ndugu wasomaji napenda kuwaletea aina nyingine ya mbegu ya maharage ambayo ni bora na nzuri kwa kupandwa kwa maeneo yote yanayokubali zao hili. Mbegu hii ilifanyiwa uchunguzi kwenye chuo cha uchunguzi wa mbe UYOLE Mbeya na kuruhusiwa kwa ajili ya kilimo ndani ya jamii
BILFA 16
Mbegu hii ya maharage ni nyekundu yenye vichirizi vichiriz vyeupe kwa mbali hukua kwenye uwanda uliombali na bahari usawa wa800-2000 kutoka baharini. mbegu hii hukua haraka na huzaa maharage yenye rangi nyekundu na huwa na matawi kuanzia 4-6. Mbegu hii hutoa maua ya pink vishuba au vikoba vyeupena vikikomaa huwa na rangi ya maziwa
KIASI CHA MBEGU NA UZALISHAJI
Mbegu hii nyekundu hupandwa kilo 70-80 kwa hekta moja ambayo ni sawa na ekari mbili na nusu.mbegu hii huzaa vizuri pia ila inamapungufu ukilinganisha na uyole 04 ambayo ni sawa na miche 205000. kwa hekari moja unapata tani 1.4-1.6 za maharage yaliyoko tayari kama utayalima kitaalam
Ni vyema kufanya palilizi mapema ili kuyapa maharage sapoti nzuri katika ukuaji wake. ili kupata mavuno mazuri pia ni vyema tuka hudumia vizur zao hili kwa kupuliza dawa pale wadudu wanapoanza kushambulia mimea.
MDA WA KUPANDA NA KUVUNA
Mbegu hii ya maharage hupandwa mwezi wa 3 kama mvua zikiwahi na endapo mvua zitachelewa hupandwa mwezi wa nne. Maharage haya huchukua siku 110 kukomaa hadi kuvunwa. Wakati maharage yanapokauaka tu ni vyema kuvunwa ili kukwepa hasara ya kupasukapasuka ovyoo shambani.
No comments:
Post a Comment