UGONJWA SUGU WA MFUMO WA HEWA.
(Chronic Respiratory Disease-CRD)
Maelezo
Ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria ambao hushambulia zaidi kuku na bata mzinga.
Jinsi Ugonjwa Unavyoenea
• Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi cha kuku wagonjwa na wenye
vimelea. Pia kupitia mfumo wa hewa kutoka ndege wagonjwa.
• Njia kuu ya kuenea kwa maambukizi ni kupitia mayai, hivyo maambukizi huendelea kutoka kizazi hadi
kizazi.
• Tahadhari: Wageni, wafanyakazi na magari yanaweza kusambaza ugonjwa kutoka shamba hadi shamba
au banda hadi banda
Dalili
Ugonjwa huu hushambulia zaidi mfumo wa hewa na hivyo kusababisha dalili zifuatazo:
• Kuku hukoroma
• Kuku hutoa makamasi
• Kuku wanakohoa kwa muda mrefu, wiki hadi miezi
• Kuvimba macho
• Kutingisha kichwa
• Vifo vya kuku vinaweza kufikia hadi asilimia 20
Uchunguzi wa Mzoga
• Athari kubwa za ugonjwa huu ni kwenye mfumo wa hewa, hivyo mabadiliko yanakuwa katika mfumo
mzima wa hewa.
• Kamasi nzito zenye usaha zilizotapakaa kwenye pua, koromeo, mapafu na vifuko vya hewa
Tiba
• Madawa aina ya sulfa na antibiotiki yanaweza kutumika kwa ajili ya tiba na kinga.
_Tylosin
_Lincomycin
Nk
Pata ushauri wa Doct
KILIMO NA UFUGAJIINAWATAKIA UFUGAJI MWEMA.
Usisahau Ku download app ya blog hii play store.
AU BOFYA HAPA CHINI UPAKUE APP YETU
No comments:
Post a Comment