Dawa za Asili za Mimea (Kuzuia Wadudu Waharibifu wa Mazao) - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Sunday, June 18, 2017

Dawa za Asili za Mimea (Kuzuia Wadudu Waharibifu wa Mazao)

Unaweza kutumia mimea fulani kupunguza idadi ya wadudu waharibifu shambani mwako. Panda mimea ambayo huepukwa na wadudu waharibifu karibu na mimea inayohitaji kulindwa. Kwa mfano, minyoo fulani ambayo hula na kudhoofisha mizizi ya mimea mingi haiwezi kukaribia mimea ya matageta. Na vipepeo fulani ambao huharibu kabichi hawakaribii kabichi zilizopandwa karibu na mimea ya rosemary, sage, au thyme.Hata hivyo, tahadhari hii yafaa: Mimea fulani huwavutia wadudu waharibifu.
JINATIBAUTUMIAJI
MnyaaKuua MchwaMatone 10 ya mnyaa + maji lita moja. Koroga. Nyunyuzia/ Pulizia kwenye mchwa
UtupaWadudu wanaoshambulia mbogaTwanga kiganja kimoja cha majani. Loweka kwenye lita 1 ya maji kwa masaa 24. Chuja. Ongeza 1/8 ya kipande cha mche wa sabuni. Pulizia kwenye mboga
Muarobaini – MajaniWadudu wa mbogaPonda ganja mkona 1 wa majani. Changanya kwenye lita 1 ya maji. Loweka kwa siku mbili , halafu ongeza sabuni 1/8 ya kipande mche. Nyunyuzia kwenye mboga.
Muarobaini - MbeguWadudu wanaoshambulia mbogaTwanga mbegu kilo 5 (kisado kimajo). Loweka kwenye maji lita 15 kwa masaa 24. Chuja na pulizia/ nyunyuzia kwenye mboga
PapaiKuua mchwa Ponda majani laini ya mpapai.Ongeza lita 1 ya maji. Chuja na pulizia/ nyunyuzia kwenye mchwa
Bangi MwituKuhifadhi vyakula vya nafaka (food grains)Sambaza halafu weka gunia juu yake. Endelea hivyo hivyo.
Mkojo wa n’gombeKuua mchwa/ wadudu wa mbogaUache mkojo kwa siku 10 –14. Kwa kila lita 1 ya mkojo ongeza lita 2 za maji na 1/8 sabuni ya mche. Nyunyuzia kwenye mchwa au mboga
Mnanaa (mbarika mwitu)Kuua wadudu wanaoshambulia mbogaGram 100 mbegu + lita 1 maji + 1/8 sabuni mche. Pulizia/ nyunyizia kwenye mboga
Kitunguu saumuKuua wadudu wanaoshambulia mbogaGram 100 (3-4) twanga. Ongezea lita 1 ya maji. Acha kwa saa 24. Chuja na ongeza 1/8 ya kipande cha mche wa sabuni. Pulizia/ Nyunyuzia kwenye wadudu
Pilipili KaliKuua wadudu kwenye mbogaChanganya vijiko 3 vya chakula na lita 1 ya maji. Acha kwa saa 12. Ongezea 1/8 ya kipande cha sabuni mche. Nyunyizia kwenye mimea
Mashona nguoKuua waduduChemsha mbegu kikombe 1 na lita 1 ya maji kwa dakika 10 au loweka siku moja na ongezea 1/8 ya kipande cha sabuni mche. Nyunyuzia kwenye mboga
Muarobaini Kideri(New Castle disease)Twanga majani 1kg, ongeza maji lita 1. Wanyweshe kuku asubui. Fanya hivi kila mwezi
MajivuKuua wadudu mafuta (aphids)Nyunyizia majivu kwenye wadudu wanaoshambulia mboga
MajivuKuhifadhi mazaoChanganya majivu + pilipili kichaa + Cyprus. Sambaza kwenye gunia halafu weka gunia juu yake. Endelea hivyo hivyo.
MarejeaMboleaPanda shambani na baadaye limia chini ardhini

Je wajua Vyura, Ndege, na Wadudu Huboresha Shamba


Lakini unaweza kuwamalizaje wadudu waharibifu shambani mwako bila kutumia dawa? Usisahau kwamba zaidi ya kuwaua wadudu waharibifu, dawa hizo huua viumbe muhimu kama vile minyoo na kuvu. Pia, kumbuka kwamba vyura ni muhimu sana katika kilimo. Chura anaweza kula wadudu waharibifu 10,000 kwa muda wa miezi mitatu naye hachagui anachokula. Yeye hula viumbe wanaoharibu mimea kama vile nyenje, wadudu na viwavi wa aina fulani, na konokono.
Ndege pia hula viumbe waharibifu. Kitabu Gardening Without Poisons chasema kwamba ndege aina ya wren alionekana akiwalisha “makinda wake buibui na viwavi 500 alasiri moja katika majira ya kiangazi.” Ukitaka ndege kadhaa aina ya wren au ndege wengine wanaokula wadudu waje shambani mwako basi weka chakula cha ndege na vifaa vya kujenga kiota mahala wanapoweza kuviona. Muda si muda, utaona wakija! Na vipi wadudu? Wadudu wengi wanaoboresha shamba hula wadudu waharibifu. Ukinunua wadudu aina ya ladybug kisha uwaweke shambani mwako, watawamaliza mara moja wadudu aina ya aphid kwani wanapenda kula wadudu hao sana. Mayai ya kivunja-jungu yanaweza pia kununuliwa na kuwekwa shambani. Mayai hayo yakianguliwa, vivunja-jungu watakula wadudu wote walio karibu nao.

USISAHAU KUDOWNLOAD APPLICATION YA KILIMO BORA IPO PLAY STORE

                                      DOWNLOAD HAPA SASA

                     

No comments:

Post a Comment