MAGONJWA YA NYANYA DALILI NA UTHIBITI WAKE. - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Friday, June 16, 2017

MAGONJWA YA NYANYA DALILI NA UTHIBITI WAKE.

1.Dalili za madoa yatokanayo na bakteria hutokea kwenye majani, matawi na kwenye
matunda ya nyanya.
DALILI
Dalili bayana zaidi huonekana kwenye majani, ndio maana ya hilo jina ‘Madoa ya majani kutokana
na bakteria’. Makovu madogo ya rangi ya manjano-kijani hujitokeza kwenye majani machanga na
matokeo yake ni majani yaliyopindapinda, yaliyokoza, yaliyotota na yenye kuonesha ishara kama
yenye mafuta kwenye majani yaliyokomaa.
Makovu hukua haraka na yanaweza kufikia ukubwa wa 0.25-0.5 sm, huwa na rangi ya
kahawia/nyekundu. Umbo la makovu kwa kawaida huwa na pembe kwa vile hufuata umbile la
mishipa midogo ya majani. Makovu mara nyingi hutokea kwenye ncha na pembezoni mwa jani
ambamo unyevu huhifadhiwa. Katika hali ya ujoto/ukavu, majani huonekana yamechanika
chanika kutokana na maeneo ya pembezoni mwa majani na kati ya makovu hukauka na kukatika.
Ukubwa wa makovu huongezeka kutokana na muda ambao majani yanakuwa na maji. Kwenye
matunda, madoa huanza kwa kuwa na rangi ya kijani kibichi na kuonyesha sehemu kama
1: Madoa kutokana na Bakteria (Bacterial spot) (Xanthomonas
zilizotota maji. Kwa kawaida hufikia ukubwa wa 0.5 sm. Madoa haya hatimaye huwa yenye
mnyanyuko, rangi ya kahawia na yenye kukwaruza kwenye tunda la nyanya. Madoa haya kawaida
hufanya njia za kupenya aina nyengine za ukungu na bakteria wavamizi na kusababisha kuoza kwa
matunda.
UDHIBITI
Madoa ya majani yanayosababishwa na bakteria yakishaingia tu shambani au kwenye jengo la
kuoteshea mimea ni vigumu kuyadhibiti. Mbinu zifuatazo zinaweza kuchukuliwa kudhibiti
ugonjwa huu:
Mbinu bora za kilimo
Mbegu zisizo na vimelea vya magonjwa.Miche isiyo na magonjwa .Mzunguko wa mazao.Epuka maeneo yaliyopandwa nyanya kwa muda wa mwaka mmoja.Tumia miche iliyopasishwa.Ondosha shambani na choma moto mabaki ya mimea iliyoathirika na masalio.Safisha na kuua vimelea vya magonjwa katika vitalu kabla ya kusia mbegu.
Matumizi ya kemikali: Madoa yanayosababishwa na bakteria yanaweza kudhibitiwa kwa kutumia
kemikali zifuatazo; Acibenzolar (Actigard 50WG) Copper fungicides (Champ Dry prill, Champ
Formula 2, Copper-Count-N, Cuprofix MZ Disperss, Kocide, Kocide DF, Nordox, Tofix Dispress
Basic Copper) Copper/ EBDC/Zoxamide Mixtures, Cuprof ix Dispress MZ, Gavel, Mankocide)
Famoxadone/Cymoxanil (Tanos) na Streptomycin (Agri-strep).
Kibaiolojia: Virusi vinavyoshambulia bakteria hudhibiti magonjwa haya, lakini ni lazima viwekwe
shambani wakati wa jioni angalau mara mbili kwa wiki. Bakteria wa jamii ya Xanthomonas ambao
hawasababishi magonjwa hutoa udhibiti wa kiasi wa madoa yanayosababishwa na bakteria.
