KILIMO BORA CHA MTAMA - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Thursday, September 7, 2017

KILIMO BORA CHA MTAMA

KILIMO BORA CHA MTAMA


MTAMA-SORGHUM (Sorghum vulgare)



1.UTANGULIZI

 Mtama ni kundi la mbegu punje ndogo katika jamii ya nafaka ambayo ina kiasi kikubwa cha kabohaidreti.Ni zao lenye uwezo mkubwa wa kuvumilia hali ya ukame kuliko mazao mengi ya jamii yake,Hivyo hulimwa maeneo mengi Duniani yenye mvua Pungufu na hata yenye mvua za kutosha.Ni moja ya zao ambalo likitumika vizuri husaidia kwa kiasi kikubwa kukabliana na mabadiliko ya hali ya nchi na pia katika vita ya kuzuia njaa.Mtama hutumika Kama vile unga wa ugali,kupikia mikate ya mtama,kupika ubwabwa wa mtama,Unaweza kuchemshwa na Kuliwa (mnyoma-lugha ya kiasili),Viwanda vya bia kutengeneza bia,Pia majani na mabua yake yanaweza kutumika kama chakula cha mifugo,na pia mabua Makavu yanaweza kutumika katika kujengaea uwa .

2.HALI YA HEWA IFAAYO
Mtama ni zao linaloweza kustahimili ukame.Hivyo unaweza kulimwa na kukua kuanzia ukanda wa chini wa bahari 0 - 100 mita hadi Mwinuko wa mita 1500.pia unaweza kulima zaidi ya hapo lakini pasiwe na baridi kali mtama haukubali seheme zenye baridi.Huitaji kiasi cha mvua cha wastani wa milimita 300 - 800 za kwa mwaka ili uweze kukua vizuri.Mtama hukubali sehemu zenye joto hivyo huitaji nyuzi joto 18 - 33 °C.

3.ARDHI IFAAYO KWA KILIMO CHA MTAMA
Mtama unapenda ardhi ambayo haituamisdhi maji na mwingine unavumila katika ardhi inayotuamisha maji kidogo,hivyo kwa mavuno mazuri usipande katika ardhi ambayo hutuamisha maji kwa ajili ya kupata mavuno bora,kama ni udongo wa mfinyanzi hakikisha maji hayasimami shambani kwa muda mrefu ikinyesha mvua.Mtama hukubali katika kichanga chenye rutuba au mchanganyiko wa mchanga na mfinyanzi au mfinyanzi.Hukua vizuri katika udongo wenye soil PH  5 - 9.

4.MAANDALIZI YA SHAMBA
Andaa shamba lako mapema kabla ya msimu wa kupanda mtama kuanza.Shamba lisafishwe na kulima kwa jembe la mkono,jembe la kukokotwa na Ng'ombe au trekta  na pia unaweza kupanda bila kulima (zero tillage).

5.MBEGU BORA ZA MTAMA
Zipo aina mbalimbali za mtama na mbegu zake.Aina hizi hutofautiana kulingana na rangi zake,nyekundu,kahawia,nyeupe ambazo zinajumuisha aina zaidi ya 20 za mtama duniani.Pia mtama na aina zake huwa kuna ambao ni mtama mchachu (Hasa mbegu za kahawia na nyekundu),mtamu  hasa Rangi nyeupe.Wakulima wengi hupendelea mtama mweupe.Pia mtama wa mbegu sa kisasa huwa laini kuliko mbegu za asili ambao ni mtama mgumu.Mtama wa asili huwa ni mbegu ndefu kwenda juu na huchukua muda mrefu kupanda hadi kuvuna kuliko mtama wa kisasa ambao mwingi ni mfupi na huchukua muda mfupi zaidi na hutoa mavuno bora zaidi ya mtama wa asili.
AINA HIZO NI KAMA VILE;
               1.SEREDO
 Hii ni aina nyingine yenye punje za kahawia, na inapendekezwa Kulimwa kwenye eneo lenye mwinuko wa mita 1,500 kutoka usawa wa bahari. Aina hii huchanua baada ya siku 71 na hukomaa katika kipindi cha siku 120. Aina hii huwa ni ndefu, na ina uwezo wa kuzalisha Tani 2  kwa ekari moja. Ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa wa milia, kutu, mabaka kwenye majani, na madoa ya kahawia kwenye majani.
                 2.SERENA na DOBBS.
  Aina hii huwana  punje za kahawia. Aina hii hustawi kwenye eneo lenye mvua za wastani na hukomaa katika kipindi cha siku 110. Aina hii huwa na shina na mizizi imara, ambapo huweza kuzalisha kiasi cha Tani 1.5 kwa ekari moja. Ambapo zinahitajika kilo 5 za mbegu kwa hekari moja. Aina hii ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa milia, kutu, na madoa ya kahawia kwenye majani.
           3.GADAM
 Hufanya vizuri katika sehemu ambazo si kame sana. Katika nchi nyingi mfano Kenya, aina hii ya mtama hutumika kutengenezea bia na pia kwa chakula. Aina hii huvumilia bungo na ugonjwa wa majani.
                 4.HAKIKA NA WAHI
 Hizi ni aina mbili za mtama ambazo zimezalishwa na kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga kwa ajili ya kuoteshwa kwenye mashamba yalioathiriwa na viduha. Mbegu hizi zina rangi ya manjano iliyopauka. Unga wa aina zote mbili zinafaa sana kwa kupika ugali.
                   5.PATO na MACIA
Hizi hutoa mbegu nyeupe laini na hufaa kwa ugali na hata kwa unga wa Dona (kusaga bila Kukoboa)
                          6.MBEGU NYINGINE
Tegemeo,Lulu,Sandala,Imani.
                7.MBEGU ZA ASILI
Huchukua muda mrefu kupandwa hadi kuvunwa.Zaidi ya siku 120

