JIFUNZE MBINU ZA KISASA ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA MAYAI PAMOJA NA CHANJO ZAO - KILIMO NA UFUGAJI

Latest

Karibu uweze kujifunza na kujipatia elimu kuhusiana na kilimo na ufugaji ambapo utajifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji pia utajifunza dondoo mbalimbali na mbinu bora na za kisasa za ufugaji

Wednesday, May 10, 2017

JIFUNZE MBINU ZA KISASA ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA MAYAI PAMOJA NA CHANJO ZAO

                                     Image result for chicken farming


KANINI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA MAYAI PAMOJA NA CHANJO


 🌀Siku ya 1 Wape:glucose siku ya 2 _6 wape otc changanya na vitamin.Changanya aminovit  kwenye chakula (kilo 1 kwa mfuko 1 wa kg 50) kuanzia wiki ya kwanza hadi ya 4.

🌀Siku ya 7: Chanjo ya newcastle - masaa 2 tu, weka maji na vitamin mara baada ya kutoa maji ya chanjo.

🌀Wiki ya pili: Chanjo ya gumboro - masaa 2 tu ukisha Toa maji ya chanjo utawapa maji yenye vitamin (utailudia tena baada ya miezi 3)

🌀Wiki ya tatu: Chanjo ya Newcastle tena.

🌀Wiki ya nne: Hakikisha kuku wako wanakuwa katika dose kubwa ya vitamin pamoja na otc.

🌀Wiki ya sita: Wape kuku wako maji ya vitamin asubuhi na matupu jioni.

🌀Wiki ya saba _ nane:Wape kuku wako chanjo ya ndui.( Hii chanjo ni ya sindano)
Baada ya siku kazaa utawapa  dawa ya minyoo (piperazine au lekiworm) Dawa ya minyoo utakuwa unaludia kuwapa kila baada ya miezi 3

🌀Wiki ya kumi na mbili:   Wape chanjo ya newcastle masaa 2 tu kisha utabadili maji na kuwa wekea maji yenye vitamin (utaludia kila baada ya miezi 3)

🌀Wiki ya kumi na sita:  Kata midomo kisha wape neoxyvital kwa siku 3-5 andaa viota.

🌀Wiki ya 54: Wape virutubisho vyenye kuongeza wingi wa mayai mfano glp (kilo 1 kwa kila kilo 50 za chakula, kwenye maji usikose kuwa wekea vitamin

🌀Wiki ya 72: Tumia v-rid kusafisha mabanda ili kuua vijidudu pia weka maji ya dawa hii kwenye dish ya kusafishia miguu (footbath) ili kuhakikisha udhibiti wa vijidudu (biosecurity) na kwamba vifaranga wanaowekwa hawaathiriwi na vijidudu hivyo.

🌀Wiki ya 96: Ondoa kuku wote waliozeeka.


⚠KUKU WA MAYAI ILI WATAGE VIZURI.⚠

✍✍Kuku wa mayai ili watage vizuri wanatakiwa walishwe chakula bora kwa utaratibu unaotakiwa, ukiwazidishia au kuwaongezea hawatotaga vizuri. Wanatakiwa walishwe kati na kati kulingana na umri kama ifuatavyo:-
UMRI WA WIKI 1 -2
Katika umri huu wanapewa chakula aina ya “Super Starter” kwa ajili ya kuwatengenezea kinga mbadala ili waweze kuhimili mikiki mikiki ya vijidudu vya magonjwa kadri wanavyoendelea kukua, wanapewa chakula hicho kwa kiwango maalum kama ifuatavyo:-
Wiki ya 1: Gramu 12 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 2: Gramu 22 kwa kuku mmoja kwa siku moja
UMRI WA WIKI 3 – 8
Hapa wanakuwa bado ni vifaranga na wanapewa chakula aina ya “Chick Starter” kwa ajili ya kuendelea kuwajenga miili yao waweze kupoekea virutubisho vizuri, hii inatokana na kwamba kuna baadhi ya viinilishe vinafanya kazi ya kumeng’enya chakula na kupatikana viinilishe vingine, kwahiyo vikikosekana katika mwili wa kuku basi hata wale chakula gani bora, hawawezi kutoa mazao bora, lakini kwa kuwapa “Chick Starter” itawapelekea kuwa na virutubisho hivyo muhimu. Kiwango na ulishaji wake ni kama ifuatavyo:-
Wiki ya 3: Gram 27 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 4: Gram 32 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 5: Gram 38 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 6: Gram 42 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 7: Gram 46 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 8: Gram 50 kwa kuku mmoja kwa siku moja
UMRI WA WIKI 9 – 18
Katika umri huu kuku wanapewa chakula aina ya “Grower Mash” kwa ajili ya kuwakuza na kuwajenga mfumo wa uzazi kwa maandalizi ya utagaji. Kiwango cha chakula kinategemea na wiki kama ifuatavyo:-
Wiki ya 9: Gram 56 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 10: Gram 62 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 11: Gram 64 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 12: Gram 66 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 13: Gram 68 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 14: Gram 74 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 15: Gram 74 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 16: Gram 80 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 17: Gram 82 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 18: Gram 88 kwa kuku mmoja kwa siku moja
UMRI WA WIKI 19 – 40
Huu ni umri ambao kuku wanataga kwa kiwango kikubwa sana (85% hadi 100%) hali ambayo inawafanya kutumia nguvu nyingi mno, hivyo hupewa chakula aina ya “Layers Phase 1” kwa ajili ya kufidia nguvu ya ziada wanayotumia ili waendelee kutaga kwa kiwango hichohicho. Ulishaji wake ni kama ifuatavyo:-
Wiki ya 19: Gram 92 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 20: Gram 102 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 21: Gram 108 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 22: Gram 114 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 23: Gram 116 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 24: Gram 120 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 25 – 40: Gram 130 kwa kuku mmoja kwa siku moja
UMRI WA WIKI 41 – 80
Katika umri huu kuku wanakuwa wameanza kuchoka na huanza kutaga kwa kiwango cha kawaida (65% hadi 75%) hivyo hupewa chakula aina ya “Layers Phase 2” kwa ajili kuendeleza (maintain) kiwango chao hicho kwa muda mrefu. Kiwango chao ni “Gram 130 kwa kuku mmoja kwa siku moja”.

Nb: ✍Kwa wafugaji wa kuku wa mayai (layers) kwa wakati huu wa baridi ni lazima uongeze ratio ya chakula kama ulikuwa unawapa grm120 basi ongeza grm10 Zaidi au wafungie mapanzia ili wasipunguze kutaga kwasababu ya baridi⚠

Katika ufugaji kuku kibiashara ni lazima udhibiti magonjwa , kuna magonjwa yenye chanjo na yasiyo na chanjo hivyo hakikisha kuku wako unawapa chanjo ili uwakinge na magonjwa hatari kama mdonde.


ENDELEA KUTEMBELEA BLOG HII KILA SIKU ILI UJIFUNZE MENGI ZAIDI.

No comments:

Post a Comment