UFUGAJI WA KUKU: MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUTUNZA VIFARANGA - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Monday, April 10, 2017

UFUGAJI WA KUKU: MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUTUNZA VIFARANGA



ZINGATIA HAYA WAKATI WA KUTUNZA VIFALANGA.

Habali wafugaji leo ni siku nyingine tena, tukiendelea na masomo mbalimbali yanayo husu ufugaji kuku. Kwa kawaida kulea vifalanga ni changamoto kwa wafugaji wengi, hivyo huamua kununua kuku wakiwa wakubwa na pale vifalanga vinapototolewa. Huwaachia kuku wawatunze vifalanga hao. Mfumo huu ni

(1) UTUNZAJI WA ASILI : Njia hii hutumika kwa vifalanga wachache ambao temba huachiwa kulea vifalanga vyake. Wakati temba anapo walea utagaji hukoma, hivyo huchukua muda mwingi huyo kuku kuja kutaga tena.
Mfugaji kibiashara ni lazima ufuge kibiashara kwa mfumo wa

(2)KUWA KUTUNZA VIFALANGA KWA KUTUMIA CHANZO CHAJOTO:
Kulea vifalanga cha kwanza cha kuzingatia ni
Mfumo huu wengi wanauona kuwa ni mgumu kutokana na kushindwa kuutumia na hatimaye vifalanga kufa. HUU NI UTANGULIZI TU MFUGAJI KALIBU KATIKA SOMO HILI LA LEO. BANDA BORA.
Vifalanga hawahitaji eneo kubwa sana katika majuma manne ya kwanza.Nafasi inayohitajika kwa kukadiria ni meta 1 ya mraba kwa vifalanga 16. Kwa mfano nyumba yenye meta 10 za mraba inatosha kwa vifalanga 160 hadi kwa umri wa majuma manne. Vipimo vya nyumba yenye eneo kama hili inaweza kuwa na hatua 5 kwa 4. Utajenga banda kutegemea na eneo ulio nalo.
VYOMBO KATIKA NYUMBA YA KULELE VIFALANGA. (1)KITALU/BROODER/BRUDA : Brooder ya kukuzia vifalanga inatakiwa iwe ya mduara isiyopinda mahali ni vizuri kutumia silingboard, au mbao, kwanini inatakiwa iwe ni mduara ; tunafanya ivo kwa ajili ya kuzuia wasilundikane kwenye kona ndio maana mzunguko wa brooder unatakiwa kuwa ni mduara.Kwa maeneo ya kijijini brooder unaweza kutengenezea kwa kutumia viloba vya magunia.Ndani ya brooder hiyo ndio kuna kuwa na chanzo cha joto unaweza tumia , jiko la mkaa, balbu, au chemli.
_Vifalanga vitalia kwa fulaha
Katika banda la Vifalanga ni muhimu kuwa na joto lisio kithiri hasa pale kwenye siku za mwanzo na nyakati za usiku.Mwanga na mzunguko wa hewa ndani ya bruda ni muhimu kwani huvutia na kuvishawishi vifaranga kuanza kula . Weka madirisha makubwa yenye kuingiza hewa safi na kutoa ile chafu. Banda lisilo na hewa ya kutosha huchochea kuenea kwa magonjwa ya mfumo wa hewa. Andaa nafasi ya kutosha ili kuepuka vifaranga kurundikana. UTATAMBUAJE KUWA JOTO LIMEZIDI AU LIMEPUNGUA. (1)Kama joto linatosheleza utaona yafuatayo. _Vitakimbia kimbia _Vitakunywa maji _ Vita chagua chagu na kuonesha shughuli nyingi zote ni dalili zuri za kuonesha kuwa joto linatosheleza. (2)Kama joto halitoshelezi utaona yafuatayo.
Tukumbuke kuwa kuna magonjwa yanayo ambukiza kupitia Yale maji wanayo kunywa vifalanga wako hivyo kwakuhakikisha usalama wa maji utakuwa umewanusuru vifalanga wako dhidi ya magonjwa hayo.
_Vifalanga wakiona baridi hujikusanya kalibu sana na chanzo cha joto. _Au hujikusanya wenyewe kwa pamoja na kulia kwa sauti. Dalili hizi huonesha kuwa joto ni pungufu hivyo kuna ulazima wa kuongeza joto. (3)Kama joto limezidi utaona yafuatayo _ Vifalanga hukaa mbali na chanzo cha joto. _Husinzia na kuzubaa _ Kama ni kwenye Chumba vifalanga hukimbilia mlango ili vipate upepo. Katika hali hii ni dalili za kuonesha kuwa joto limezidi hivyo unatakiwa kupandisha taa juu , kupunguza vyanzo vya joto na kuwapa vifalanga maji mengi. VYOMBO VYA KUWEKEA MAJI. Vifalanga wanahitaji maji katika kuwapa maji hakikisha kuwa hayo majina ni safi unaweza ukayachemsha kisha ukayachuja kama utakuwa na wasi wasi nayo.
Lakini kuna wengine wao huamua kuwa mwagia vifalanga chini chakula mlemle wanapo lala. Hii ni hatari kubwa kwa vifalanga hao kuambukizana Magonjwa kiurahisi. Kwani kinyesi cha kifalanga kinacho umwa kikichanganyika kwenye hiko chakula , halafu akaja kifalanga mzima akala chakula hiko kuna uwezekano wa kuambukizwa ugonjwa kiurahisi sana.Hapo ndio utakuta Mtu vifalanga wake wanaumwa coccidiosis, amewapa dawa hawaponi. Atajiuliza kwanini hakuna cha kwanini hapo hiyo ni kwasababu banda lako , matunzo yako ni mabaya banda lako limekuwa banda la maambukizi wala sio uponyaji tena.
Unaweza kununua vyombo vya kuwekea maji drinkers, lakini kwa vifalanga ni vema katika hayo maji yaliomo kwenye drinkers ile sehemu ya kunywea uweke kokoto safi ndogo ndogo ili kuwafanya vifalanga wasilowe wakati watakapo kuwa wanakunywa maji. Kama hauna uwezo wakununua drinker basi unaweza ukatumia njia yeyote ya kutengeneza chombo cha kuwekea maji ila hakikisha kuwa hakivuji maji. Hakikisha kuwa banda ni safi na kavu wakati wote ili kuzuia malazi kwani chanzo cha maambukizi kutokana na unyevunyevu pia. VYOMBO VYA KUWEKEA CHAKULA. Wafugaji wengi hutumia feeders kuwalishia vifalanga wao chakula. Nawengine hutengeneza vyombo mfano wa feeders kwa kulishia vifalanga wao . Yote ni sawa ila chamuhimu ni kuzingatia usafi wa hivyo vyombo. Sifa za banda bora. _Banda lenye kuingiza hewa safi na ya kutosha _Banda lenye kuingiza mwanga wa kutosha _Banda lenye kuzuia upepo mkali _Banda lisio ruhusu maji kusimama na kuingia ndani na kwamba liwe imara. _Banda liwe rahisi kusafishwa _Banda liwe na eneo la kutosha kulingana na idadi ya Kuku.
Ufugaji mwema.
_Banda liwe sehemu salama , kwa wezi na wadudu .
Ahsante

No comments:

Post a Comment