MRADI WA KILIMO CHA MATANGO
Matumizi: Matango hutumika kama tunda, ijapokuwa ni aina ya mboga na huongeza vitamin A, C na maji mwilini. Pia, tango linaweza kutumiwa kama saladi wakati wa mlo.
Hali ya hewa: Matango hustawi kwenye hali ya joto, hali kadhali kwenye sehemu yenye joto kidogo pia hustawi. Matango yanahitaji joto wastani wa nyuzi joto 20°C – 25°C. Zao hili pia huhitaji maji kwa wingi, ingawa unyevu ukizidi husababisha magonjwa kwenye majani na maua.
Udongo: Kwa ustawi mzuri wa matango,udongo unatakiwa kuwa na rutubaya kutosha, na chachu ya kuanzia 5.5hadi 6.7, mwinuko unaotakiwa nikuanzia mita 1000-1200 kutoka usawawa bahari Tofauti na ilivyo mazao mengine, matango hayahitaji mwanga mkali sana kwa kuwa husababisha maua dume kuzaliwa, hivyo kuathiri uzalishaji wa idadi ya matunda ya matango. Mwanga kidogo husababisha maua jike kuchanua kwa wingi kuongeza kiwango cha mazao. Mwanga unapokuwa mwingi, inabidi kutumia neti au aina nyingine ya vizuizi ili kupunguza mwanga, ambapo pia itasaidia kulinda mmea dhidi ya upepo mkali ambao unaweza kuharibu maua na matunda, au mmea kwa ujumla.
Kupanda: Mara nyingi matango hupandwa moja kwa moja shambani. Wakulima wengine hupanda kwenye vitalu au makopo na baadae kuhamishia miche inapofikia sentimita 8-12. Endapo mbegu zimepandwa shambani moja kwa moja, inatakiwa ipunguzwe na kubakia mche mmoja tu kwenye kila shimo
Nafasi: Nafasi kati ya mche na mche ni sentimita60-70, na nafasi kati mstari namstari ni sentimita 70-90. Mimea inatakiwaiwekewe miti ili iweze kuzaamatunda mengi na kuepuka kukaachini ambapo matunda yanaweza kuoza au kuharibiwa na wadudu.
Mbolea: Mbolea ni muhimu sana, kabla yakupanda au kuhamisha miche. Mbolea inayoweza kutumika ni samadi au yaviwandani isiyokuwa na madhara kwamazingira na afya ya binadamu. Baadaya kupanda, tumia mbolea ya maji majikila baada ya siku 14-21, mpaka mmea uweke matunda
Palizi: Palizi ni muhimu, ili kuepuka magonjwa na kunyang’anyana chakula kati ya zao na magugu.
Wadudu waharibifu: Wadudu waharibifu wa matango ni pamoja na Vidukari, inzi weupe, na minyoo ya mizizi.
Magonjwa: Magonjwa yaliyozoeleka kushambulia matango ni pamoja na Ukungu, fusari, na magonjwa ya virusi. Dawa aina ya KARATE itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda na FUNGICIDE itasaidia kwa mashambulizi ya fangasi.
Kuvuna: Matango yanaweza kuwa tayari kuvunwa kuanzia siku 50-60 na matunda yanatakiwa yawe na urefu wa sentimita 15 mpaka 20. Makadirio ya mavuno ni tani 6 kwa ekari moja. Ni vizuri kuwekea matango fito kwani matunda yake yakilala ardhini huoza.
from FUGA KIBIASHARA http://ift.tt/2BbEVJS
No comments:
Post a Comment