BADILI MAISHA YAKO KWA KUWEKEZA KWENE KILIMO CHA VITUNGUU SAUMU - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Saturday, June 3, 2017

BADILI MAISHA YAKO KWA KUWEKEZA KWENE KILIMO CHA VITUNGUU SAUMU

                      

Kitunguu saumu ni moja kati ya zao bora lenye manufaa mengi kwa matumizi ya kila siku kwa maisha ya mwanadamu, kiafya, Kitabibu na kwa ajili ya kutengeneza au kuchanganyia katika dawa tofauti. Pia ni kiungo mahusui katika mambo ya mapishi.
Zipo aina tisa za vitunguu swaumu ambazo hulimwa hapa

duniani katika maeneo mbalimbali.
Aina za vitunguu saumu maalufu kwa matumizi ya kawaida ni tatu,
1. SOFT NECK - ni nyeupe huzaa kwa muda mfupi.
2. SILVER SKIN - vina rangi ya silver vikikaushwa vinaweza kukaa hadi mwaka mmoja.
3. ANTICHOKE - vina rangi nyekundu kwa mbali.
katika nchi yetu ya tanzania vinapatikana vitunguu swaumu ya aina tatu
1. Kitunguu saumu chenye mafuta makali.
2. Kitunguu saumu chenye madini ya protini
3. kitunguu saumu chenye madini, protini na mafuta mepesi.

Hiki ndicho tulacho kila siku hapa kwetu na wengi hutumia kama dawa wakati hakina sifa za kuwa dawa.
NAMNA YA KULIMA

Kitunguu hiki hulimwa katika maeneo yenye baridi uwanda wa jua hafifu, mvua za wastani na joto hafifu, aridhi iwe nyeusi yenye rutuba na mfinyanzi, kusiwe na upepo mkali au ukungu mwingi.
Hulimwa kwa kuandaa kitaluna kupandikizwa baada ya miche kufikia urefu wa inchi 6-14, hupandwa kwa mstari na mche hadi mche ni nchi 3-4 na mstari kwa mstari ni nchi 12.
Kwa kifupi kitunguu swaumu ni kati ya zao gumu sana kulilima kwani hustawi katika maeneo machache sana hapa duniani. Kwa hapa tanzania hustawi katika mkoa wa manyara wilaya ya Mbulu, Hanang na babati kidogo, pia kidogo mkoa wa kilimanjaro na kwa eneo lolote ambalo hali inaendana na maeneo tajwa hapo juu.

kwa morogoro vinalimwa maeneo ya mgeta.
UANDAAJI WA SHAMBA
Tifua udongo kidogo kisha ufanye hallowing ili kurahisisha upandaji na ukaaji wa mimea tu. Tengeneza tuta za mita 1 hadi 1.5, upana mita 10 urefu. Kwa upande wa mbolea Inashauliwa utumie WINNER
UPANDIKIZAJI

Vibanguliwe vipandwe kwa kuelekezea mizizi chini na kina cha wastani 2.5 inchi, mbolea ya samadi hushauriwa zaidi kutumika, Huvunwa baada ya miezi 4 -6 kulingana na hali ya hewa na aina ya mbegu iliyotumika.
SPACING/ MUACHANO WA MBEGU NA MBEGU
Mstari hadi mstari ni inchi 8 na mmea hadi mmea ni inchi 6 yaani (8x6t)inchi
KIWANGO CHA MBEGU

Kiwango cha mbegu ni kilo 200 - 300 kwa heka moja
MAVUNO

Ni tani 5 -6 kwa heka moja
UANDAAJI WA MBEGU

Kitunguu swaumu hupandwa "BULB" na sio mbegu kama vitunguu maji. Ni ile Punje ambayo Imekuwa na kukomaa vizuri na isyoathiliwa na magonjwa
MAGONJWA

1. Vitunguu saumu havishambuliwi na magonjwa kama ilivyo mazao mengine.
2. Mimea ikianza kutoa maua, yaache yawe marefu hadi yajikunje kisha utayakata ili kuongeza uzalishaji.
Wadudu wasumbufu ni THRIPS na ukungu upande wa magojwa.
Kwa upande wa ukungu anza na RIDOMILL GOLD upulizie mara nne kisha malizia na score kwa ajili ya Thrips tumia ACTARA au MATCH.
Hushambuliwa na magonjwa kuanzia wiki ya Tatu hadi ya saba, Tumia madwa ya kupuliza yatumikayo kwa nyanya na vitunguu vya kawaida.
SOKO

Kwa kariakoo kilo moja ni kati ya TSH 4000 hadi 6000. Ila kwa ujumla ni bidhaa ambayo inahitajika kwa wingi ndani na nje ya nchi.
Tunakutakia kila la kheri katika safari yako ya kilimo bora.


USISAHAU KUDOWNLOAD APPLICATION YA KILIMO BORA IPO PLAY STORE

DOWNLOAD HAPA SASA

                     

No comments:

Post a Comment