Fahamu jinsi ya kufuga kuku aina ya kuroiler wenye faida kubwa - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Friday, June 2, 2017

Fahamu jinsi ya kufuga kuku aina ya kuroiler wenye faida kubwa




Tazama video hiyo hapo juu👆👆


KUROILER

Kwanini #Kuroiler ndio kuku mwenye faida kuliko kuku mwingine yoyote .

Kuroiler ni mchanganyiko wa kuku wa aina mbili. Ni mchanganyiko wa Jogoo wa broiler ( Kutoka Sasso). Hawa Sasso wanakuwa na umbo kubwa na kuongeza uzito (nyama).
Akapandishwa Jike wa Rhodes Island Red huyu anasifa kubwa Kwenye utagaji wa Mayai.
Kwahio Kuroiler ni Kuku mwenye  sifa za kuwa na uzito mkubwa ( kutoka kwa Baba) na Mayai mengi ( kutoka kwa mama).

Hivyo Basi kama wewe ni Mfugaji na unataka kupata kipato kupitia Kuku fuga #Kuroiler. 
Kwasababu:
1. Anakua kwa Haraka zaidi.  (Karithi kwa Jogoo)
2. Anataga Mayai mengi zaidi ( karithi kwa mama)
3. Ana kuwa na uzito mkubwa zaidi ya kuku mwingine. Jogoo anaweza kufikisha kilo 5 katika miezi mitano wakati kuku wengine wa kienyeji wanafika kilo 3 Baada ya Mwaka mmoja.
4. Mayai ya Kuroiler na nyama yake ni Bora zaidi. Mayai yana kiini cha njano na radha nzuri sana.
5. Gharama za kuwatunza ni za kawaida kabisa: unaweza ukamuachia akajitafutia Chakula mwenyewe.


USISAHAU KUDOWNLOAD APPLICATION YA KILIMO BORA IPO PLAY STORE

DOWNLOAD HAPA SASA

                     

Tembelea blog hii kila siku

2 comments:

  1. Kwa mfano nitafuga kuku 10,000 kuku nitawauza wapi na nani atanunua mayai nayo?

    ReplyDelete
  2. Na mayai ya huyo kroiler yanafanana na ya kienyeji au ni tofauti.

    ReplyDelete