2: Mnyauko kutokana na bakteria (Bacterial wilt)
DALILI
Dalili za awali ni kunyauka kwa majani ya kwenye ncha. Baada ya siku mbili dalili hii huwa ni ya
kudumu, na mti wote hunyauka na kufa kutokana na kuendelea kwa ugonjwa. Matawi yote
hunyauka kwa wakati mmoja. Shina la mti ulionyauka likikatwa shehemu ya kati huwa na rangi
nyeusi na huonekana kama iliyotota maji.
Shina linapokamuliwa, hutoa maji ya utelezi kijivujivu unaotiririka. Hatua zinazofuata za ugonjwa huu ni kuoza kwa sehemu ya kati ya shina na hii husababisha uwazi katika sehemu hiyo.
Mzizi ulioathirika huoza na kuwa na rangi ya kahawia mpaka nyeusi. Mnyauko wa bakteria hausasababishi madoa kwenye matunda. Mmea hunyauka ukiwa na rangi ya kijani, (majani hayawi ya njano au kuwa na madoa) na inaweza kutokea ghafla.
Katika hali ya ugonjwa kusambaa taratibu, mti hutoa mizizi mingi juu ya shina na mmea hudumaa.
Kuanguka kabisa kwa mmea hutokea wakati nyuzi joto zinapofikia 320C au juu ya hapo.
UDHIBITI
Mnyauko unaosababishwa na bakteria unaweza kutambuliwa shambani kwa kukata sehemu ya
chini ya shina urefu wa 2-3 sm na kuisimamisha kwenye glasi ya maji. Ikiwa ugonjwa upo, basi
michirizi ya bakteria kama nyuzi hutoka kwenye kipande hicho cha shina sekunde chache tu baada
ya kukisimamisha kwenye maji.
Mbinu bora za kilimo
Mzunguko wa mazao na yale ambayo hayaathiriki.Usipande nyanya katika udongo ambao ugonjwa huu uliwahi kuwemo.Tumia aina za mbegu zenye kustahimili/zisizopata ugonjwa wa mnyauko bakteria. (Kama vileFortune Maker, Kenton na Taiwan F1).Toa na angamiza mimea iliyonyauka kutoka shambani kupunguza usambaaji wa maradhi.Ruhusu mafuriko yenye kuenea.Ongezea mbolea ya samadi.Panda katika msimu ambao si rafiki kwa ugonjwa huu.Zuia minyoo fundo (root-knot nematodes) kwani husaidia uingiaji wa ugonjwa.Changanya na mazao jamii ya kunde.Epuka kutumia ardhi kwa miaka 3-4 baada ya uzalishaji wa nyanya.
Kemikali: Mnyauko wa Bacteria unaweza kudhibitiwa kwa kutumia Chlorothalonil (Bravo
720/Ensign, Bravo Ultrex, Bravo Weather Stik, Echo 720, Echo 90DF, Echo Zn, Ridomil/Bravo).
Juu ya hivyo, tahadhari inapaswa ichukuliwe kuepuka usugu wa vimelea vya ugonjwa, hivyo mbinu
ya matumizi ya kemikali katika kuzuia ugonjwa inabidi ichanganye na mbinu nyinginezo.
Kibaiolojia: Kuzuia kunyauka kunakosababishwa na bakteria kunajumuisha matumizi ya ardhi
zenye kuzuia ugonjwa na ardhi zenye vimelea wapinzani (km. Candida ethanolica, Pythium
oligandrum).
2. Yanayosababishwa na Ukungu
DALILI
Dalili za ukungu mapema hutokea kwenye matunda, shina, na majani ya nyanya. Majani huonesha
madoa ya kahawia iliyokoza na yenye mfumo wa duara zenye kati moja. Madoa kwanza hujitokeza
kwenye majani yaliyokomaa na kuendelea juu ya mmea. Majani yenye madoa huweza kufa kabla ya
