Kumbukumbu
Mfugaji anashauriwa atunze kumbukumbu za chanjo na matibabu ili zimsaidie kujua yafuatayo:
- Muda sahihi wa kuanza chanjo na kurudia chanjo.
- Idadi ya kuku wanaotakiwa kuchanjwa muda wa kuchanja ukifika.
- Kiasi cha dawa kinachohitajika (dozi) kuandaliwa.
- Aina ya chanjo inayohitajika kulingana na magonjwa yanayojitokeza mara kwa mara.
Kushirikiana
Udhibiti wa magonjwa kwa njia ya chanjo unahitaji nguvu ya pamoja ili kupata matokeo mazuri. Ni vizuri wafugaji kwenye eneo moja wakishiriki kupanga mkakati na kusimamia utekelezaji wa suala zima la uchanjaji. Umuhimu wa kuchanja kuku kwa wakati mmoja katika eneo ni muhumu ili kudhibiti ugonjwa kwa wakati mmoja. Mfugaji anayeamua kuchanja azingatie ratiba ya chanjo ya ugonjwa husika ili kuweza kupata matokeo mazuri
No comments:
Post a Comment