6.UPANDAJI WA MTAMA
Mtama upandwe moja kwa moja shambani katika mashimo katika kina cha sentimeta 2.5 hadi 5.Kiasi cha mbegu kupanda inategemea nafasi na aina ya mbegu unayopanda na aina ya upandaji,Mbegu ambazo hupndwa kwa nafasi ndogo ndogo huchukua kiasi cha kg 2.5 hadi 5 na ule ambao hupandwa kwa nafasi kubwa huchukua Kg 2.5 - 3 kwa ekari
NAFASI ZA UPANDAJI
kwa mtama wa asili tumia Sentimeta 70 kwa 30 au Sentimeta 80 kwa 30 ,kwani huu huwa ni mrefu zaidi kwenda juu na pia katika shina acha miche 2 au 1 ambao huwa na afya zaidi.
mtama wa kisasa tumia nafasi ya sentimeta 60 kwa 15 au 60 kwa 20
Muda wa kupanda mtama ni pale msimu wa mvua unapoanza kulingana na siku za mtama wako kupandwa hadi kuvunwa ili kuuepusha kuvuna katika kipindi cha mvua.Pia mtama wa asili ukipanda mapema zaidi unaweza kukusumbua kwa kupata tatizo la kuanguka kipindi ambacho mvua huwa nyingi zaidi.Hivyo usipande mapema sana msimu wa mvua unapoanza.
KILIMO MSETO -unaweza kuchanganya mtama na mazao mengine japokuwa kama ni kilimo cha biashara haishauriwi kufnya hivyo.unaweza kuchanganya mtama na mazao kama vile Kunde,maharage,choroko n.k

7.PALIZI
Palizi ya mtama ifanyike mapema mara tuu mtama wako unapoona unaanza kushambuliwa na magugu.Kipindi cha mwanzoni mimea ya mtama huitaji hali ya usafi zaidi kuliko unapokuwa mkubwa hivyo huitaji kupaliliwa mara mbili kupandwa hadi kuvunwa.
Pia kama katika shimo kuna miche zaidi ya miwili inabidi ipunguzwe mapema tuu katika palizi ya kwanza.Pia unaweza kupalilia kwa kutumia Dawa maalum za palizi za Magugu ambazo uantakiwa uwe mwangalifu usipulize katika mtama mdogo au katika majani ya mtama wako.

8.MBOLEA
Mtama unaweza kuvumilia katika shamba lenye rutuba kidogo lakini hustawi zaidi katika shamba lenye rutuba ya kutosha.hivyo unaweza kutumia mbolea za samadi katika kupanda au mbolea za viwandani kama vile DAP au TSP na kukuzia mbolea za CAN au UREA kiasi cha kg 50 kwa ekari.

9.WADUDU NA MAGONJWA
WADUDU
Mtama hushambuliwa zaidi na ndege (Quelea) Kwelea kwelea.Pia Funza wa Mabua na wadudu wengine ambao unaweza kuwazuia kwa kupuliza dawa za wadudu kama vile DUDUBA, .Ndege unaweza kutumia mbinu mbalimbali za kufukuza au kama ni wengi kuwasiliana na kitengo cha udhibiti wa ndege kwa msaada zaidi.
MAGONJWA.
Ugonjwa mkuu wa mtama ni KUTU (smuts) ambapo unaweza kuzuia kwa kupuliza dawa za ukungu.
10.UVUNAJI WA MTAMA NA MUDA WA KUKOMAA
Mtama huchukua siku tofauti za kupandwa kukomaa hadi kuvunwa kulingana na aina ya mbegu uliyopanda Kwa kawaida huchukua siku 120 - 150 Mtama mrefu na siku 115-120 Mtama Mfupi.Mtama ukishakomaa na kukauka huvunwa kwa kukatwa masuke yake kwa kisu kikali kwa mtama mfupi na kuangushwa chini na kukatwa masuke kwa kisu kwa mtama mrefu.Pia ili kuuwahisha kuvuna mtama unaweza kukata mabua yake na kuulaza chini shamabani hadi utakavyokauka vya kutosha.Kisha baada ya kukauka masuke yake hupigwa kwa fimbo au magongo katika turubai safi au sakafu ya sementi ili kuutenganisha na masuke yake,Pia kuna mashine maalumu za kufanya kazi hii.

11.KUHIFADHI
Mtama ukishavunwa na kukaushwa vizuri huifadhiwa katika magunia maalum ambayo hayaruhusu wadudu kupenya na kuharibu mtama au kwa kutumia magunia ya kawaida ambapo mtama kabla ya kuwekwa huchanganywa na dawa maalum za wadudu kama vile Akteliki au SHUMBA.Yahifadhi magunia yako katika sehemu kavu isiyo na unyevu.
MTAMA kwa kawaida ukilimwa vizuri hutoa wastani wa Tani 1 hadi 2.5 kwa ekari

SHUKRANI-Nashukuru kwa ushirikiano wako nataraji hili litakuwa lenye manufaa kwa kilimo chako cha mtama.

Kwa mahitaji zaidi ya ushauri wa kilimo wasiliana na
ABDALLAH UMANDE
0769429140
umande11@gmail.com
http://ift.tt/2eQ1r5C


from KILIMO BIASHARA http://ift.tt/2j9C8Nd
USISAHAU KUPAKUA / KDOWNLOAD APPLICATION MPYA YA KILIMO CHA KISASA IPO PLAY STORE SASA BUREE KABISA

No comments:

Post a Comment