wakati wake na kusababisha kupukutika mapema kwa majani, matunda huungua kwa jua na kuwa
na rangi isiyopendeza.
Madoa ya kwenye matunda hujitokeza kwa juu kwenye ncha ya shina. Kwa kawaida madoa huwa
na rangi ya kahawia iliyokoza mpaka nyeusi, yaliyozama ndani, magumu na yenye duara za kipekee
zenye mfumo wa kati moja. Kuoza kwa chini ya shina huweza kutokea kwenye miche michanga.
Hali hii hujionyesha kwa kuzunguka shina sehemu ya chini. Miche iliyoathirika hudumaa na huweza
kunyauka na kufa. Miche mikubwa iliyoathirika huwa na makovu ambayo kawaida huwa upande
mmoja tu wa shina na hurefuka na kudidimia kwenye mashina na vikonyo. Dalili za ugonjwa wa
ukungu mapema mara nyingi hudhaniwa kuwa ni ukungu chelewa, lakini kwenye ukungu chelewa
makovu yamefifia, madogo na hayana alama za duara zilizonyanyuka.
UDHIBITI
Ukungu mapema unaweza kubainika shambani kwa kutafuta madoa ya kahawia iliyokoza ya kiasi
cha 1.2 sm kwa upana. Ni vigumu sana kuzuia ukungu mapema ukishaanza shambani. Njia
muhimu ya kudhibiti ukungu mapema ni kuzuia kuingia kwake na kusambaa.
Mbinu bora za kilimo
Zungusha mazao ya nyanya na nafaka ndogo ndogo, mahindi au jamii za kunde.Panda aina zenye kustahimili ‘early blight’. (Km. Floradade, Hytec 36, Julius F1 na Zest F1).Tumia mbegu safi.Limia na kufukia mabaki ya mazao baada ya mavuno na choma moto mazao yaliyoathirika natakataka zote za mazao.Epuka kumwagilia kwa juu.Ongezea mbolea ya samadi.Tumia matandazo kuzuia kurukia kwa maji.Hakikisha kupanda kwa nafasi sahihi na kufunga vijiti.Toa majani ya chini yaliyoathirika ili kuboresha mzunguko wa hewa.Epuka kutumia ardhi kwa angalau miaka 2 baada ya uzalishaji wa nyanya.
Kemikali: ‘Early blight’ inaweza kudhibitiwa kwa kutumia dawa za ukungu Boscalid ( Endura
Captan, Captan 4F, Captan 50), dawa za ukungu zenye shaba (Champ Dry Prill, Champ Formula 2,
Copper-Count-N, Kocide 101, Kocide DF, Kocide 4.5LF, Kocide 3000, Nordox Tri Basic),
Chlorothalonil na Chlorothalonil Mixtures (Bravo 720/Echo, Bravo Ultrex/Echo 90DF, Bravo
Weather Stik, Echo Zn, Ridomil Gold/Bravo), EBDC, Copper FBDC na EBDC/Zaxamide (Cuaprofix Disperss M2, Dithane/Gavel, Maneb 75, Manex, Mankocide, Manzate F1, Penncozeb 80W, Penncozeb 75DF), Famoxadone+Cymoxanil (Tanos, Fenamidone, Reason 500SC, Penthiopyrad,
Fontelis, Pyrimethanil, Scala), Strobilurin na Strobilurin Mixtures (Cabrio, Flint, Quadris)
Kibaiolojia: Kuna mazao mengi yatokanayo na mimea ambayo husemekana kuwa na sifa za sumu
kwa aina nyingi za ukungu.
Haya ni mazao asilia ambayo hupoteza nguvu zake haraka juu ya majani na kwenye udongo. Juu ya hivyo, taarifa kidogo sana zinajulikana kuhusu viwango vyao vya matumizi, athari zao juu ya viumbe marafiki, na binadamu.
4: Ukungu Chelewa (Late blight)
DALILI
Dalili za ukungu chelewa hujitokeza kwenye matunda, majani, shina na matawi. Kwenye majani
