UFUGAJI WA KUKU: UTAMBUE MFUMO WA UFUGAJI KUKU WA NUSU HURIA - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Wednesday, April 26, 2017

UFUGAJI WA KUKU: UTAMBUE MFUMO WA UFUGAJI KUKU WA NUSU HURIA



Karibu tena ndugu mfugaji ujifunze kitu kidogo hapa ili uongeze mradi wako
Wafugaji wengi wamejikita katika ufugaji kuku wa kienyeji, kuku wa kienyeji ni kuku wazuri na wenye soko zuri. Pia wanasifika
katika kuhimili magonjwa; kuku wakienyeji wakiugua wakipatiwa tiba Basi kurudi katika hali yao ya kawaida ni haraka kuliko Kuku wengine, katika ufugaji kuku kuna mifumo ya ufugaji mi 3
1. Huria 2 . Nusu huria 3. Ndani Katika kila mfumo hapo kuna faida na hasara zake , kwa mfugaji wa Kuku kienyeji mifumo mizuri kuitumia ni huria na nusu huria. Tambua kuwa kuku wa kienyeji ni kuku wenye pilika pilika hivyo ukiwafuga kwa kuwafungia ndani utakuwa kama umewanyima uhuru.
Katika kuutumia mfumo huu kuku huwekwa kwenye mabanda yenye hewa ya kutosha na mabanda hayo huwekewa uzio . Uzio unaweza kujenga kwa kutumia matofali , wavu miti hata kwa kutumia nyasi au makuti.
Na uwezekano wa kuku kudonoana, kula mayai huwa ni Mkubwa. Hapa tutajifunza mfumo wa nusu huria, faida zake na jinsi ya kuuboresha ili kuku wako wawe na maendeleo mazuri. Mfumo huu ni mzuri kwa kuku aina zote( isipo kuwa broiler) ila hapa tunaongelea kwa kuku wa kienyeji.
Kuuboresha mfumo huu ndani ya huo uzio unaweza panda majani ambayo kuku hupenda kula. Katika mfumo wa huria kuku huwa huru Zaidi huko nje wanako chunga hukutana na majani ya kila aina . Hivyo kuku wako unapo wafuga kwa nusu huria hakikisha ndani ya uzio wa banda lako kuna kuwa na bustani ya mboga mboga mchicha nk. Pia unaweza panda miti ambayo ni dawa za asili kwa kuku.
1. Mpapai 2. Mlonge longe 3. Aloe vera 4. Mwarobaini. 5Lusina. Nk Katika mfumo huu ni lazima uwe na sehemu ya kulelea Vifaranga kwa kuwa Vifaranga vinapototorewa huhitaji joto na uangalizi mzuri basi ni lazima kuwepo na Chumba cha Vifaranga. Kuku wako watakapo angua Vifaranga utavilea katika hiko Chumba kwa muda mpaka utakapo ona kuwa wanaweza kwenda kujichanganya na kuku wakubwa katika hiyo sehemu yenye uzio.
Faida za mfumo huu ni kama ifuatavyo.
_Tabia mbaya ya kuku kama kudonoana Si nyingi
_Mfumo huu hutumika kwa kuku wenye umri wowote
_Utunzaji wa kuku ni rahisi kulinganisha na ule wa huria.
_Kuku huwa salama na maadui
_ Mfugaji huwapa kuku chakukula ziada na kupata matokeo mazuri
_Ni rahisi kujua idadi yake na kuwa tenganisha kwa makundi
_Kuku hupata mwanga wa jua wakotosha na wakati jua kali hukaa bandani.
_Ni rahisi kudhibiti kuku na wadudu vimelea vya magojwa _Ni rahisi kutambua kuku wagonjwa
_Ni njia bora kuliko zote kufugia kuku wa asili
_Upotevu wa mayai na kuku upungua _Ni rahisi kukusanya mbolea _ Ni rahis kutunza kumbukumbu
Hasara za mfumo huu ni kama ifuatavyo
_ Hutumika zaidi maeneo yenye makazi mengi ya watu
_Unahitaji gharama za uzio
_ Mfumo huu sio mzuri kwa kuku wa nyama( broiler)
_Matumizi ya muda mrefu katika eneo husika laweza kuwa na minyoo au vimelea vingine vyovyote vya ugonjwa.
Utumiaji mzuri wa mfumo huu ni kama ifuatavyo
1. Fanya usafi eneo husika na banda/ jipangie utaratibu wakusafisha eneo lote na banda kwa kutumia dawa za kuuwa wadudu( bacteria)
2. Usiruhusu kila Mtu aingie ndani ya uzio wa banda lako ikiwezekana weka utaratibu kabla ya kuingia ndani ya uzio mlangoni kuwepo na dawa ili wanapoingai waweze kukanyaga na viatu vyao ndipo waingie (Disinfectant)
FUGA KIBIASHARA INAWATAKIA UFUGAJI MWEMA WENYE MAFANIKIO.

No comments:

Post a Comment