VIFARANGA NYAMA ANZA /BROILER STARTER, VIFARANGA NYAMA KUZIA, VIFARANGA MAYAI ANZA/CHICK MASH, KUKU MAYAI KUZIA/GROWER, KUKU MAYAI TAGA /LAYER MASH, NGURUWE WATOTO, NGURUWE KUKUZIA, NGURUWE NENEPESHA, NA NG'OMBE MAZIWA
Kwanza ifahamike kuwa kuna formular nyingi Sana unazoweza kuzitumia kwa lengo la kutengeneza chakula cha mifugo yako lengo tu ni uweze kupunguza angalau gharama za uendeshaji wa mradi wako, Hapa mimi nawapa mojawapo ya formular hizo na faida ya kujua kuchanganya chakula peke yako nyumbani ni kupunguza gharama za kununua chakula cha kiwandani, uweze kutumia malighafi zinazopatikana eneo lako nk.
Ili kuweza kufikia huko unahitaji vitu ama malighafi utakazozitumia ili ziweze kukupatia virutubisho vikuu anavyohitaji mfugo wako ili aweze kukuzalihishia unachokitaka na virutubisho hivyo ni proteins, vitamins, madini, fat, na carbohydrates.
Malighafi tutakazotumia hapa ni pumba mahindi =carbohydrates, Mashudu alizeti=protein+fat, dagaa sagwa=protein+madini, chokaa mifugo=madini, and madini mchanganyiko/premix=madini na chumvi=madini.
CHAKULA CHETU TUTAKACHOTENGENEZA NI CHA KILO 100.
VIFARANGA NYAMA ANZA /BROILER STARTER
Pumba mahindi.... 76kg
Mashudu alizeti.... 12kg
Dagaa sagwa........ 10kg
Premix... .................0.5kg
Chokaa mifugo..... 1kg
Chumvi sagwa......0.5kg
VIFARANGA NYAMA KUZIA
Pumba mahindi 76kg
Mashudu alizeti 15kg
Dagaa sagwa 7kg
Premix 0.5kg
Chokaa mifugo 1kg
VIFARANGA MAYAI ANZA
Chumvi sagwa 0.5kg
Pumba mahindi 76kg
Mashudu alizeti 16kg
Dagaa sagwa 5kg
Premix 0.5kg
Chokaa mifugo 2kg
KUKU MAYAI KUZIA
Chumvi sagwa 0.5kg
Pumba mahindi 80kg
Mashudu 12kg
Chokaa 2kg
Dagaa 5kg
Premix 0.5kg
KUKU MAYAI TAGA
Chumvi 0.5kg
Pumba 80kg
Mashudu 14 kg
Dagaa 3kg
Premix 0.5kg
Chokaa 2kg
NGURUWE WATOTO
Chumvi 0.5kg
Pumba 76kg
Mashudu 15 kg
Dagaa 6kg
Premix 0.5kg
Chokaa 2kg
NGURUWE KUKUZIA
Chumvi 0.5kg
Pumba 78kg
Mashudu 15kg
Dagaa 4kg
Premix 0.5kg
Chokaa 2kg
NGURUWE NENEPESHA
Chumvi 0.5kg
Pumba 80kg
Mashudu 15kg
Dagaa 2kg
Premix 0.5kg
Chokaa 2kg
NG'OMBE MAZIWA
Chumvi 0.5kg
Pumba 80kg
Mashudu 17kg
Chokaa 2kg
Chumvi 0.5kg
Premix 0.5kg
NOTE PALIPOANDIKWA PREMIX, HIZI HUWA ZINAUZWA MADUKA YA MIFUGO SASA UTAKACHOFANYA KAMA KUKU WAKO NI WA MAYAI NA WAPO KWENYE UMRI WA GROWER UTANUNUA GROWER PREMIX, KAMA WANATAGA UTANUNUA LAYER PREMIX, HIVYO HIVYO KAMA NI WA NYAMA UTANUNUA BROILER PREMIX, KAMA NI NG'OMBE UTANUNUA CATTLE PREMIX, NA KAMA NI NGURUWE UTANUNUA PIG PREMIX
Pia sehemu yenye Pumba mahindi unaweza usiweke tu pumba yenyewe bali unaweza kuchanganya pumba nusu na paraza nusu kwa mfano kama pumba imeandikwa 76kg unaweza kugawa nusu 38kg ikawa pumba na hiyo 38kg nyingine ikawa paraza lakini iwe tu ni kwa kuku isiwe kwa nguruwe au ng'ombe, na pia sehemu yenye chokaa unaweza ukagawa ikawa chokaa na mifupa sagwa ukifanya hivi chakula chako kitakua vizuri zaidi.
KUKU KIENYEJI/BATA
UJAZO NI KILO 50.
Pumba mahindi 38kg
Mashudu 7kg
Mifupa/chokaa 2kg
Dagaa 2kg
Chumvi 0.5kg
Premix 0.5kg
Mwisho wa somo la 4
I'm interested thank u
ReplyDelete