madoa ya kijani kibichi/kahawia hujitokeza upande wa juu wa majani, na pembezoni mwa
majani huwa kijani kibichi na huwa kama iliyotota, kwa kawaida madoa hutanuka ghafla hadi
majani yote yanapokufa. Nyakati za hewa ya unyevu, ukungu mweupe/kijivujivu hujitokeza
kwenye kingo za madoa katika sehemu za chini za majani. Wakati wa joto, sehemu
zilizoathirika huonesha kukauka. Madoa ya kahawia na yaliyorefuka hujitokeza kwenye
mashina.
Kwenye matunda, madoa ya kijivujivu/kijani yaliyotota hujitokeza kwenye nusu ya tunda
upande wa juu. Madoa haya baadae husambaa na kugeuka kahawia, yaliyokunjamana na
magumu. Wakati wa hali ya unyevu ukungu mweupe hujitokeza kwenye sehemu za matunda
yaliyoathirika. Dalili za ukungu chelewa mara nyingi hudhaniwa ni ukungu mapema (Alternaria
solani), lakini dalili za ukungu mapema mara nyingi huwa za duara zaidi, kubwa, na zilizokoza
na za duara zenye kati moja. Ukungu chelewa hauna duara hizi.
UDHIBITI
Nyanya zilizoambukizwa huweza kushambuliwa kwa haraka na kuteketezwa na ukungu
chelewa. Kuzuia ugonjwa huu ni shida sana ukishajiimarisha shambani. Njia muhimu sana ya
kuzuia ukungu chelewa ni kuhakikisha haijajiimarisha na kusambaa. Hii inaweza kufanyika
kwa kutumia mbinu zifuatazo:
Mbinu bora za kilimo
Zungusha mazao mengine kwa miaka 3 hadi 4.Tumia aina zenye kustahamili ugonjwa huu (km. Meru, Tengeru 97 na Shengena).Tumia mbegu safi.Ondoa mabaki ya mazao na choma moto mimea iliyoathirika na mabaki ya mimea.Tumia moto au mvuke kuua vimelea katika maeneo yaliyoathirika.Weka matandazo ya nyasi kuzuia kurukia kwa maji.Tumia zana safi baina ya mashamba.Hakikisha maji hayatuami na kuwe na mzunguko mzuri wa hewa.Toa majani ya chini yaliyoathirika kusaidia mzunguko mzuri wa hewa.Hakikisha kupanda kwa nafasi inayotakiwa.
Kemikali: Ukungu chelewa unaweza kudhibitiwa kwa kutumia dawa za ukungu za aina ya
mrututu (Champ Dry Prill, Champ Formula 2, Copper-Count-N, Kocide 101, kocide DF, Kocide
4.5LF, Kocide 3000, Kocide 6000), Cholorothalolin na Cholorothalonil Mixtures (Bravo
720/Echo 720, Bravo Ultrex/Echo 90DF, Bravo Weather Stik, Echo Zn, Ridomil
gold/Bravo),EBDC, Copper EBDC/ Zoxamide (Cuprofix MZ Disperss, Dithane, Gavel, Maneb
75 DF, Manex, Mankocide, Manzate F1, Penncozeb 80W, Penncozeb 75DF), Famoxadone +
Cymoxanil (Tanos, Fenamidone, eason 500SC) Strobilurin na Strobilurin Mixtures ( Cabrio
Flint Quadris).
Kibaiolojia: Mpaka hivi sasa hakuna dawa ya kibaiolojia inayo weza kudhibiti/kuzuia ukungu
chelewa.
Kadi 4: Ukungu Chelewa (Late blight) (Phytophthora infestans)
Kadi 5: Mnyauko kutokana na Ukungu

USISAHAU KUDOWNLOAD APPLICATION YA KILIMO BORA IPO PLAY STORE

                                      DOWNLOAD HAPA SASA

                     

No comments:

Post a Comment