MAGONJWA YA MIFUGO, DALILI, KINGA NA TIBA SEHEMU YA 2 - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Sunday, October 8, 2017

MAGONJWA YA MIFUGO, DALILI, KINGA NA TIBA SEHEMU YA 2

Kama ulikosa kuona gonjwa la kwanza unaweza kuangalia na kusoma kwa kubofya  HAPA

MASTITIS
Huu ni ugonjwa wa kuvimba kiwele na chuchu kitaalam huitwa (iflamation of udder or mamary gland) na hii usababishwa na maambukizi ya viumbe wadogo (micro organisms).

VICHOCHEZI
Mastitis Inaweza mkuchochewa na vitu vifuatavyo
  • usafi wa banda
  • usafi wa kiwele
  • mkono wa mkamuaji au mashine
  • umahili wa mkamuaji
  • majeraha katika chuchu au kiwele
  • kuwepo kwa magonjwa mengine mfano FMD

HATUA ZA MASTITIS
Kuna haina mbili za mastitisi ambazo ni

CLINICAL MASTITIS
Hii huziilishwa na uvimbe na unaweza kua
  • ukishika hua ngumu
  • maumivu makali
  • kubadilika kwa rangi katika chuchu
  • chuchu kulika
B.KUBADILIKA KWA MAZIWA
Maziwa hubadilika na kua 
  • na usaa
  • damu
  • au kuganda


 SUB CLINICAL MASTITIS
Katika hatua hii maziwa hua kawaida na chuchu hua kawaida lakini hua na upungufu wa maziwa kwa asilimia kubwa.

KUTAMBUA UGONJWA
Utambuzi wa mastitis hutegemea na hatua ya maambukizi lakini maziwa hupimwa maabala ili kugundua kama kunamaabukizi ya ugonjwa huu.

TIBA
  • Kwa kuchomwa sindano, kama hali imekua mbaya unaweza kuchomwa sindano za    antibiotic kupunguza na kumaliza kabisa 
  • udder infusion, njia hii dawa huwekwa ndani ya chuch baada ya kusafishwa na kuondolewa maziwa na usaa.
  • direct intral parechimal injection, hii hutumika katika chuchu zilizo lika saa.
 
kuna njia nyingi za kutibu mastitis lakini hizo ni baadhi ya mbinu wasiliana nasi kufahamu zaidi kwa kubofya HAPA

KINGA
Zifuatazo ni kinga za mastitis
  • kuosha chuchu na kiwele  kwa kutumia dawa
  • usafi wa banda na mazingira
  • epuka kuacha maziwa ndani ya chuchu
  • kamua kwa umakini


 



    USISAHAU KUPAKUA / KUDOWNLOAD APPLICATION YA KILIMO BORA IPO PLAY STORE ILI UPATE HABARI KWA URAHISI BONYEZA LINK HII KUDOWNLOAD ==> http://ift.tt/2tqvrGF

    No comments:

    Post a Comment