UFUGAJI WA KUKU: UJUE UGONJWA WA MAFUA YA KUKU ( infectious coryza) NA TIBA YAKE - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Wednesday, April 26, 2017

UFUGAJI WA KUKU: UJUE UGONJWA WA MAFUA YA KUKU ( infectious coryza) NA TIBA YAKE



HABARI MFUGAJI KARIBU HAPA TENA.

Leo tunazungumzia ugonjwa wa Mafua ya kuku( infectious coryza)

    MAELEZO

Ni ugonjwa unaoitwa infectious coryza huenezwa na bacteria. anaeitwa (hemophilus paragallinarum).
Ugonjwa huu hushambulia  kuku aina zote. Na usipo kuwa makini kwenye usafi wa banda na vyombo , kuruhusu watu kuingia ovyo bandani au kuku wa jirani kuja kuingia kwenye banda lako; ugonjwa huu unaweza shambulia kuku wako kwa kila wiki.

*DALILI ZA UGONJWA HUU*  =

_Kuvimba uso chini na nyuma ya macho.
_Kupumua kwa shida na kukoroma
_Kutoka makamasi puani,
_ Mdomoni kuwa na hali ya mterezo
_Macho kuvimba
_Kushindwa kula.
_Kupiga chafya , macho kuonekana kama yanatoka machozi

*JINSI UGONJWA UNAVYOENEA:*

_Ugonjwa huu huenea kutokana kuku mmoja kwenda kwa kuku mwingine, au kutoka banda moja kwenda banda lingine.

_Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilicho chafuliwa na kinyesi cha kuku Mgonjwa.
_Ugonjwa huu uneea na kuambukizwa kwa mfumo wa hewa  pale kuku wanapopiga chafya.

*UNASHAURIWA*

Pindi ugonjwa unapo ingia bandani kwako wale kuku watakao onesha dalili za ugonjwa huu , watenge kisha wape tiba kuku wako wote; unatakiwa kuwatenga kwa ajili ya kupunguza maambukizi bandani.

*DALILI ZA MZOGA UKIUPASUA*
Usaha mweupe hadi njano huonekana kwenye macho na ndani ya pua

*MATIBABU*

Zipo dawa nyingi za kutibu ugonjwa huu  antibiotic/ sulfa. Hizi ni baadhi tu.

Fluban
Ganadexil
Tylodox
Teramycin.nk

Ushauri:Tumia fluban kwa Kuku wanaooneshadalili za mafua  bila  vifo.

Tumia  Ganadexil/tylodox kwa Kuku wenye mafua  ambao tayali kuna vifo vimetokea.
__________________________

2 comments:

  1. Ugonjwa unachukua muda gani kupona tangu ukianza kutumia dawa?
    Maana unatumia dawa lakini kuku bado Wana koroma mafua..

    ReplyDelete