Kuna hii biashara ya mahindi ya kuchoma (maarufu kama gobo). Unaweza kulima kwa kutumia mtaji kidogo na kupata sarafu za kutosha. Angalia mchanganuo ufuatao: kukodi shamba ekari moja wastani wa tsh 50,000/=, kulima 30,000/=, kupalilia 30,000/=, mbolea mifuko mi-3, tsh 150,000/=, madawa wastani tsh 50,000/=; Jumla kuu ni tsh. 310,000/=. Gharama hii hauitoi mara moja bali ni kidogo kidogo kutegemea
hatua husika. Mahindi huchukua wastani wa siku 90 (miezi mitatu) tangu kupanda hadi kugoboa (yaani kuvuna haya mahindi mabichi).
Unaweza kupanda kwa kutumia mvua au kutumia umwagiliaji mahali popote Tanzania. Kwa ekari moja ukilima kwa kuzingatia utaalamu una uhakika wa kuvuna kuanzia mahindi 9,800. Hindi moja huuzwa kwa tsh. 150/= hadi 250/=, kutegemea hali ya soko kwa bei ya jumla. Ukikokotoa utaona kuwa kwa ekari moja unaweza kupata tsh. 1,470,000/= kwa kadirio la chini na tsh. 2,450,000/= kwa kadirio la juu.
Ukitoa gharama za uendeshaji (za moja kwa moja) unaweza kukunja faida ya hadi tsh 2,140,000/= kwa kadirio la juu. Ukilima eka 5, una uhakika wa faida ya tsh milioni 10.7. Je, ukilima misimu kadhaa, bado utashindwa kujenga nyumba ya maana au kuwa na maisha yenye unafuu? Bila shaka utaweza! Unachohitaji wewe ni mambo yafuatayo: utayari, uthubutu, kuwa-up-to-date kwa taarifa za misimu na masoko na uwe ni mtu wa kufuatilia fursa na kujifunza. Fursa zipo 'bwerere', kama una 'allergy' na kilimo tafuta na ujifunze fursa nyinginezo; LAKINI; mtu YEYOTE anaposema fedha ni ngumu, kiukweli anakuwa hayupo "serious" kabisa na haya maisha!
No comments:
Post a Comment