangia sana kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira duniani.
Kwa sasa takwimu zinaonesha kiwango cha ukosefu wa ajira kwa Tanzania ni asilimia xxxx (xx%). Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za namna ya kupambana na tatizo la ajira Tanzanizia lakini binafsi bado naamini tatizo la ajira litaondolewa na vijana wenyewe lakini hii haimanishi serikali haina mchango wowote katika kutatua tatizo la jaira.
Vijana wengi baada ya kuhitimu hawafikirii kutengeneza ajira badala yake wanatumia mda mwingi kutafuta kazi za kuajiriwa ofisini kitu ambacho kiuchumi kina athari kubwa. Baadhi ya vijana wamekuwa wakilalamikia sana kuhusu tatizo la mitaji, ndio katika ufugaji mtaji ni mhimu sana katika kufanikisha mradi wa ufugaji lakini mimi binafsi naamini katika wazo yaani business plan yako maana hata wakati mwingine unaweza ambiwa ukipewa hata millioni mia (100) utakuta huna wazo lolote la kuwekeza hiyo millioni mia (100) ndo maana nasema mtaji sio tatizo kihiivyo bali wazo ndo kitu mhimu na cha msingi.
Mwanzoni mwa mwaka 2016 niliamua kuanza ufugaji wa kuku wa mayai amabapo nilinunua vifaranga wapatao 1100 kutoka Malawi kwa aaajiri ya kuanza ufugaji rasmi. Baada ya kuku wangu kuanza kutaga na kuona faida inayopatikana na kupata ujuzi mbalimbali juu ya namna bora ya ufugaji wa kuku wa mayai, nilipata msukumo mkubwa sana wa kuandika kitabu hiki ambacho kitasaidia msomaji au mfugaji namna bora ya kufuga kuku wa mayai.
Kitabu hiki kinaeleza kwa undani kadri nilivyoandika jinsi ya namna ya ufugaji bora wa kuku wa mayai. Kitabu hiki kinajumuisha maeneo makuu nane (08) katika ufugaji wa kuku kuanzia siku ya kwanza ya kupokea vifaranga hadi uuzwaji wa mayai ambayo ni: utangulizi, uandaaji wa banda la kuku, Maandalizi bora ya upokeaji wa vifaranga wenye umri wa siku moja, Mahitaji ya maji na chakula cha kuku, chanjo ya vifaranga na kuku, utunzaji wa mahesabu na kukumbukumbu za mradi wa ufugaji wa kuku wa mayai, utunzaji wa ubora wa mayai na masoko ya mayai na bidhaa mbalimbali zitokanazo na kuku.
UANDAAJI WA BANDA LA KUKU
Kwa kawaida na njia rahisi ufugaji wa kuku wa mayai hufanyika kwenye banda yaani nyumba ya kuku. Banda hasa katika ufugaji mdogo wa kuku limekuwa likitumika sana kwa mazingira yetu ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Banda la kuku wa mayai linawezwa kujengwa kwa kutumia mbao, miti, tofali za kuchoma, mbichi au za saruji, au kwa kutumia mabati. Lakini kwa uzoefu wangu ni bora banda lako lijengwe kwa kutumia tofali za kuchoma au za saruji ili liwe na uimara zaidi.
Banda lenye ubora ni lile ambalo linawapa usalama kuku wako wa mayai. Banda lako hakikisha lina uimara zaidi ambao utazuia wezi kuingia ndani kiurahisi, kuzuia nyoka kuingia ndani, ndege na wanyama wakali ambao wanaweza kuathiri kuku wako. 
Kwa wastani ukubwa wa mita moja ya mraba ya banda inabeba kuku watatu (03) kwa mujibu wa FAO lakini kwa uzoefu wangu mita moja ya mraba inaweza kubeba hadi kuku watano (05), kwa hiyo unashauriwa kupima ukubwa wa banda lako kulingana na idadi ya kuku wa mayai unaotegemea kufuga ndani ya banda lako. Mara nyingi kwa uzoefu wangu ni bora banda lako moja liwe na uwezo wa kubeba kuku mia tatu (300) maana hii itarahisisha utoaji wa huduma ndani ya banda kwa maana ya utoaji wa maji, chakula na huduma zingine kwa ufanisi zaidi. 
Unapochagua sehemu nzuri ya ujenzi wa banda lako hakikisha iwe rahisi kwako kupata maji kwa ajiri ya kuku wako, chanzo cha joto na mwanga (mkaa, taa ya chemri au umeme vitahitajika katika ufugaji wako), huduma za veterinary, barabara nzuri zinazoweza kupitika kwa mwaka mzima hata kipindi cha mvua, chakula cha kuku na soko la kuuza mayai na bidhaa mbalimbali zitokanazo na ufugaji wa kuku kama vile kuku waliopunguza kiwango cha utagaji na mbolea itokanayo na kuku.
Hakikisha pia banda lako haliingizi maji ndani maana unyevunyevu ndani ya banda la kuku ni mwiko kwa sababu bacteria wengi husababishwa na unyevunyevu. Pia hakikisha banda lako haliingizi mwanga wa jua moja kwa moja ndani ya banda lako la kuku maana mwanga wa jua wa moja kwa moja huathiri ukuaji wa kuku wa mayai na hata utagaji pia.
Baada ya kukamilisha banda lako hakikisha umelisakafia au umeweka zege ili kutoruhusu bacteria ndani ya banda. Pia hakikisha banda lako umeliwekea maranda ya mbao au maganda ya mchele. Binafsi napendelea sana kutumia maganda ya mchele na nashauri kama unaweza kuyapata kiurahisi unaweza kuyatumia nawe pia. Hakikisha unayaondoa baada ya kulainika na kuwa mbolea, mbolea hii waweza uza au itumia shambani kwako hasa katika kulimia mboga mboga ambazo pia hutumika kwa kuku wako ili viini vya mayai wa kuku wako view vya kijani maana mayai ya aina hiyo hupenwa sana na wateja.
Madrisha ya banda lako yanapaswa kuwa makubwa ili hewa na mwanga (usiokuwa na joto la jua) vipite kwa urahisi na kurahisisha mzunguko mzuri wa hewa ndani ya banda. Banda lako liwe na madirisha pande zote mbili yaani mbele na nyuma ili iwe rahisi kuruhusu hewa kutoka na kuingia ndani ya banda. Madirisha yako yanaweza tengenezwa kwa mbao na kuwekewa nondo ambazo si rahisi mtu kuingiza kicha ila kuzia wezi kuingia ndani ya banda kiurahisi. Madirisha yako unaweza kuyawekea nyavu na pazia ambazo zitashushwa kipindi cha usiku.
Eneo la nje kuzunguka banda lako la kufugia kuku kuwe na usafi wa kudumu. Hali ya usafi nje ya banda itafanya wadudu kama siafu au mchwa na wanyama kama panya na paka mwitu wakose maficho. Nje ya banda ndani ya uzio kuwe na miti midogo na mimea mingine midogo kwa ajili ya kivuli.
Banda lako liwe rahisi kusafisha. Kuta na sakafu visiribwe zisiwe na nyufa ili kurahisisha kusafisha. Pia itadhibiti kusiwe na wadudu wa kujificha katika nyufa kama papasi, viroboto n.k. Banda lako liwe kavu mda wote na lisiwe na harufu mbaya na wadudu kama inzi.

No comments:

Post a Comment